Elections 2010 Watanzania wanachotaka ni ukweli na ukweli mtupu siyo porojo

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Jana waziri wa nishati na madini William Ngeleja alikaririwa navyombo vya habari akisema kwamba Tanzania inapata kati ya asilimia 30-40 ya thamani ya mauzo ya dhahabu na siyo asilimia 3 kama alivyosema Dr.Slaa wakati wa mdahalo. Ninalotaka kusema ni kwamba; Ngeleja kama waziri mwenye dhamana ya rasilimali hiyo anazo takwimu halisi za ni kiasi gani cha madini hayo kimekuwa kikichimbwa mwaka hadi mwaka, kimeuzwa kwa kiasi gani cha fedha na kati ya fedha hizo serikali inaambulia nini. Sasa basi kinacho mkataza waziri huyo kutoa takwimu hizo ili kila mmoja ajiridhishe ni nini? Ikumbukwe mh.Ngeleja amekuwa na tabia ya usanii wakati anapokuwa akishughulikia masuala muhimu ya kitaifa. Nakumbuka wakati wa mjadala wa mgodi wa Kiwira; Mh.Ngeleja alitoa maelezo ya kuwa bei ya T.sh 700 million zilizokuwa zimetolewa na TANPOWER SUPPLY Ltd kwaajili ya kununua asili 70 ya mgodi huo zilikuwa sahihi eti kwasababu mtaji wa mgodi huo ulikuwa T.shs 1 billion. Wakati anayasema hayo alijua fika ya kuwa mgodi huo tayari ulikuwa umefanyiwa tathimini na kugundulika ya kwamba thamani yake halisi ilikuwa kati ya T.shs 4-7 billion. Hii ina maana katika vitabu vya hesabu vya mgodi huo kulikuwepo na kitu kinachoitwa "capital reserve". Capital reserve hiyo ambayo ni sawa na tofauti kati ya thamani ya mgodi na mtaji uliokuwa umetolewa, ilitakiwa ama ilipwe kwa wenye mali kwanza au igeuzwe mtaji kabla mgodi haujabinafsishwa. Kwakuwa jambo hilo lilikuwa halikuzingatiwa wakati Kiwira inabinafsishwa ina maana katika zoezi hilo TANPOWER SUPPLIES Ltd iliwaibia Watanzania zaidi ya T.shs 4 billion. Na waziri Ngeleja ameshiriki kwenye wizi huo kwa kuficha ukweli huo.
 
Back
Top Bottom