Watanzania wanaipa sana Credit CCM..hadi inaudhi!

Pamoja na ushindi huu mnono.. bado tuna haja ya kukaa chini na kutafakari.. Kura 26000 walizopata wapinzani wetu(CCM) wamezipataje? tufanye nini ili Chaguzi zijazo CCM iambulie 0! lengo ni kuikomboa nchi come 2015
 
Maybe there is a reason watu hawaamini !; A zebra never changes its stripes.. (na jambazi ni jambazi tu..) asipoiba sio kwamba kaacha bali kabanwa...

Therefore issue sio kuacha kuwaogopa / kutokuwaamini bali issue ni kuhakikisha hawapewi upenyo wa kufanikisha wizi wao..



"If you know your enemies and know yourself, you will not be imperiled in a hundred battles; if you do not know your enemies but do know yourself, you will win one and lose one; if you do not know your enemies nor yourself, you will be imperiled in every single battle." Sun Tzu
 
Kufuta miaka 50 of constant abuse is not an easy task. Ni vigumu kuamini you are trully free from the hands of that serial abuser. Watanzania wako kwenye process of regaining thier confidence.
 
Way to go man. Wanachokifanya CCM siku zote ni kupenyeza hofu ndani ya mioyo ya wananchi. Na kinachowasaidia kushinda mara nyingi ni kutumia hofu hiyo kupiga bao
 
MM, Ule mkwara wako kuwa kama cdm itapoteza arume east viongozi wate wajiuzulu umesaidia kidogo! Japokuwa Samsoni alikujibu kiaina lakini pia mkwara ule ulifanya vichwa vya viongozi wetu kutafuta njia nyingine ya kulinda kura! lakini kwa kusema ukweli mpango wa uchakachuaji ulikuwa wa hali ya juu! hata mie mwenyewe siamini tumewezaje kuwadhibiti kwa kiasi kile duuu! ilikuwa ni noma mzee.
 
Pamoja na ushindi huu mnono.. bado tuna haja ya kukaa chini na kutafakari.. Kura 26000 walizopata wapinzani wetu(CCM) wamezipataje? tufanye nini ili Chaguzi zijazo CCM iambulie 0! lengo ni kuikomboa nchi come 2015


Ha ha ha ! hizo lazima ziwepo ccm ni taasisi ina watu kila sehemu wanayoitumikia na wanaishi kwa kuitegemea sasa hao 26,000 ni wale wote wenye maslahi na ccm.
La muhimu hapa ni kuwawin au kuwapata wale wote ambao hawafungamani na upande wowote ambao ndiyo wengi sasa mpango uwe tutawapata vipi hawa.
 
Pasco Mayalla yuko online? maana huyu jamaa njaa itamuuwa......aje sasa kutueleza ni nani mshindi Arumeru?
 
Kwa wale waliotazama mfululizo wa sinema tatu (Trilogy) za The Lord of the Rings (The Fellowship of the Ring, The Two Towers na The Return of the King) wataona kuwa CCM imekuwa ikitishia watu kama mzimu wa Sauron. Watu watapambana lakini akifika Sauron majeshi yote yanaangukia mikononi mwake. Mwisho wake ilibidi ateuliwe mtoto mdogo dhaifu Frodo (Joshua Nassari) ili akaitupe pete ya uchawi ya Sauron. Alipitia wakati mgumu sana hadi kufanikisha Aragon (Watanzania) kuwa mfalme (The Return of the King).

