Watanzania Waasia kwenye vyombo vya Usalama

Mimi nafikiri kunahitajika mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Nipo katika jitihada za kumtafuta "inspirational leader".

Yes, we can get one!
 
Nitashangaa sana kama tunaiga wanayosema waingereza kuhusu institutional racism huko Uingereza baada ya ushindi wa Obama na kuyalinganisha na hapa Tanzania. Hawa watanzania wenzetu wenye asili ya asia ni watanzania wazalendo lakini uzalendo wao utaia shaka kiasi cha kujiuliza kwanini waaminiwe hata madaraka ya nchi. Kuna mifano lukuki ya kuwatilia shaka. Hebu angalia kwenye field ya biashara walivyoingia na kufanya rushwa na milungula iwe kitu cha ajabu. Kama wameingiza rushwa kwenye biashara unategemea nini wakiingia kwenye siasa au uongozi wa taifa? Angalia kila ikifika wakati wa uchaguzi huku bara wote wanakimbilia UK, Canada au India, uchaguzi ukiisha ndio wanarudi, what kind of uzalendo is this? Kuna mifano mingine midogo, angalia Rostam mfanya biashara mwenye asili ya Asia alivyoifanya CCM, jamaa amekuwa rais by proxy kwa muda, angalia alivyoichezea nchi. Angalia Vithlani na aliyofanya, hayuko wazi kwenye siasa na uongozi. Do you want more of them?
Au niambie wahindi wangapi wameenda National service, JKT, kama wapo basi ujue hao ndio wazalendo kweli au kama sio wazalendo basi walikuwa na ajenda nyingine.
Kwa upande wa Zanzibar siwezi kulinganisha sana na sisi huku bara, watanzania wenye asili ya Asia kule visiwani wanajiona watanzania/wazanzibar na wako proud. Lakini walioko huku bara, wanaona nchi yetu ni shambani wanachuma tu, wanaenda zao kivulini ni kama mamluki.
Hapa Mwanakijiji naomba kupingana na wewe, sio kwa msingi wa ubaguzi wa rangi wala ukaburu, ni kutokana na tabia zao. niksema zao naomba ieleweke kuwa sio wote. Wapo wachache ambao (alnoor Kassam, shivji likes) ni wa maana sana, alkini wengi michosho. Let us be frank.
 
Mimi nadhani kuna vitu ambavyo wao wenyewe wanastahili kuanza kuvifanya kama haki yao ya kiraia. Wakati umefika kuwaona Wahindi na Waararbu kama mojawapo ya makabila ya Tanzania. Na wao wahindi waanza kujitambua hivyo kuwa na wao ni raia wa Tanzania wenye haki sawa siyo tu ya kuchuma na kunufaika kiuchumi bali pia kuhakikisha kuwa kile wanachokichuma wanakilinda pia.

Naamini ndugu zetu hawa wakianza kuingia katika taasisi za usalama tutakuwa tunaelekea kwenye level mpya ya kupiga vita ufisadi na rushwa hasa kubwa kubwa. Lakini hili haliwezekani hadi kizazi cha vijana wao kitakaposema kuwa "tanzania ni yetu pia" na siku moja wahindi kumi au ishirini wakaamua kujitokeza kujiunga na mafunzo ya Polisi au ukadeti pale Monduli. Hili linawezekana.
 
kwenye hii vita ya ufisadi, nimesikia watanzania wachache wenye asili ya Asia wanaoishi Canada, walau walijitokeza kulaani ufisadi na wizi uliofanya na wenzao wenye asili ya Asia. Kama wengi wangekuwa hivyo nadhani mambo yasingekuwa kama yalivyo sasa.
 
Nitashangaa sana kama tunaiga wanayosema waingereza kuhusu institutional racism huko Uingereza baada ya ushindi wa Obama na kuyalinganisha na hapa Tanzania. Hawa watanzania wenzetu wenye asili ya asia ni watanzania wazalendo lakini uzalendo wao utaia shaka kiasi cha kujiuliza kwanini waaminiwe hata madaraka ya nchi. Kuna mifano lukuki ya kuwatilia shaka. Hebu angalia kwenye field ya biashara walivyoingia na kufanya rushwa na milungula iwe kitu cha ajabu. Kama wameingiza rushwa kwenye biashara unategemea nini wakiingia kwenye siasa au uongozi wa taifa?

Ni kutokuwa mkweli kufikiria kuwa rushwa ni suala la asili ya mtu. HIvi unataka watu waamini kuwa Watanzania wenye asili ya Afrika (weusi) hawatoi au kupokea rushwa kwenye biashara? Ukifiria sana utaona kuwa yawezekana sisi weusi ndiyo vinara wa rushwa kwa sababu hili kundi la watu wachache linaonekana zaidi kuliko kundi la wengi. Kama kuna tatizo la rushwa katika biashara kuwalaumu wahindi na waarabu ni kujaribu kuficha vichwa vyetu mchangani kama mbuni. Rushwa ni tatizo letu kama vile lilivyo lao.

Angalia kila ikifika wakati wa uchaguzi huku bara wote wanakimbilia UK, Canada au India, uchaguzi ukiisha ndio wanarudi, what kind of uzalendo is this?

Ndio sababu kubwa ya kuanza kuwarecruit waweze kuingia kwenye vyombo vyetu vya usalama.

Kuna mifano mingine midogo, angalia Rostam mfanya biashara mwenye asili ya Asia alivyoifanya CCM, jamaa amekuwa rais by proxy kwa muda, angalia alivyoichezea nchi. Angalia Vithlani na aliyofanya, hayuko wazi kwenye siasa na uongozi. Do you want more of them?

Hebu toa mifano ya wafanyabiashara weusi ambao na wenyewe hawana influence ya namna hiyo katika serikali yetu. Utaona ni wengi tu!

Au niambie wahindi wangapi wameenda National service, JKT, kama wapo basi ujue hao ndio wazalendo kweli au kama sio wazalendo basi walikuwa na ajenda nyingine.

Wapo wengi tu walioenda JKT hasa miaka yetu sisi ile ya 70 na hata early 80s.

Kwa upande wa Zanzibar siwezi kulinganisha sana na sisi huku bara, watanzania wenye asili ya Asia kule visiwani wanajiona watanzania/wazanzibar na wako proud. Lakini walioko huku bara, wanaona nchi yetu ni shambani wanachuma tu, wanaenda zao kivulini ni kama mamluki.

Siyo wote wako hivyo, kama vile kuna watu ambao wanajiona wao si Watanzania hasa wanapokuwa ughaibuni na hao jamaa ni weusi tii tii. Nimeshakutana na wabongo hapa ambao ukitaja Tanzania wanakushangaa.

Hapa Mwanakijiji naomba kupingana na wewe, sio kwa msingi wa ubaguzi wa rangi wala ukaburu, ni kutokana na tabia zao. niksema zao naomba ieleweke kuwa sio wote. Wapo wachache ambao (alnoor Kassam, shivji likes) ni wa maana sana, alkini wengi michosho. Let us be frank.

Sawa lakini tunafanya nini kuhakikisha wanakuwa accommodated kwenye nchi yao pia. Ni kwa jinsi gani hatuwatendei kibaguzi. Afrika ya Kusini leo hii wanaweza kutumikia nchi yao kwa pamoja. The same thing in Botswana na Namibia.

Sisi ni kitu gani kinatushinda?
 
Mwanakijiji unachosema ni kweli. Asili ya mtu sio ishara ya tabia yake. Hata sisi wenyewe ni wezi wakubwa umeona kaka yako alivyo mwizi, baba yangu alivyofisadi, mjomba wako alivyotufilisi. Ninachosema ni kuwa hawa jamaa si rahisi kuwaamini kutokana na matendo yao, ni wachache sana lakini impact yao ni kubwa kupita kiasi. \ni vema tukiwaangalia kwa jicho la makini kabla ya kuwapa uongozi wa vyombo vyetu vya usalama.
 
Bongolander, miye sijazungumzia kuwapa uongozi wa vyombo vyetu vya usalama. Nimezungumzia wao kutumikia na kuanza kama wengine tu kama ni Ukuruta basi waende kuwa makuruta kama ni street cops wawe street cops. Kama ni maafisa tu wa vyeo vya chini jeshini n.k iwe hivyo na kama katika utumishi waoo wakapata kupanda ngazi basi wapande kwa haki kama wengine tu.
 
simple: Institutional racism.. (circumstancial rather than deliberate)
Waarabu in most cases wako business oriented as well as wahindi. Family business in most cases, maduka etc. they hail from a class of traders and merchants rather than farmers.

They, in all likelihood fail to see any merits of joining such forces because all they want is wealth and prosperity. I cant imagine that they are interested in honour, sijui defending their country etc.
Its much easier to bribe the police when necessary, get rich and then become an MP by buying the votes... All the while, the paramount objective being to further their economic interests... very simple logic... but it works so i cant blame them.

kinyambiss,

This is deeply entrenched in the Hindu caste system, the issue assumes a religion dimension.

Wahindi wengi wanaokuja Tanzania wako katika caste ya wafanyabiashara, wahindi walio katika caste ya kufanya kazi kama za usalama, kwa sababu ya obligations zao kwa nchi wanakuwa wengi wanabaki India.Ni vigumu kumkuta muhindi hata US Army, labda awe Engineer Kalasinga wa ngama (ambao wanajulikana kwa uinjinia)

Matatizo mengi tunayoyaona kwa wengi wa wahindi (kutooana na wengine, kutojichanganya etc) yana mizizi katika Hinduism na caste system yake.
 
Last edited:
Hakuna kitu kinachoonesha utii wa mtu kwa nchi yake kama utayari wake kufa kwa ajili ya nchi hiyo. Ni kipimo cha juu kabisa cha mapenzi ya mtu kwa nchi yake. Lakini pia kuitumikia nchi katika nafasi mbalimbali kunaonesha jinsi gani mtu anavyolipenda Taifa lake.

a. Kwanini Watanzania wenye asili ya Uhindi au Uarabuni hawaingii kwenye vikosi vya usalama?

Wewe mwenye asili ya Tanzania umeingia kwenye vikosi vya ulinzi na usalama, magereza na polisi ?

Au unataka mwenye asili ya Kihindi ndio aonyeshe "kipimo cha juu kabisa cha mapenzi ya mtu kwa nchi" kwa kwenda kukufia wewe kwa ajili ya nchi yako ya asili?
 
Manake sio hao wa kiasia tu! utaratibu wa kujiunga na majeshi yenyewe ni mizengwe ya kufa mtu hata wabantu wapo wengi tu ambao wanauwezo wakulitumikia taifa kupitia majeshi lakini kikwazo kikubwa ni utaratibu mzima wa kujiunga na vyombo hivyo.

Utaratibu hauko wazi na hautoi fursa sawa kwa watu kujiunga. Kama hatuta badilisha mfumo na uendeshaji wa vyombo hivyo usitegemee waasia tu bali hata watu wenye sifa na uwezo hawatajiunga na taasisi hizo.
 
Wewe mwenye asili ya Tanzania umeingia kwenye vikosi vya ulinzi na usalama, magereza na polisi ?

NDIYO! have you?

Au unataka mwenye asili ya Kihindi ndio aonyeshe "kipimo cha juu kabisa cha mapenzi ya mtu kwa nchi" kwa kwenda kukufia wewe kwa ajili ya nchi yako ya asili?

Wala sihitaji hiyo, lakini nchi yangu wakati wowote ikiniita kuitumikia na kuilinda niko tayari "saa yoyote, wakati wowote, na mahali popote nitakapoamriwa"!
 
Kwanini wakurya wanaingia kwa wingi kwenye majeshi yetu?wangekwa wengi mngeanza kupiga filimbi ooh mbona IGP muhindi?!....... "mbona bosi wa usalama wa taifa muarabu tena muislamu?......!!!

Hehehe mkuu YOYO hii imeniacha hoiii, mkianza hivyo mtasema kwa nini wakurya wanakuwa sana maraisi wa chuo kikuu cha dar es salaam?
 
Lakini huko India, Pakistani, Indonesia n.k wahindi wanafanya kazi za usalama pia. Na wako tayari kufia nchi zao na kujitoa mhanga kulinda taifa lao. Yawezekana kuwa ni kweli bado hawajakubali kuwa wao ni Watanzania hasa au ni watanzania as long as things are going good for them?

Je yawezekana ni kwa sababu hawaoni sababu ya kushiriki katika usalama wa Taifa namna hii maana naamini tunaweza kuwa na maagenti wazuri tu katika TISS, wapelelezi n.k na tukaweza kufanikiwa katika mapambano ya vita vya ufisadi?

Mkuu, mafisadi ndio haohao wahindi sasa itakuwa vipi waingie tena usalama?
 
Hakuna kitu kinachoonesha utii wa mtu kwa nchi yake kama utayari wake kufa kwa ajili ya nchi hiyo. Ni kipimo cha juu kabisa cha mapenzi ya mtu kwa nchi yake. Lakini pia kuitumikia nchi katika nafasi mbalimbali kunaonesha jinsi gani mtu anavyolipenda Taifa lake.

Mojawapo ya vitu ambavyo havionekani sana katika Taifa letu ni Watanzania wenzetu wenye asili ya Asia (wahindi, Waarabu, n.k) kujiunga na vyombo vyetu vya usalama hasa majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama.

Nikikumbuka vizuri baada ya uasi mwaka 1964 ni maafisa wachache wa kizungu ambao waliendelea na jeshi na ni mmoja ambaye aliendelea kuitumikia kwa muda mrefu tu. Sifahamu sasa hivi kama kuna maafisa wowote wa JWTZ ambao aidha wana asili ya Uhindi au Uarabuni.

Kwa upande wa Polisi kumekuwepo na maafisa kadhaa wa Kihindi na wenye asili ya Uarabuni lakini nadhani sasa hivi wengi watakuwa wameshastaafu. Nafahamu wapo vijana wachache ambao waliingia huko (namkumbuka Bi. Khadija K. binti wa kiarabu aliyejiunga toka Tanga) na pia Insp. Khan ambao at the time nilikuwa nashangaa kweli kuwaona kwenye jeshi letu.

Hata kwenye taasisi nyingine (ukiondoa za Kitaaluma) bado jamii hii ya Watanzania inakosekana sana. Sijui idadi yao kwenye TRA, Public service n.k

Kwa upande wa Magereza ndiyo sijui kabisa kama kuna watanzania wenye asili ya nje ya bara letu ambao wanaitumikia nchi yao hivyo. Wakati ambao nakumbuka tuliweza kuwaona Wahindi na Waarabu wengi ni wakati wa JKT ule. Sijui katika JKT hiii ya kujitolea inakuwaje.

BIla ya shaka unajiuliza "what is the point". Point yangu ni kuwa inaonekana aidha kwa makusudi au by default mchango wa Watanzania hawa unataka kuishia kwenye siasa na biashara au sekta binafsi na siyo kwenye utumishi wa umma.

Nakabiliwa na maswali machache:

a. Kwanini Watanzania wenye asili ya Uhindi au Uarabuni hawaingii kwenye vikosi vya usalama? Zamani nakumbuka tulikuwa tunawatania kuwa wao ni "watoto mayai" hawawezi kazi za shurba lakini nikagundua kuwa hata kule Uhindi na Uarabuni kuna majeshi na POlisi na wao wanapewa mafunzo ya kijeshi na kuhenyeka kama sisi. Hivyo suala la "umayai" halipo.

b. Ni juhudi gani zinafanyika kurecruit Watanzania hawa hasa kutokana na ujuzi wao wa mambo ya biashara, utaalamu wa IT, n.k n.k na hivyo kuleta vipaji ambavyo vinahitajika sana kwenye vyombo vyetu hivi?

c. NI kwa kiasi gani familia za ndugu zetu hawa zinawa encourage watoto wao kuitumikia nchi yao kwa zaidi ya siasa na biashara na kuingia kwenye utumishi wa umma. Watakuwa wanaendelea kutoa misaada tu mpaka lini.

Mwanakijiji;
Thanks for usefull comments. nimeona hata kubofya THANKS hakutoshi. asante sana. Sasa rudi nyumbani....

Please your mobile on my PM is highly needed
 
NDIYO! have you?

