Tatizo si wananchi, tatizo ni mfumo wa uchaguzi hautoi mwanya kwa wananchi kufanya maamuzi. Hii ni hatari sana kama wananchi wanakosa imani na system nzima ya uchaguzi. Tungekuwa na chaguzi huru na haki watu wengi wangeshiriki. Lakini tatizo lingine linalofanywa na Tume ya uchaguzi ya CCM ni voters supression. Ku-scramble majina ya wale wanaoonekana kutowaunga mkono ni moja ya njia pekee iliyobaki ya kupunguza hamasa ya wapiga kura. Mtu hawezi kuwa anahamishwa vituo uchaguzi baada ya uchaguzi bila ridhaa yake. Tume inabandika majina siku moja kabla mtu anatoka kwake na kufika kituoa alichopigia kura uchaguzi uliopita bila mafanikio. Hii ni demotivation factor kubwa sana ya ushiriki wake uchaguzi ujao.
2015 inaweza kuwa worse zaidi.
Ndio maana wasomi wanalilia katiba mpya ambayo rais atakuwa na madaraka machache na bunge kupewa madaraka mengi. Ila vile vile katiba mpya inayorohusu kila mmoja wetu afaidi keki ya nchi yetu. Na sio wachache ndio wanakula nchi hii lakini wengi wanabakia mafukara. Binafsi naunga mkono katiba mpya ila SIO KWA MTAJI WA KISIASA. Katiba mpya isimamiwe na wasomi ambapo taaluma itumike katika kuitunga. Vyenginevyo tutapata KATIBA MBOVU BADALA YA KATIBA MPYA.