Magabe Kibiti
JF-Expert Member
- Jan 20, 2008
- 292
- 0
Mods tafadhali naombeni hii ikae hapa angalau weekend hii ingawa haiusiani na siasa moja kwa moja.
Nilikuwa napitia blog ya michuzi na nikaona tangazo la watanzania walioko Dallas ambao wameanzisha restaurant yao na kuiita kijiweni. Tafadhali fuata hii link hapa chini:
MICHUZI
Kwa kweli nimefurahi sana kuona vijana wa kitanzania wakishirikia na kufanya mambo makubwa kama haya ya biashara halali za kuwapatia pesa na nafasi muhimu ya lines of credit toka kwa benki za marekani. Mimi siishi Dallas ila nimefurahishwa sana na hili.
Huu ni mfano wa kuigwa na natumaini watanzania wengi wataendelea na moyo huu wa kufanya mambo makubwa huko kwenye nchi walizoamua kuishi na kutafuta mali. Hii pia itakuwa ni nafasi nzuri ya kutambulisha vyakula vya kitanzania na kiafrika kwa wamarekani ambao hawajawi kufika Afrika.
Hongereni sana kwa kazi nzuri na mfano mzuri mlioonyesha wenzetu wa Dallas