Watanzania waliotorosha fedha nje kufilisiwa!

Kwa Tanzania ya sasa na sisiemu ya leo sidhani kama kuna kiongozi yeyote mwenye utashi wa kisiasa wa kuzuia pesa haramu zisitoroshwe. Wanaotorosha pesa hizo kwenda katika nchi tajiri sio kwamba 'sirikali' haiwafahamu, wanafahamika sana tu na huenda hata Mhe Meghji anawajua. Sema sasa Mhe Meghji anatoa kauli hii utadhani anaongea na watoto wa shule za awali, ambao hawajui maana ya utoroshaji wa fedha. Ina maana sheria za namna hii hatunazo tangu zama na zama kweli? Mimi ninavyojua ni kwamba Benki Kuu wana utaratibu wao maalum wa kuratibu pesa zote zinazoingia na kutoka nchini, pamoja na kujua baadhi ya vyanzo vyake na kujua wahusika. Pia mabenki yote nchini yana taratibu za namna hii, ikiwa ni pamoja na kuripoti taarifa hizi katika Benki kuu.
Aliyokuwa anayasema Mhe Mrema miaka ya tisini kuwa pesa zilikuwa zinasafirishwa kwenda nje ya nchi katika vifungashio vya majani ya chai ni zipi? Si ndo pesa hizi haramu ama?
Hawa wanasiasa waache usanii, tushawagundua sana.
Anyway, siku zao zahesabika!
 
Kuna Vigogo Wengine Watoto Wao Au Ndugu Zao Wamejilipua Nje Na Wanawatumia Pesa , Sasa Kwa Sababu Wanauraia Wa Nchi Zingine Serikali Imeshafikiria Njia Zaidi Ya Kushugulikia Watu Hawa Kama Ndio Wanaotumiwa Na Baba Zao Walio Ndani Ya Tanzania Kutorosha Pesa

Kusema la ukweli mpaka sasa waTZ waliojilipua niliokutana nao ng'ambo ni wengi sana wabeba maboksi na kwao mambo sio mazuri ndio maana wakaamua kujilipua nje na maisha yao kwa kweli wengine sio hata mazuri kulinganisha na wasomi walio bongo, most of them hela wanayopata wanaitolea jasho na mara nyingine wanawatumia ndugu zao fedha TZ sio fedha kutoka TZ kwenda kwao.

Sasa badala ya kufuatilia mavitu bongo wakati ndio watu wanaporomosha majumba na kutafuna fedha kikwelikweli, itakuwa ni danganya toto kufuatilia watu waliojilipua. Haya ni maoni yangu.
 
naona hapa meghji ana cheza kombolela na viongozi wenzake.yaani kila siku wanabadilisha misemo tu vitendo hakuna,kweli mwaka wa harasa ni hasara tu.jk rudi kwa mganga wako ukajiangalie tena.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom