Watanzania waibuka kidedea mbio za Olimpiki Marathon! - wafanikiwa kumaliza hadi mwisho kabisa

kichwat

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
1,819
587
Hatimaye hayawi hayawi YAMEKUWA baada ya Watanzania wawili kufanikiwa KUMALIZA mbio za Marathon katika siku ya mwisho ya michezo ya Olimpiki, London 2012.

Hiyo ni baada ya mkimbiaji wetu mahiri Mussa Faustine kushika nafasi ya 33, huku mwenzake Ramadhan Samson akifanikiwa kushika nafasi ya 66 kati ya wakimbiaji 85 waliomaliza mbio hizo.

Kama kawaida yetu, sote tujumuike pamoja kuwapongeza vijana wetu kwa KAZI KUBWA waliyoifanya ya kufanikiwa kumaliza mbio hizo za Km 42 (yaani zaidi ya tripu 10 za Ubungo-Mwenge kwa kupitia Sam Nujoma).

Wahenga walisema KUMALIZA NI JUHUDI, KUSHINDA MIPANGO YA MUNGU. (ingawa kwa mtaji huo basi Mungu atakuwa na upendeleo kwa wenzetu).

...Wapi Gida Buday!

kwa matokeo kamili bofya hapa: http://www.london2012.com/athletics/event/men-marathon/index.html?v=20120812-214304762
 
Hamna kitu hapo kushindwa na kuboronga hakuna tofaut na serikali ya ccm kushindwa kuongoza kwa hili ndungu nasema ni rabbish n foolish
 
Aiseeeere baba yangu tusiwalaumu wakimbiaji,tazizo sio hao tatizo ni jei kei mi nawakiki chichiemu ikingika madarakani mpira 2tafika mbali mahakama itatenda haki,wanafunzi watafaulu, wasanii wanufaika,,lakini kama kiongozi wao alie madarakani mbumbumbu hakuna kitachoeleweka kamwe hacha niishie hapo

nipate mbege nikalale
 
Kwani walikwenda kumaliza kukimbia au kushinda? Hili ndilo tatizo kubwa tulilo nalo watanzania. Tunapenda kujisifu na kusifiwa hata kwa upuuzi. Hivi hapa kuna kuibuka kidedea eti wamemaliza mbio? Mtoa hoja angeachana na ugonjwa huu wa kujifisia hata upuuzi. Hizo sifa zinawafaa wanasiasa na wasanii wetu lakini si watanzania wote. Kesho utasikia wakijisifu kuwa maskini wa Tanzania ni wapole au hawalalamiki kama wa nchi nyingine na upuuzi mwingine.
 
Stephen Kiprotich clinched the gold medal in the men's marathon at the 2012 London Olympics-winning in a time of 2:08.01. The Ugandan athlete won ahead of Kenyan runners Abel Kirui and Wilson Kiprotich-winning by almost 200-meters after blowing the competition away in the final ten kilometers of the race. The 23-year-old won his first Olympic title with the victory in the event, having sat behind the Kenyan pace before pulling away to victory. The competition had no answer to the Ugandan's kick and, at such a young age, no doubt has a bright future ahead of him in the sport.

And by the time he neared the finish line, Stephen Kiprotich had such a commanding lead that he grabbed a flag from the stands and wore it on his way to gold. After finishing, he dropped to his knees, bowed and then raised his hands high over his head. A moment to cherish because these haven't happened all that often for Uganda. This was the country's seventh Olympic medal in any sport and second gold. John Akii-Bua, a 400-meter hurdler, won the other gold 40 years ago in Munich. "I made history with my people," Kiprotich said. "They didn't expect me to win. I was keeping behind them, keeping the fire burning. When they go, they thought they'd left me, but I was there. "I kept in touch. Later, I said, 'I believe in myself.' Then, I made my move."

Source: Men's Olympic Marathon 2012: Result, Stephen Kiprotich Wins Men's Marathon | Bleacher Report

Source: Uganda's Kiprotich wins men's Olympic marathon - Connecticut Post
 
Hatimaye hayawi hayawi YAMEKUWA baada ya Watanzania wawili kufanikiwa kumaliza mbio za Marathon katika siku ya mwisho ya michezo ya Olimpiki, London 2012.

