Watanzania waishio nje ya nchi

kamkoda

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
396
71
Leo asubuhi hii nimesikia waziri fulani akisema wanataka takwimu za watanzania waishio nje ya nchi ili waweze kukusanya mapato yao na kupigia upatu kwenye katiba uraia wa nchi mbili...wazo hili sio baya

Je waziri huyu anafahamu ukweli huu?

1. Makampuni mengi yaliyopo ndani hayalipi kodi vizuri zaidi ya 'paye'
2. Wageni wa nje waliopo ndani wengi wanavibali feki. Mapato yao hayajakusanywa.
3. Wageni wengi waliopo chini pia hawastahili kuwepo nchini kwa kuwa hawana sifa hizo, ni mibaka uchumi.
4. Kodi nyingi ya sekta isiyo rasmi ama inayopotea kwa ujanja ujanja wa wachache ni karibu mara tatu kuliko ile inayokusanywa.
5. Wageni walioingia nchini kama wataalamu na kujivua gamba kuwa wawekezaji wamulikwe, wao wanawajua kwa kuwa ni wezi.
6.Ahakikishe wanapiga kura uchaguzi ujao wa 2015 kabla ya kutamani mapato yao.

Ningemshauri afanyie kazi hayo hapo juu kwanza kuliko kuvaa soksi wakati amekwisha vaa kiatu.
 
Halafu hao watanzania wanaishi nje wengi wanalipa kodi huko huko walipo...Nahisi itakuwa kama kuwaongea mzigo..anyway kama alivosema mleta hoja hata hapa kuna wakwepaji wa kodi na hawajabanwa.
 
Huyo waziri ni mtupu, kwanza abadilishe safu ya uongozi TRA make akina kitilya hawajui cha kufanya kila mwaka kodi iliyoanzishwa na baba wa taifa huongeza asilimia na kukaa maofisini kama mazezeta, wakati wigo wa kodi ni mpana sana hawa wahuni wanao jifanya wawekezaji na kufanya biashara bila kulipa kodi mbona hawawagusi? viongozi wetu wengi wanafikilia kwa kutumia viuno tu wamelewa vyeo.SAD
 
Pia kuna amabao wanaingia nchini kwa gia ya NGO , then baadae unashangaa eti ni wawekezaji!
 
Umesema waziri fulani bila shaka unamjua,mtaje tumchambue kinyumenyume tumecmhoshwa na viongozi uozo! inase
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom