Watanzania tunapenda mepesi mepesi!

Tanzania haina vipaumbele (priorities) tunachukulia mambo kwa pupa tunashindwa kuweka mipango ya muda mrefu tunataka tufanye kitu kionekane leo kisichukue muda mrefu ili watu wapate 10% mapema kabla hawajaacha madaraka

Angalia badala ya kuisaidia TRL isimame tunaanza kufikiria train ya upepo ambayo gharama yake ni kubwa mara mia hiyo ni akili au matope, si kwamba hao wanaopanga hivyo hawajui kuwa kwa uchumi wetu huu itatuchukua muda mrefu ila wanataka 10% yao wachukue then they dont care kama mpango huo utaendea au utakufa

Wamiliki wa vyombo mbalimbali vya habari na waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika kuipigia kelele serikali lakini waandishi wengi wa Tanzania wamewekwa mifukoni kazi yao ni kupamba hata pasipopambika hawajui kwamba kwa kufanya hivyo wanaangamiza si kizazi hiki tu bali na vizazi vifuatavyo

Viongozi wengi wa vyama vya siasa angalia wabunge wetu hawa ndio wanaotegemewa kuongoza kelele dhidi ya serikali na si kwamba hawajui wajibu wao bali hufanya hivyo kwa maslahi yao kwanza ndiyo taifa baadae

Kada nyingine inayotakiwa isaidie kuikumbusha serikali kutekeleza wajibu wake ni wasomi wetu inakatisha tamaa kuona msomi anasahau taaluma yake na kuanza kuipamba serikali hata kama utekelezaji wake hauridhishi mfano REDET
 
Tumetayarishwa kwa hayo. Mtoto angali mdogo anakunywa maziwa na uji akiisha komaa anakula ugali na makukuru. Bado kitambo kidogo Bongo itakuwa si ile tuliyoizea, si ile polisi wanaweza wakaambiwa kamata yule bambikizia kesi weka ndani hakuna mdhamana, si ile ambayo wala rushwa na wategaji kazini wanatukuzwa wana akili, si ile ambayo mfugaji anafukuzwa katika ardhi yake, kisha ni ya mwarabu (nani alikuwepo kabla ya mwingine?), si ile ambayo mfanyakazi analipa kodi mpaka haelewi nini cha kufanya (PAYE=30%, NSSF=10%, VAT=18%, (Maji 1%-EWURA, Umeme-1% EWURA, Umeme 3%-REA, bado kuna excise duty au kod zingine amounting 20-25%, etc) haya yote analipa mfanyakazi (almost more than 80% of your salary goes into taxes), na hii ndiyo wanayotumia wahindi kuiba kwani ukilipa kihalali mfanyakazi hataweze kumudu maisha na ndiyo maana wana payment za uani ili kuweza kusave 40% (NSSF ni kama kodi tu maana inachukuliwa na ukiangalia sheria iliyopo inamkandamiza sana mfanyakazi). haya yote yana mwisho. Chama kinachotaka kishinde kije na sera ya kuboresha mafao ya wafanya kazi na kuwapunguzia mzigo. wapige kampeni mpaka kijijini ili kijijini nao waweze kuelewa. Nadhani kama mimi nilivyokaribia kuchoka na utaratibu wa nchi hii nadhani kuna wengi nyuma yangu na itafikia wakati watasema sasa hii mwisho hapa na hapo ndipo watakapojua kuwa wa Tanzania kumbe hatuko hivyo!!!!!!
 
Yes anayewaza kinyume na mimi ni adui! ili kuzuia ubishi na kuonekana adui unakubaliana na mbishani hata kama huko sahihi!
 
Watu wanakuja JF na kukandya kwamba JF imepoteza muelekeo, lakini hawafanyi lolote katika kuchangia positively (wanapenda vizuri vilivyoundwa, kuviunda hawataki.)

Ukiuliza maswali magumu lakini yaliyo relevant kuhusu kuwako kwa mungu anayeruhusu maovu duniani unaonekana mtu wa ajabu. By the way unaweza kuona kama nachomekea issue isiyo relevant, lakini matatizo yetu 99% unaweza kuya trace back kwenye hili, the 1% is just for the sake of uncertainty principle and the second law of thermodynamics, nothing is 100%, even nothing is not 100% nothing.

Kila mtu analalamikia serikali wakati book definition ya serikali ni watu wenyewe. Siku ya kupiga kura ikifika less than 50% of eligible voters wana vote.

Kila mtu mtaalam, wanaojua wachache.

Watu wanaongea sana bila kufikiri, wanaoweza kufikiri hawaongei.
 
ujasiri mtu hazaliwi nao bali hujengwa,
Kwa Tanzania mjadala mkuu ulipaswa kama nchi tuchague ni aina gani ya siasa inayotupasa kwa sasa, kwa maana hatueleweki.
pili aina ya elimu tuliyonayo na tunayoendelea nayo je inatufaa au? maana kuna watu na heshima zao na elimu zao lakini decision na behavior zao ni za watu wasioelimika kabisa,
unajua ni aibu kwa mtu mwenye elimu ya maana kukwambia mabilioni ya fedha ni vijisenti tu na waTAnzania wote tunamfuraia kwa kutupa msamiati mpya, na hakuna action yoyote inayochukuliwa
 
ujasiri mtu hazaliwi nao bali hujengwa,
Kwa Tanzania mjadala mkuu ulipaswa kama nchi tuchague ni aina gani ya siasa inayotupasa kwa sasa, kwa maana hatueleweki.
pili aina ya elimu tuliyonayo na tunayoendelea nayo je inatufaa au? maana kuna watu na heshima zao na elimu zao lakini decision na behavior zao ni za watu wasioelimika kabisa,
unajua ni aibu kwa mtu mwenye elimu ya maana kukwambia mabilioni ya fedha ni vijisenti tu na waTAnzania wote tunamfuraia kwa kutupa msamiati mpya, na hakuna action yoyote inayochukuliwa

Hakuna elimu itakayofundishwa darasani na kukosa kutiliwa mkazo katika jamii itakayoweza kubadilisha mambo.

Huyo Chenge aliyesema "vijisenti" wala huwezi kusema utalaumu elimu yetu, Chenge kasoma mpaka Harvard, kama swala ni elimu - I intend classroom/ western education- Chenge anayo, ya kimataifa. That goes not only for our current leaders, lakini hata ukirudi katika awamu ya Mwalimu, utakuta tulikuwa na ma Ivy Leaguers kibao, Princeton,Yale, Harvard the works ! Mpaka across the pond, Edinburgh, LSE, Oxbridgbe I won't be surprised kama tuna watu wa Eton na Sandhurst :) .

Swala ni, je jamii yetu ina standards gani in general? Tuna level gani ya accountability? Kauli ya mtu inapewa uzito gani?

Ukisikiliza ile press conference ya Malecela, ukamsikiliza Kova, ukamsikiliza Muro, utaona hakuna accountability, hakuna preciseness. Watanzania tuna style ya kuongea iliyo shaghalabaghala, kuanzia Nyerere Malecela na the learned gentry wa nchi, watu wa kati kina Kova, vijana watanashati wa leo kina Muro, mpaka watoto wa uswazi wasiojua hata Kiswahili. Hakuna clarity ya kujieleza, which is a symptom of lack of clarity in thinking.

Kuna swali moja lilitakiwa kuulizwa kutokana na maelezo ya Jerry Muro lakini sijalisikia mpaka sasa kuulizwa.

Kuna wakati Jerry katika kubwabwaja kwake, labda katika kujionyesha kwamba yeye ni matawi ya juu na hawezi kuchukua rushwa ya milioni kumi - by the way figure ya rushwa ilikuwa inapanda na kushuka baina ya milioni kumi na milioni arobaini, utasema Dow Jones on a bad week- katika kujionyesha kwamba yeye ni matawi ya juu -mpaka kumsema Kova ni mtu mdogo sana- Jerry akasema amepewa offer ya rushwa kubwa zaidi ya shilingi milioni 150.

Lakini sijasikia mtu yeyote kuuliza hii rushwa amepewa na nani? M,bona hatujaisikia details zake etc etc. Au ni mie tu ambaye siijui hii issue?

Lakini pale Jerry alipokuwa anasema ikaonekana ni kama kigenge cha waandishi wa habari, na waandishi wa habari hawawezi kumuuliza mwenzao maswali probing, maana labda hata na wao wenyewe wana dirty laundry zao.

Tunarudi kule kule alikosema mchangiaji mmoja hapo juu, badala ya kutafuta ukweli, tunatafuta teams, na mtu yeyote anaye maono tofauti ni adui.

Simplistic thinking indeed.
 
Yatosha kuchangia ktk thread hii.Isome,ukiielewa anza kuchukua hatua.
Kama imekugusa ni vizuri kama hujaguswa jiulize kama upo kawaida au la na kama hujaielewa,muulize mwanakijiji.
 
Yatosha kuchangia ktk thread hii.Isome,ukiielewa anza kuchukua hatua.
Kama imekugusa ni vizuri kama hujaguswa jiulize kama upo kawaida au la na kama hujaielewa,muulize mwanakijiji.

Utajuaje kwamba yatosha kuchangia kabla hujajua kitakachochangiwa?
 
Umegusa ukweli mtupuuu..

Tufanyeje sasa kuondokana na hili kwa haraka ikiwezekana..? umetoa njia sahihii ya kutokutosheka kuhojiii,,namii naanza sasa kuanzia ngazi ya familia hadi kijamiii.

wabunge wetu ndo wanaoiniudhiii zaidiii jamaniiii...ni wepesi, wanafiki, waoga, malimbukeni wa kupigania maendeleo ya wapiga kura wao..Mfumoo mbovuu unaolea kwa nguvuu tabia hiyoooo..wachache bungeni (wapinzani) wameonyesha njia na wanaojiita wapiganaji wa vita ya ufisadi kumbe wenyewee rohoniii ndo mafisadiii zaidii basii tuu kutaka umaarufuuuuu kupitia media nyepesiii tulizonazoooooo..

Inaniuuma sana kiongozi wa serilaki anapohojiwa na waandishii huku wakimpa maswali ya kumpamba na kujipendekezaaaa......

inaniuumaa sana wanaojiita wapiganajii wa ufisadii ili hali wakiendeleaa kubaki chamani ambako uhai ni UFISADIIIII..

Inaniuumaa sana naposhindwaa kuwa jasirii kwa wakati na kupinga yale yotee nisiyopendezwaaa nayoooo...

...
Angalia usije hoji bila mantiki???
 
Hatupendi mambo ya kugonganisha vichwa; hatupendi kubishana na kuhojiana hadi mtu akubali kushindwa kwa hoja; tunapenda mambo mepesi mepesi.

Tunapenda mambo mepesi mepesi, tunapenda majibu mepesi mepesi. Ndio maana sasa najua kwanini ilikuwa vigumu sana kwa watu kumshinda Nyerere kwa hoja hadi kufikia kudai kuwa "haambiliki". Kumbe walikuwa ni wepesi wepesi. Si tunawaona leo jamani!

Tuamke!
Halafu kibaya zaidi ukipenda uliza unaonwa kama vile unajifanya unajua kumbe mtu pengine unauliza ili ujuzwe.

We are more of 'normatives' debaters rather than 'positive' ones. Nililiona ili nikasema nikisema watu watasema huyu Juma kazidi sasa, maana ukisema tu huko kwenye thread zingine unaonekana huyu nae. Kumbe mtu ni average thinker tu anaetaka opinion za wengine ili ujue.

Ni kweli atupendi kuumiza vicha, na tunapenda kusikia vile tunavyotaka kusikia vingine huwa vinaitwa pumba sasa humu ndani.
 
Utajuaje kwamba yatosha kuchangia kabla hujajua kitakachochangiwa?

MCHANGO HAKUNA NA WALA HAUHITAJIKI KTK THREAD HII KWANI NI UJUMBE AMBAO UNATAKIWA KUFANYIWA KAZI KWA KADA ZOTE.
Ndio nikasema kama umeguswa chukua hatua,kama hujaguswa jiulize kama upo kawaida na kama huelewi muulize mwanakijiji.
 
MCHANGO HAKUNA NA WALA HAUHITAJIKI KTK THREAD HII KWANI NI UJUMBE AMBAO UNATAKIWA KUFANYIWA KAZI KWA KADA ZOTE.
Ndio nikasema kama umeguswa chukua hatua,kama hujaguswa jiulize kama upo kawaida na kama huelewi muulize mwanakijiji.

Maneno yako yanadhihirisha zaidi Watanzania wanavyopenda nyepesi nyepesi.

Unataka kwenda kuufanyia kazi mchango na kusimamisha mabadilishano ya mawazo wakati mchango uko halfbaked.

Ndiyo hii hii spirit ya kujitia tuna majibu mepesi kwa maswali magumu inayozungumziwa hapa, kabla hatujamaliza kuongea, vunja mkutano twende ktatua matatizo tusiyoyajua.

Kama umeguswa au hujaguswa na nini? Kuna watu wanaweza kuja ku dispute the very essence of your reasoning, kwa nini unataka kuwa dictator? Kwa nini huruhusu watu waseme? Maana ya JF ni nini kama si kubadilishana mawazo? Kama wewe hutaki kubadilishana mawazo unafanya nini hapa JF?

Usitake kuziba watu midomo kwa guise ya hasty action, soma motto hapo juu, We dare speak openly.
 
Hata hapa JF wanapenda mambo mepesi, nimemuuliza slaa maswali watu wanakuja juu eti una-provoke mzee agh!