Hiyo ni baada ya mkimbiaji wetu mahiri Mussa Faustine kushika nafasi ya 33, huku mwenzake Ramadhan Samson akifanikiwa kushika nafasi ya 66 kati ya wakimbiaji 85 waliomaliza mbio hizo.

Kama kawaida yetu, sote tujumuike pamoja kuwapongeza vijana wetu kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kufanikiwa kumaliza mbio hizo za Km 42 (yaani zaidi ya tripu 10 za Ubungo-Mwenge kwa kupitia Sam Nujoma).
Wahenga walisema KUMALIZA NI JUHUDI, KUSHINDA MIPANGO YA MUNGU. (ingawa kwa mtaji huo basi Mungu atakuwa na upendeleo kwa wenzetu).

kwa matokeo kamili bofya hapa: http://www.london2012.com/athletics/event/men-marathon/index.html?v=20120812-214304762

Jamani huu ni zaidi ya ujinga kusheherekea kushindwa, Tanzania tumechemsha kola Olimpiki kwa kuambulia kapa kasoro ile ya Moscow (1980 ) ambapo Bayi na Nyambui walipotuletea medali 2.
Kama mnawapongeza hawa walioshindwa hakuna haja ya kuendelea kupoteza pesa kutuma watalii.
BTW, inabidi umpongeze yule bondia alietwanga kwenye duru za awali na yule mwogeleaji alieshika namba 57 kati ya 62 akijifurahisha kwenye freestyle duru ya awali, Dah...Nimechoka kwa kweli kwa aibu na ujinga wetu.
 
Hawa jamaa wamejitahidi sana kusema ukweli, namba 33 sio mchezo maana ni dakika 9 tu nyuma ya mshindi katika shindano la zaidi ya masaa mawili ni margin ndogo sana, at least wameonyesha kuwa wamo maana wale wa kuogelea walikuwa sio professionals kabisa walienda kujifurahisha zaidi.
 
Wakirudi, tuwaulize kisayansi kabisa hawa watu wa Olympics Taifa, "kwanini mnatuletea aibu? Siku hatuutaki huu ujinga". Serious kabisa tuwaulize hivyo waelewe tumechoshwa!
 
Hakuna kitu, they have to work hard!! Ni kosa kubwa kuwaambia wamejitahidi wakati wana-east africa wamekula medali. Let them work hard siyo kulala hadi saa mbili ndo wanaanza mazoezi, hakuna kitu kirahisi kihivyo.
 
Wakirudi, tuwaulize kisayansi kabisa hawa watu wa Olympics Taifa, "kwanini mnatuletea aibu? Siku hatuutaki huu ujinga". Serious kabisa tuwaulize hivyo waelewe tumechoshwa!
Watakuambia serikali haiwapi fedha, ndiyo mwisho wao wa kufikiri. Hawawezi kubuni mbinu nyingine ya kupata fedha. In short, they are tired, no more thinking zaidi ya kuvizia bajeti kutoka serikali. Ndiyo maana mi nasema kila siku tusipobadilika mentality ya kuendelea kujaza wazee hata bila kuchanganya vijana aka damu changa tena iliyo-smart, tutaendelea kupiga kelele kwenye keyboard.
 
Mkuu,
Wakijibu hivyo tuwaambie kabisa hatujaridhishwa na majibu kabisa na wala hatuziamini kazi za mikono yenu, watoke au siku wasipeleke wanamichezo kama hakuna maandalizi, kama maandalizi ya medali yanaanza leo hapo sawa!
 
Hakuwezi kupatikana ushindi bila ya juhudi za lazima za serikali na washiriki

Serikali inatakiwa kulea vipaji vya watoto ndio waweze kufanikiwa wakiwa wakubwa.
 
