Watanzania wapige kura bila kufikiria kura za maoni

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,377
3,823
Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuhusu matokeo ya maoni ya wananchi kuhusu uchaguzi wa October 2010. Matokeo ya utafiti yaliyotolewa na REDEt na Synovate yalimpa ushindi mkubwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM Mh. Dr. Kikwete. Sitaki kusema kama utafiti ulikuwa na kasoro au la kwa sababu hayo ni ya kitaalamu zaidi.
Ninalotaka kuwaasa Watanzana ni kuwa habari hii inaeweza kuathiri ‘turn-up’ siku ya ya kupiga kura. Kwa sababu baadhi ya wapiga kura wanaweza kusema kumbe mshindi kashajulikana ya nini. nijisumbue?’ Pia matokeo ya ucaguzi yatakapotoka inawezekana tafsiri yake ikaleta usumbufu au rabsha ikiwa yatakuwa na tofauti kubwa na hizi findings. Kuna uwezekano mkubwa ripoti hizi zikawakatisha tamaa baadhi ya wapiga kura “This is a psychological reality!’ kwa kujua hilo nawaomba watanzania wenzangu tupige kura bila kufikiria kura hizo za maoni. Tafadhali tusiache kupiga kura October 31
 
Back
Top Bottom