Hivyo nikifananisha matukio ya mfululizo huu:
  1. The Fellowship of the Ring: Nassari, Vicent Nyerere, Mbowe, Slaa, Lwakatare, wafuasi wote wa CDM na Watanzania kwa ujumla waliunda Fellowship (Umoja) ili kuuangusha mzimu wa Sauron (CCM)
  2. The Two Towers: Ni mapambano makali katika kata mbalimbali (Towers) za Arumeru Mashariki. Wakati mwingine Frodo (Joshua Nassari) alipata mashambulizi makubwa ambayo baadhi yetu yalitupa hofu juu ya kufanikiwa mission yetu. Gandalf the Grey (Mbowe, Slaa etc) alikuwepo na farasi (Helkopta) kusaidia mapambano katika hatua ambazo zilionekana ni ngumu sana.
  3. The Return of the King: Battle is seriously fiercer now. Frodo gets so close to the victory but Gollum (Tume ya Uchaguzi, TISS, Tendwa, Rushwa, Polisi etc) anajaribu walau kwa dakika ya mwisho kuchelewesha ushindi. Hatimaye pete ya uchawi (hofu juu ya CCM) yatupwa, na Aragon (Watanzania) awa Mfalme.

I highly recommend these films. The Lord of the Ring is 5th highest grossing film in history behind Avatar, Titanic, Harry Potter and the Deathly Hallows Part 2 na Transformers: Dark of the Moon.

Tusiidharau CCM. Tusiipe credit sana CCM. Tulinde kura hata hivyo.

Movement for Change,
Movement for Chadema.

THE LORD OF THE RINGS: THE RETUN OF THE KING!!!
 
Mkuuuuu nimekupata nipo mstari wa mbele.
Najihaadaa kwenda kulikomboa jimbo la bukoba vijijini.
 
Wanasahau CCM ni chama kama vyama vingine!
timu yenye usajili mzuri,mazoezi na uongozi thabiti ndio hutwaa ubingwa..kama ni ukongwe basi
Wapi Cosmo,mseto na nyota nyekundu
 
..Jana tarehe 01/04/2012, mwandishi nguli na mwanaharakati, ndugu Adam Lusekelo alikuwa anatimiza mwaka toka afariki. Ilikuwa niandike kitu cha kumkumbuka, lakini nilikuwa safarini, sikuweza. Ushindi wa Arumeru kwa CDM, ni zawadi kwa wapenda mabadiliko. Naamin huyu ndugu yetu huko kaburini anageuka kwa furaha!
 
Bado kuna kazi kubwa sana ya kuuelimisha umma wa watanzania ya kuwa wao ndiyo wenye nchi. Wao ndiyo wenye mamlaka na viongozi wapo ili kuwatumikia wananchi, kwa ridhaa wanayopewa na wananchi. Watanzania wengi bado wana ile kasumba ya kuwaona viongozi ni miungu midogo.

Hii dhana nadhani ilitokana na kuwa na chama kimoja kwa muda mrefu, na watu kufikiri ya kuwa chama ndicho kinachowafanya wao (watanzania) wawepo, badala ya kuona ya kuwa wao (watanzania) ndiyo wanaokipa chama na serikali dhamana ya kuongoza. Na iwapo viongozi hawawezi kuwatumikia wananchi, basi wananchi wana kila haki ya kuwaondoa!

Kutokana na kutokufahamu nguvu kubwa waliyonayo, wananchi wengi wanafikiri ya kuwa haiwezekani kuiondoa ccm. Hawawezi hata kufikiri kuwa Tanzania bila ccm inawezekana, na ya kuwa ccm siyo serikali. Tanzania inaweza kuwa na serikali inayofanya kazi vizuri sana, na isiwe serikali ya ccm.

Kazi kubwa ninayoiona mbele yetu ni sisi tuliofumbuka macho na kulielewa hilo kufanya kazi ya ziada kuwaelimisha watanzania wenzetu juu ya ukweli huu. Nadhani kutokana na ushindi mkubwa wa CHADEMA huko Arumeru, kuna watu watakaoanza kufunguka. Hata hivyo haitoshi. Tuna budi sote kuendelea kutoa elimu ya uraia kwa wengine ili kila mtu aelewe umuhimu wake katika kuleta mabadiliko ya kweli na maendeleo kwa Taifa letu. Vilevile changamoto hii tuvipe vyama vyote vya siasa kujitahidi kuwafikia wananchi huko majimboni, hususan vijijini na kutoa elimu ya uraia ili wananchi wetu wajue nguvu yao.

Tazama, Arumeru wamenong'ona, bila kelele, lakini nchi imesikia!
 
Wananchi wakifunguliwa na kujiamini hakuna lolote CCM inaweza kufanya kushinda uchaguzi wowote mdogo kuanzia sasa. Watanzania mjiamini!! Watu pekee ambao hatuwezi kuwasaidia kwa kweli ni wa Dar tu.
 
Wananchi wakifunguliwa na kujiamini hakuna lolote CCM inaweza kufanya kushinda uchaguzi wowote mdogo kuanzia sasa. Watanzania mjiamini!! Watu pekee ambao hatuwezi kuwasaidia kwa kweli ni wa Dar tu.
Mwisho wa Ubunge wa Makongoro Mahanga ni mwezi wa 5, subili kwa mara nyingine tena utaisikia sauti ya wakazi wa jimbo la Segerea.
Ila nakubaliana na wewe CCM haikustahili kuwa na hata mbunge mmoja kwa hapa Dar es salaam.
 
Wananchi wakifunguliwa na kujiamini hakuna lolote CCM inaweza kufanya kushinda uchaguzi wowote mdogo kuanzia sasa. Watanzania mjiamini!! Watu pekee ambao hatuwezi kuwasaidia kwa kweli ni wa Dar tu.

Taratibu MM, Dar kubwa hii. Wengine tuko ubungo na wengine Kawe.
 
Wananchi wakifunguliwa na kujiamini hakuna lolote CCM inaweza kufanya kushinda uchaguzi wowote mdogo kuanzia sasa. Watanzania mjiamini!! Watu pekee ambao hatuwezi kuwasaidia kwa kweli ni wa Dar tu.

Japo watu wa DAR pia wamegawanyika..Naomba DAR unayomaanisha iwe, ILALA,KIGAMBONI,UKONGA,TEMEKE,KINONDONI na siyo UBUNGO au KAWE..huku walau kuna watu wana spirit kama za Mbeya, Mwanza, Musoma, Arusha, Kagera, Kilimanjaro etc.
 
Kama kuna vitu vimeniudhi jana ni hili la Watanzania kuuiona CCM kila mahali kama jinamizi fulani hivi. NImewaambia matokeo hayabadiliki watu "what if what if!". Imefika mahali CCM ikikohoa watu wanapiga magoti na kuamkia "shikamoo". Matokeo yalikuwa yanajulikana kwa mtu yeyote ambaye angetaka kuyajua masaa zaidi ya kumi na mbili kabla. Lakini watu wakabakia kufikiria "labda watachakachua". Well, kuchakachua kunawezekana unapowapa credit mno; ni kana kwamba huweiz kuwazuia.

Makamanda wa CDM na wengine waliofanya kazi ya ajabu ya counter intelligence na vijana ambao hawakuchoka waliamini CCM inaweza kuzuiwa na vyombo vyake kupigishwa marktime. Wananchi wasiogope ving'ora na saluti, wasiogope kelele na TBC; kinachozungumza ni kura tu!! Ndio lugha pekee ambayo watawala wanaielewa!

Jamani CCM ni wananchi kama sisi!!! fungukeni; msiidharau wala kuudharau uwezo wake lakini msiifanye kana kwamba ina nguvu fulani ya Kimungu! HAINA. Arumeru Mashariki wamethibitisha.

Wacha na miye nipumzike.

Mzee mimi sikuwa na 'IF' yoyote kwako, infact nilitumia nafasi hiyo kuwaconvice wenzangu tuliokuwa bize na vituo vya TV kwamba sasa kazi imekwisha, twendeni tukasherekee..and that is what we did..mpaka night kali kuanzia muda ule wa around nne kasoro baada ya tangazo lako..sikupenda kuwa Tommaso.....Ballot Box ndiyo Kila kitu
 
Back
Top Bottom