Hakuwezi kupatikana ushindi bila ya juhudi za lazima za serikali na washiriki

Serikali inatakiwa kulea vipaji vya watoto ndio waweze kufanikiwa wakiwa wakubwa.
Bado hizi kauli zinatuchelewesha kufanya vitu vya maana, kila kitu serikali serikali ifanye hiki na kile, jua linachomoza jua linazama. Ni lini tutaanza kusema mmoja mmoja nahitaji kujitoa kwa ajili ya michezo ijayo ya olympic 2016 nchini brazil ili nirudi na medali ya dhahabu? Ni lini tutaanza kujiwekea malengo ya kutaka kuitangaza nchi yetu kupitia michezo na mambo mengine yanayojumuisha nchi nyingi? Ni lini basi, ni lini, ni lini ......? Kama watu wanajua umuhimu wa kujituma katika kazi zao na kujinyakulia zawadi kemu kemu kwa faida yao na familia zao basi taratibu hii mentality ya watu (pamoja na viongozi wetu) kudharau fani za michezo (siyo michezo tu) itakuwa ndo mwanzo wa watu wengi kukaa na kubweteka wakisubiri serikali iwafanyie kitu. Lets wake up and use any chances!! Watu wakianzia ndani kuvunja record za kitaifa, africa then tutakuwa tumepiga hatua kubwa.
 
Kwani walikwenda kumaliza kukimbia au kushinda? Hili ndilo tatizo kubwa tulilo nalo watanzania. Tunapenda kujisifu na kusifiwa hata kwa upuuzi. Hivi hapa kuna kuibuka kidedea eti wamemaliza mbio? Mtoa hoja angeachana na ugonjwa huu wa kujifisia hata upuuzi. Hizo sifa zinawafaa wanasiasa na wasanii wetu lakini si watanzania wote. Kesho utasikia wakijisifu kuwa maskini wa Tanzania ni wapole au hawalalamiki kama wa nchi nyingine na upuuzi mwingine.

The guy is being sarcastic, hakuna pongezi alioitoa hapa zaidi ya kejeli.
 
Hatimaye hayawi hayawi YAMEKUWA baada ya Watanzania wawili kufanikiwa kumaliza mbio za Marathon katika siku ya mwisho ya michezo ya Olimpiki, London 2012.

Hiyo ni baada ya mkimbiaji wetu mahiri Mussa Faustine kushika nafasi ya 33, huku mwenzake Ramadhan Samson akifanikiwa kushika nafasi ya 66 kati ya wakimbiaji 85 waliomaliza mbio hizo.

Kama kawaida yetu, sote tujumuike pamoja kuwapongeza vijana wetu kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kufanikiwa kumaliza mbio hizo za Km 42 (yaani zaidi ya tripu 10 za Ubungo-Mwenge kwa kupitia Sam Nujoma).
Wahenga walisema KUMALIZA NI JUHUDI, KUSHINDA MIPANGO YA MUNGU. (ingawa kwa mtaji huo basi Mungu atakuwa na upendeleo kwa wenzetu).

kwa matokeo kamili bofya hapa: http://www.london2012.com/athletics/event/men-marathon/index.html?v=20120812-214304762

Mkuu, wachache watakuelewa katika hili. Umeona mbali sana. Mwanzilishi wa michezo ya olympics alisema 'The aim of the olympics games is not to WIN but to take PART'. Hongera vijana wetu
 
Nasikia kamati ya Olympic ilitoa milioni 294 Bayi na wenzake wakalamba zote na kupeleka kambi shuleni kwake Kibaha ahahahahahaaaaa hii nchi ni zaidi ya uijuavyo!!!!!
 
Wakenya wanajua riadha ni njia mojawapo ya kuushinda umasikini. Sisi wengi bado hatujastukia hilo bado. Ukiangalia wale Wakenya wanaoshinda Marathons maarufu hapa duniani kama vile Chicago marathon, London marathon, New York marathon wanapata hela nzuri sana. Mbio ndefu zinalipa vizuri kwa hiyo wengine ambao wana vipaji vya riadha huwa wanajituma sana. Mfano mzuri ni yule Samuel Kamau (R.I.P)

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom