Watanzania waishio Ughaibuni: Haki ya Kupiga Kura

alibaba

Senior Member
Jun 24, 2009
185
43
Mh: Mama Balozi Tanzania House London.
Mh: Waziri Mkuu, Dar es salaam.
Mh: M/Kiti Tume ya Uchaguzi, Dar es salaam.

Wapendwa WanaJF na Watanzania kwa jumla.

Kutokana na Utandawazi ulioenea Kiteknolojia ambao umesaidia kurahisisha mambo mengi hasa katika sekta ya Mawasiliano, nadhani wakati umefika kwa Watanzania wanaoishi Ughaibuni kushiriki katika uchaguzi mkuu na kutumia Haki yao ya kidemokrasia, kwenye Uchguzi wa Rais wa Jamhuri.

Wanajamvi naomba kuwasilisha hoja.
 
Si jambo baya lakini wakisema watu waende na vitambulisho vyao sijui itakuaje?
 
Naamini ni jambo linalowezekana, na bila shaka kitambulisho cha Utanzania wako kitahitajika, Hvyo wale ambao utanzania wao hauna utata waanze. na wale wenye utata utaratibu utafutwe wa kuweza kuwasaidia waweze kutekeleza haki hiyo.
 
tusianze na negativity..naamini watanzania wengi wako safi kwani ni wanafunzi ambao wana haki kikatiba kupiga kura tuwajadili hao ili wapate haki yao na wengine wengi tu hawana matatizo hayo mnayojaribu kuyakuza tujadili hii hoja kwa upeo mzuri na nia njema kwa nchi yetu kwani wakati sasa umefika kuona watanzania wenye exposure wataamua vipi kama watapewa haki ya kupiga kura ughaibuni>>!!!!
 
Mh: Mama Balozi Tanzania House London.
Mh: Waziri Mkuu, Dar es salaam.
Mh: M/Kiti Tume ya Uchaguzi, Dar es salaam.
Wapendwa WanaJF na Watanzania kwa jumla.

Kutokana na Utandawazi ulioenea Kiteknologia ambao umesaidia kurahisisha mambo mengi hasa katika sekta ya Mawasiliano, nadhani wakati umefika kwa Watanzania wanaoishi Ughaibuni kushiriki katika uchaguzi mkuu na kutumia Haki yao ya kidemokrasia, kwenye Uchguzi wa Rais wa Jamhuri.
Wanajamvi naomba kuwasilisha hoja.

Ni wazo zuri sana ila ili serikali ikubali ni lazima ihakikishiwe kuwa mtawapigia kura CCM na siyo Upinzani. Cha kufanya ni kununua fulana za kijani kwa wingi ili wapitishe maamuzi ya kuruhusu. Vinginevyo hilo litakuwa halina maslahi kwa Taifa(a.k.a maslahi ya CCM) kama wao walivyozoea kutuambia
 
Hofstede,
Na kazi ndio hiyo , kukielewesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Wakati wa Kupinduliwa unakaribia au kwa uhakika Umewadia.
 
Ndugu wanaJF, watanzania wenzangu,
Kuna aya moja ya maandiko matakatifu huwa naipenda na kuiamini sana, inasema hivi; Haki huinua Taifa.
Nimeikumbuka sana aya hii hususan wakati huu ambapo taifa letu limeufikia tena mwaka wa uchaguzi mkuu. Natamani haki itendeke kwa asilimia mia katika jambo hili. Nafurahi pia kwamba katika salamu za mwaka mpya Rais wetu amelieleza taifa juu ya nia ya serikali anayoiongoza kuhakikisha kuwa uchaguzi tunaouendea utakuwa huru na wa haki. Kinachonifurahisha si kwamba nina uhakika Mkuu wa nchi ataisimamia pasi shaka kauli yake (maana alishasema nyingi, na zimebaki kuwa maneno tu) . Nafurahishwa na ukweli kwamba kwa kauli yake tutampima, na kwa kauli hiyo hiyo tutasimama kudai haki itendeke.
Mojawapo ya haki ambazo hazijawahi kutendeka nchini Tanzania katika chaguzi zote kuu zilizopita, ni haki ya watanzania walioko mahabusu, na watanzania waishio nje ya nchi kupiga kura kuwachagua viongozi wa taifa lao. Haki hii ipo kihalali katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 5 inayosema; kila raia wa Tanzania aliyefikisha umri wa miaka 18 anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania na wananchi isipokuwa kama; mtu huyo ana uraia wa nchi nyingine, mtu ana ugonjwa wa akili, ametiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai, ameshindwa kuthibitisha au kutoa kitambulisho cha umri, uraia au uandikishaji kama mpiga kura. Aidha, kwa mujibu wa Ibara ndogo 5 (1) na (2) raia wote waishio nje ya nchi walio mahabusu, wanaotumikia vifungo chini ya miezi sita, wagonjwa na walemavu wana haki sawa na raia wengine ya kupiga kura kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Raia hao hawawezi kupiga kura za Wabunge wala madiwani kwa kuwa wanaishi nje ya majimbo na kata zinazofanya chaguzi huo.
Iliwahi kusemwa katika vyombo vya habari na kusikika bungeni, kwamba mnamo mwaka 2006, akiwa nchi Namibia Rais Kikwete aliwaahidi watanzania waishio nje ya nchi kwamba; 2010 watapata haki yao ya kupiga kura.
Ni wakati wa Rais kukumbuka ahadi yake hii, ni wakati wa watanzania walioko nje ya nchi na mahabusuni (magerezani) kutambua haki yao hii na kuidai kwa nguvu zote.
Ni wakati wa kumwambia Rais na wahusika wengine hivi; Mheshimwa Rais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa ujumbe huu wa wazi natumia haki yangu na wajibu wangu kudai haki hiyo itendeke sasa. Timiza ahadi yako ili haki ipate kushamiri na kuliinua taifa letu.
 