Wala sihitaji hiyo, lakini nchi yangu wakati wowote ikiniita kuitumikia na kuilinda niko tayari "saa yoyote, wakati wowote, na mahali popote nitakapoamriwa"!

Mbona unaji contradict mwenyewe? Kama una serve kwa nini uko "tayari" kufanya ulichosema utafanya?
 
NDIYO! have you?

Hapana. Ndio maana sijanyooshea Mhindi kidole kwa kutoingia jeshini, polisi, usalama, magereza.

...lakini nchi yangu wakati wowote ikiniita kuitumikia na kuilinda niko tayari "saa yoyote, wakati wowote, na mahali popote nitakapoamriwa"!

Wakikuita mara ngapi, lini, kukiwa na vita ? Na wahindi wanaweza kusema wanasubiri kuitwa. Na hakuna ataenikatalia kwamba ikipita mbiu ya mgambo saa hivi kukusanya watu kwenda kufa kwa ajili ya nchi yao itakuwa rahisi kumpata Mhindi wa mtaa wa Mindu kuliko Mwanakijiji wa Mtaa wa Maili Nane, Mji wa Magari, anaesubiri "kuamriwa" kutumikia!

Sasa ili kuhimiza umuhimu wa wazo lako, ili baadhi yetu tujue unaongea kwa vitendo na sio porojo, hebu tuambie leo hapa, ulitumikia polisi gani, au magereza gani, au jeshi la Wananchi kikosi gani, au Usalama wa Taifa kitengo gani na lini.

Usinambie JKT ya kulazimishwa, wala sungusungu ya Mrema, wala chipukizi wa Sisiemu, wala skauti wa shule ya Uhuru. Maana humo hata Wahindi wamo.

Halafu ndio tutaendelea kuchambua Wahindi.
 
Hapana. Ndio maana sijanyooshea Mhindi kidole kwa kutoingia jeshini, polisi, usalama, magereza.

Wakikuita mara ngapi, lini, kukiwa na vita ? Na wahindi wanaweza kusema wanasubiri kuitwa. Na hakuna ataenikatalia kwamba ikipita mbiu ya mgambo saa hivi kukusanya watu kwenda kufa kwa ajili ya nchi yao itakuwa rahisi kumpata Mhindi wa mtaa wa Mindu kuliko Mwanakijiji wa Mtaa wa Maili Nane, Mji wa Magari, anaesubiri "kuamriwa" kutumikia!

Sasa ili kuhimiza umuhimu wa wazo lako, ili baadhi yetu tujue unaongea kwa vitendo na sio porojo, hebu tuambie leo hapa, ulitumikia polisi gani, au magereza gani, au jeshi la Wananchi kikosi gani, au Usalama wa Taifa kitengo gani na lini.

Usinambie JKT ya kulazimishwa, wala sungusungu ya Mrema, wala chipukizi wa Sisiemu, wala skauti wa shule ya Uhuru. Maana humo hata Wahindi wamo.

Halafu ndio tutaendelea kuchambua Wahindi.

nimeshajibu swali lako moja and that is all you gonna get. Jadili mjadala haya ya kujaribu kujua fulani anayejadili x au y yuko vipi na imekuwaje haina sababu. Angalia mjadala wenyewe ulivyo. Ukitaka kujua nimetumikia wapi call me nitakuambia kwenye simu.
 
Mjadala ni Wahindi hawa bother kuiiingia kwenye vyombo vya Usalama.

Mimi nakwambia huwezi kuanza huo mjadala kabla hujajibu swali hili, "wanaosema wahindi hawamo wao wenyewe wamo ? "

Wewe ulikuwa kwenye chombo cha Usalama lini na kipi, wapi ?

Muhindi hawezi kwenda kukufia wewe mwenye asili kama mwenyewe hujaamua kujifia bwana. I guess uliingia ukatoka, ukatokomea mtaa wa Maili Nane, Mji wa Magari. Mhindi katoka Kashmandur kaenda ishi mtaa wa Mindu.

Who is a truer patriot ? Who loves Tanzania more ?

Mr. Mtanzania wa asili, you have no moral courage to answer that question in a million years.
 
Back
Top Bottom