Watanzania waelezwa kuwa mbumbumbu wa A. Mashariki

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Watanzania waelezwa kuwa mbumbumbu wa A. Mashariki Basil Msongo, Dodoma
Daily News; Saturday,July 05, 2008 @00:03





Wanachi wengi hawafahamu shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bunge lilielezwa jana. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala aliwaeleza wabunge mjini Dodoma kuwa, hali hiyo ilibainika wakati wa mchakato wa kutafuta maoni ya wananchi kuhusu kuharakisha Shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Dk. Kamala, serikali imeanza kuzifanyia kazi hoja za wananchi na kwamba ushauri wa wadau utazingatiwa na pia maslahi ya taifa
yatalindwa.

“Uchambuzi wa hoja za wananchi utatuwezesha kubaini uwezo na udhaifu wetu katika ushirikiano wa kikanda na jinsi ya kujipanga kukabiliana na changamoto zilizopo na zitakazojitokeza siku za usoni,” alisema Dk. Kamala wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2008/2009.

Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye nchi tano zikiwamo za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Dk. Kamala alisema tangu Umoja wa Forodha ulipoanzishwa, mauzo ya Tanzania katika Jumuiya yameongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 95.4 mwaka 2004 hadi dola milioni 173.1 mwaka 2007.

Kwa mujibu wa Dk. Kamala, katika kipindi hicho hicho, kiasi cha bidhaa alizonunua Tanzania kwa nchi nyingine wanachama kimepungua kutoka dola milioni 137.7 za Marekani mwaka 2004 hadi Dola milioni 106.6 za Marekani mwaka 2007.

Alisema hakuna ushuru wa forodha katika biashara kati ya Uganda na Tanzania, lakini baadhi ya bidhaa za Kenya zinatozwa ushuru kwa kuwa endapo isingekuwa hivyo zingeathiri uchumi wetu. Bunge lilielezwa kuwa viwango vya ushuru kwa bidhaa hizo vimekuwa vikipungua kila mwaka tangu mwaka 2005 na ikifika mwaka 2010 hazitatozwa kabisa.

“Bidhaa zitokazo Kenya hazitozwi ushuru ziingiapo Rwanda na Burundi na vivyo hivyo ushuru kwa bidhaa za Uganda umepunguzwa kwa asilimia 80 chini ya utaratibu wa COMESA,” alisema Dk. Kamala. Alisema ifikapo mwaka 2010 ushindani katika soko la Afrika Mashariki utaongezeka hivyo wafanyabiashara wajizatiti ili kushindana na bidhaa za Kenya na dunia nzima.

Wakati akichangia bajeti hiyo, Mbunge wa Kuteuliwa, Thomas Mwang’onda alisema Wizara hiyo inapaswa kuhakikisha kuwa faida za Jumuiya hiyo zinagusa maslahi ya watu wa kawaida. Aliuliza kama Watanzania wanaifahamu Wizara ya Afrika Mashariki na kazi zake ama ni Wizara ya urembo tu kwa madai kuwa, inaonekana ni ya wasomi tu.

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF) alisema, Tanzania inapaswa kuchukua tahadhari kwa kuwa endapo wageni watakuja kuchukua rasilimali za Watanzania, ikiwamo ardhi yatatokea matatizo makubwa.

Alisema wageni wakitaka kutumia rasilimali nchini, lazima waingie ubia na Watanzania na akadai kuwa Watanzania ni wazito kufanya maamuzi ndiyo maana wamekuwa wakilalamikia Wakenya na Waganda.

Mbunge wa Pangani, Mohamed Rished Abdallah (CCM) alisema kama Tanzania isipokuwa makini, miradi ya Afrika Mashariki itainufaisha zaidi Kenya na kuna umuhimu wa kuiimarisha bandari ya Tanga ili ishindane na ya Mombasa na Wizara hiyo ina jukumu la kusaidia hilo.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto alisema, Wizara inapaswa kufanya tathmini ili kufahamu ni maeneo gani yameongeza faida baada ya kuanza kutumika kwa makubaliano ya ushuru wa forodha ili yaimarishwe.

Alisema Wizara pia inapaswa kuandaa ajenda ya Tanzania itakayotekelezwa wakati Tanzania itakapokuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kuanzia Juni 2010 na pia akashauri Rwanda na Burundi waingie mapema katika itifaki ya ushuru wa forodha ili Tanzania inufaike kwa kuwa kuna soko kubwa kwa wananchi milioni 7.8 wa Rwanda , na Rwanda yenye watu milioni 10.

http://habarileo.co.tz/kitaifa/?id=10249
 
Back
Top Bottom