Anzeni hapa JF msiogope kuudhiwa labda tutabadilika
 
Kwa asili huwa hatuna uwezo wa kubeba mambo mengi kichwani kwa wakati mmoja ndiyo maana kila jambo jipya linaloibuka hutusahaulisha kabisa kuhusu tulilokuwa tunalishughulikia, ndiyo maana hata miradi mingi huwa inaishia hewani au hutulazimu kuimaliza haraka haraka ili turukie miradi mingine, ubora kwetu hauna umuhimu sana bali kumaliza jukumu ndiyo lengo letu.

Ndiyo kitu kimoja rafiki yangu amewahi kusema kuwa Watanzania tuna "attention span" ndogo sana. NI kama watoto, tukianza kukomalia kitu fulani tunarushiwa pipi tunasahau kile kitu kingine!
 
Hata hapa JF wanapenda mambo mepesi, nimemuuliza slaa maswali watu wanakuja juu eti una-provoke mzee agh!

Anzeni hapa JF msiogope kuudhiwa labda tutabadilika

Tumaini.. tatizo lako wewe huwezi kujaliana na watu bila kuwatukana na kuonesha dharau. Hoja haiwi na nguvu kwa sababu imeambatana na matusi na kejeli. Tunaposema tunabishana na kujadiliana haina maana ni lazima tutukanaane au kuitana majina ya uduni. Umeona juzi Warepablikani huko US wakijadiliana na Rais wao tena kwa uwazi kabisa bila kumtukana au kumuita mjinga na mpumbavu. Ni hoja tu.

Nadhani turudie ule msemo wangu wa mwanzo sana ambao naona siku hizi umepotea hapa Hoja Hujibiwa kwa Hoja, siyo Vioja!
 
What's new? Nothing, nada!

Mimi napenda Waingereza wanavyomchachafyaga waziri wao mkuu bungeni. Those are classic exchanges man. Especially now btn David Cameron and Gordon Brown. Loves it.
 
Kwa hili mimi sina tatizo nalo, maana kila liliosemwa kwenye hiyo mada hapo juu ni sahihi.Lakini tujiulize ni kwa nini tunapenda mambo mepesi mepesi na ya kishabiki?
Hapa siyo kwamba watu wanapenda kuwa hivyo na kushangaza hata wakuu wetu wengi hawajui kuwa wana mambo mepesi ila tataizo kubwa sana ni kwamba watu hatupendi kusoma ni wavivu kupindikia, hatufanyi tafiti ya jambo lolote tunalosikia au kuambiwa, ukisikia au kuambiwa hata bila kutafakari kuwa hilo jambo lina ukweli kiasi gani, wewe unakurupuka na kuanza kulisimulia kama vile ulikuwa kwenye tukio,upuuzi mtupu.
Na hili limejihirisha wazi wazi hata katika tasisi zetu kubwa, kama elimu ya juu, huko kudesa kote huko, kuvuja kwa mitihani, madokita kufoji vyeti ni matokeo ya watu kupenda mambo mepesi mepesi na si vinginevyo.kama huna cha kusema you better keep quite why to shout?
Remember "Half of the world is composed of people who have something to say and can't and the other half who HAVE nothing to say and keep saying it"
 
Ndiyo kitu kimoja rafiki yangu amewahi kusema kuwa Watanzania tuna "attention span" ndogo sana. NI kama watoto, tukianza kukomalia kitu fulani tunarushiwa pipi tunasahau kile kitu kingine!

I am not sure as to this being entirely about lack of attention span as much as it is about low expectations, accountability and standards. Basically complacency.

Si kweli kwamba watu wanasahau, wanakumbuka sana, ila wanakuwa kama wana give up katika kufuatilia.

Ndiyo maana mimi nika imention ile Maslow hierarchy of needs, ile iko very essential.Mtu hawezi kung'ang'ania mabadiliko ya katiba na vitu vingine fundamental kama hivyo wakati anaishi katika uchumi ulio wa subsistence existence.

Worse still, hata huko kwenye subsistence existence hakuna ambition ya kutaka kutoka kwenye a lower subsistence to a higher subsistence.
 
Tunapenda mepesi mepesi na ndio maana wajawazito wenye uwezo siku zao za kujifungua zikikaribira huenda Marekani na kukaa huko hadi baada ya kujifungua ndio wanarudi nyumbani Tanzania. Why? Kwa sababu wanataka watoto wao wawe raia wa Marekani. Kuwa raia wa Marekani kutarahisisha maisha ya watoto wao hasa kwenye mambo ya elimu, tiba, n.k.
 
Back
Top Bottom