kwa 2010 nadhani mkakati kwa walio nje ni kujiandalia nauli na kurudi nyumbani kupiga kura. vinginevyo sioni serikali ikiwezesha upiga kura nje ya nchi mwaka huu.

labda wekeni nguvu ya kudai angalau daftari la uandikishwaji lifunguliwe kila ubalozi ili anagalau baadhi waweze kujiandikisha na hatimaye kufunga safari kwenda kupiga kura. vinginevyo itabidi kufunga safari mara mbili moja kwenda kujiandikisha (na kama hapo kituoni hakutawekwa zengwe) na ya pili kwenda kupiga kura.

inasikitisha lakini ndio ukweli wenyewe
 
kama haki hiyo ikipatikana tumshukuru Mungu. lakini muhimu turudi nchini mwetu tusaidiane na wenzetu kujenga taifa letu.

malimbukeni wa kuishi ng'ambo hawatosheki, wanadai haki ya kupiga kura na wakati huohuo wanataka uraia wa nchi mbili ili wapie kura kotekote!

tuache visingizio, turudi nyumbani.
 
Kahangwa
Nakubaliana na hoja yako lakini tatizo la nchi yetu ni teknolojia na wizi wa kura unaofanywana CCM na uzembe unaofanywa na vyama vya upinzani hata kuibiwa kura na CCM. Kama haki hii ikipataikana basi wapinzani watanedelea kuibiwa sana.
 
jana nimesoma blogu ya ndugu yetu michuzi na kukutana na mada nzito sana inayohusiana na watanzania ughaibuni kupiga kura. sina uhakika hii inawezekana. je katiba ya sasa itaruhusu hii kufanyika? wakenya, wa nigeria, sierra leone walio nje ya nje ya nchi watapiga kura. je tanzania tutaweza?

nimeshindwa kukopy na kupesti. mwenye uwezo atusaidie Sosi: Can Diaspora Vote in 2015
 
Hao wakimbizi wabaki huko huko. Watarudi hapa na kututia kichefuchecu kama ndugu yao Ledemuz sijui big show......huyo kiongozi wao sijui yohana mashaka kwanza ni mrundi siyo mtanzania
 
Uchaguzi mkuu wa kenya 2013 march, umethibitika kuwa utafanyika kielectronic kama ule wa marekani ili kuondoa marumbano ambayo mara nyingi yamakuwa yakisababisha vurugu na machafuko makubwa nchini humo.

Je, tanzania kuna uwezaekano wa kutumia njia hii ktk uchaguzia 2015, njia ambayo inaaminika kuwa ni ya ukweli na inayoondoa uwezekano wa matatizo ktk kupiga kura?. Njia hii ni nzuri sana kwa sababu upigaji kura unapokamilika saa 12.00 jioni, matokeo huonekana saa 12.01 jioni hiyo hiyo, pia inaokoa garama nyingi sana
 
Mkuu Hilo liko mbiyoni wahisani wa maendeleo wameifanya Kenya pilot ikifanikiwa tu inakuwa replicated bongo kwa gharama zao.wamechoka uchakachuaji wa viongozi wenye uchu wa madaraka. Stay tune.
 
walete hyo bongo ila utackia ucjakachuaji ndo utazd maana wale wakijani wana mamluki yao
 
walete hyo bongo ila utackia uchakachuaji ndo utazd maana wale wakijani wana mamluki yao
 
Kwa mujibu wa kajarida ka kenya nilikokasoma, hakuna kabisa uwezekano wa kuchakachua, couse kila anayepiga kura lazima awe na kitambulisho cha taifa cha kisasa achana na vile vya kizamani kama vya kitanzania ambavyo mtu yoyote anawezajitengenezea
 
Aisee kufananisha Kenya na Tanzania ni sawa na kufananisha kifo na usingizi.....

We still have a long way to go.......
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom