Watanzania tunapoogopa mvua na folen barabaran kuliko ukimwi

Pididy...usilinganishe maembe na nazi. Ugonjwa siyo sawa na mvua au foleni ya magari...na ugonjwa wa UKIMWI ni kitu kingine ambacho hatupaswi kukiwekea mzaha au kunena maneno yanayoonekana kuwadhihaki wenye UKIMWI.

Tuchukue hili la foleni - watu hawaogopi foleni bali wanaichukia foleni kwa sababu ya kupoteza muda doing nothing but wait; wanakuwa wanaharaka kuwahi mambo fulani nk.

Mvua, watu wanachelea kulowa na kuwa chepechepe hasa akina dada si unajua tena wanajikwatua kwa vipodozi na mapambo mbalimbali kuanzia kichwani hivyo kulowa ni mbaya.Kina baba/kaka nao hawataki kulowa kwa sababu zinazofanana na hizo..utalowaje hadi uonekane kama mwendawazimu?

Tuje kwenye UKIMWI - katika magonjwa yaliyowahi kuwatesa wanadamu na kuwapa changamoto,UKIMWI ni kiboko yao. Hii inatokana na hulka ya binadamu alivyoumbwa kama tutaangalia njia moja ya uambukizo ambayo ni kujamiiana.Tangia mwanadamu aumbwe ... tuna mifano mingi sana inayoashiria hulka ya binadamu kwenye kitendo hicho - kuanzia enzi za manabii hadi zama zetu. Sihitaji kunukuu mifano hii mizito maana itatushtua zaidi. La msingi ni kwamba, pamoja na makatazo, hatari za wazi zilizopo, binadamu idara hiyo kashindikana.Cha kufanya ni kuendelea kuhubiri usalama wa maisha tu na siyo kulaani na kuhukumu maana unaweza kunyooshea watu vidole, halafu siku ya siku ukajikuta na wewe ni miongoni mwa wagonjwa wa UKIMWI - Swali litakuwa..IMEKUWAJE MWENZETU?
 
Back
Top Bottom