Watanzania tutafakari na kufanya maamzi ya busara kabla ya kugombana.

rugumye

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
561
178
Katika historia ya Tanzania na Africa Mashariki tunakumbuka Ukristo uliingia kabla ya ukoloni enzi za akina Vasco Da Gama mfanya biashara kutoka ureno aliefika Tanganyika na Kenya. Huyu jamaa na wenzake walioingia kwa lengo kama hilo ndipo Ukristo ulipoanza kuingia Zanzibar na baadae ukaja bara. Baada ya mkutano wa Berlin 1884-85 wakoloni walipogawana Afrika ndipo wakaja wafanya biashara, wapelelezi na wahubiri wa Ukristo. Ukristo ulienea bara kwa hali kubwa sana wakati wa ukoloni.

Historia inaonesha Waarabu kutoka Omani walimtimua Vasco da Gama na kuimiliki Z'bar na kingo za bahari kunzia Mombasa, Tanga, Dsm Lindi Mwatara.
Historia imeandika kuwa Uslamu uliingia Zanzibar, Mombasa, Tabora, Kigoma na kwengineko. Warabu hao walioleta dini ya Kiisamu ndiyo hao hao walioleta utumwa.

Natafakari kwa kina leo hii kuna watu (waafrika) tunagombania dini ambazo walizileta ndiyo hao waliwatawala babu zetu na kuwatumikisha katika mashamba yao na kupeleka bidhaa zilizopatikana Ulaya...
Wrngine ndiyo hao waliouza babu zetu na kama bidhaa?

Baadhi ya Wanzibar wametokea Geita, Tabora, Kigoma, Bagamoyo.... Wanataka kujitenga kwa lipi wakati chimbuko lao nu huku bara?
Hao waliotuminisha katika dini zao waliuza babu zetu kama bidhaa, wengine waliwaua, wangine wakatumikisha kujenga reli na majumba yako kama ofisi....

Kwa nini twagombania dini za watu walitunyonya kwa kuchukua rasilimali na wengine kutupiga mnada kama bidhaa??

Lakini haya yote chanzao ni serikali yyetu ya chama twawala CCM. Haya ndiyo matunda ya wagawe uwatawale, mwaka 2005, CCM ilitumia kampeni za udini kwa kuwaahidi waisilam Mahakam ya kadhi, wakati Fulani Rais wetu JK alisimama kwenye vyombo vya habari akijitetea kuwa siyo yeye aliye anzisha swala la Mahakam ya kadhi. Waislamu wamekuwa watulivu siku nyingi lakini kwa sasa wana hasira mioyoni mwao. Hata hili tukio la mbagara ni matokeo ya yale waliyo nayo moyoni. Imekuwa ni kawaida kwa CCM kuvunja Amani ya watanzania na katiba ya nchi bila kuulizwa huku vyombo vya habari vikiwa kimya bila kukosoa jambo hilo. Mfano; Mwaka 2005 CCM iliweka kwenye irani yake ya uchaguzi swala la mahakama ya kadhi ambayo wameshindwa kuitekeleza mpaka sasa huku kikijua ni hatari kwa mshikamano na Amani ya Tanzania. Chama cha mapinduzi kwa kufanya kosa hilo kilipaswa kufutwa kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Ibara ya 20-(2) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake;- a) Kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya;- i. Imani au kundi lolote la dini. ii. Kundi lolote la kikabila pamoja watu watokeapo, rangi au jinsia. iii. n.k
 
Back
Top Bottom