Watanzania tunafuga paka anayeogopa panya, akiona panya anawaita paka wenzake waje kumsaidia.

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Ukiwa unafuga paka nyumbani kwako jaribu kumchunguza. Ukiona paka wako hakamati panya akiwaona anakimbia mpeleke kwa wataalamu wa tabia za wanyama. Inawezekana huyo siyo paka bali ni mnyama mwingine anaye fanana na paka. Basi! Inabidi umfukuze nyumbani kwako kwa sababu hana faida tena. Ukimuacha labda utakuwa umeamua awe paka wa urembo. Panya wanateketeza hazina ya mwenye nyumba ambaye ni paka, lakini anashindwa hata kuwatisha tu hao panya. Mpaka paka wadogo wadogo wapige kelele kule kwenye jumba lao kuu la mikutano. Aina hii ya paka hata akishikiwa panya hatamla. Maana amebadilika na kuiga tabia za paka wa kizungu. Nimejaribu kuweka fumbo ili MODS msije mkaifyekelea mbali japo ni nyepesi tu.
 
Nchi inaongozwa na Panya kuanzia juu mpaka medium level. Paka wamefungiwa kwenye banda lao.
 
Paka kachungulia dirishani na kujaribu kuwatisha panya walio nje. Wamemdharau na hakuna yeyote aliyekimbia.
 
Paka mkubwa ni paka shume ndiyo maana tunaomfuga tunampango wa kumfukuza nyumbani.
 
Ukiwa unafuga paka nyumbani kwako jaribu kumchunguza. Ukiona paka wako hakamati panya akiwaona anakimbia mpeleke kwa wataalamu wa tabia za wanyama. Inawezekana huyo siyo paka bali ni mnyama mwingine anaye fanana na paka. Basi! Inabidi umfukuze nyumbani kwako kwa sababu hana faida tena. Ukimuacha labda utakuwa umeamua awe paka wa urembo. Panya wanateketeza hazina ya mwenye nyumba ambaye ni paka, lakini anashindwa hata kuwatisha tu hao panya. Mpaka paka wadogo wadogo wapige kelele kule kwenye jumba lao kuu la mikutano. Aina hii ya paka hata akishikiwa panya hatamla. Maana amebadilika na kuiga tabia za paka wa kizungu. Nimejaribu kuweka fumbo ili MODS msije mkaifyekelea mbali japo ni nyepesi tu.
Tusiwalaumu dada zetu kuwa hawana maadili kwa sababu tu eti wanavaa nguo fupi. Kama imefikia hatua ya Watanzania kuitana paka na Panya nadhani ni zadi ya kushuka kwa maadili. Kila mtu ana mapungufu yake ila siyo ufikie kumuita Paka. duh, asubuhi yote hii tena jumapili? halafu ukitoka hapa unakwenda kuamudu au uliabudu Ijumaa? Katubu dhambi ya kumuita binadamu mwnzako panya.
 
Yupo paka moja mwenye makeke Mzitto K katoa kichwa nje panya wote tumbo joto!

Zitto hana ubabu huo ,mbali na azma yake ya kuutaka urais. Tsh milioni 600 alizokula wakati tume ya kuchunguza kashfa ya Madini ni Changamoto kwake, hapo anajaribu tu kufukia madhambi yake.
 
Tusiwalaumu dada zetu kuwa hawana maadili kwa sababu tu eti wanavaa nguo fupi. Kama imefikia hatua ya Watanzania kuitana paka na Panya nadhani ni zadi ya kushuka kwa maadili. Kila mtu ana mapungufu yake ila siyo ufikie kumuita Paka. duh, asubuhi yote hii tena jumapili? halafu ukitoka hapa unakwenda kuamudu au uliabudu Ijumaa? Katubu dhambi ya kumuita binadamu mwnzako panya.
Tatizo la paka wadogo kulaumiana... Yaani paka huwa hatafuti sababu ya kwa nini anaitwa paka! Yeye siku zote anawatisha wanaomuita paka hata kwa kutumia dini. BADALA YA WEWE USIYEKAMATA PANYA KUTUBU, UNAWATAKA WANAOKUONA WEWE HUKAMATI PANYA WATUBU...! Haya ni maajabu
 
Tusiwalaumu dada zetu kuwa hawana maadili kwa sababu tu eti wanavaa nguo fupi. Kama imefikia hatua ya Watanzania kuitana paka na Panya nadhani ni zadi ya kushuka kwa maadili. Kila mtu ana mapungufu yake ila siyo ufikie kumuita Paka. duh, asubuhi yote hii tena jumapili? halafu ukitoka hapa unakwenda kuamudu au uliabudu Ijumaa? Katubu dhambi ya kumuita binadamu mwnzako panya.

Wewe mwenyewe unajiita kenge. Inamaana wewe ni kenge kweli, Paka ni jina lenye sifa kuliko kenge. Sisali ijumaa, juma mosi, wala jumapili. Wewe hujui ushairi, ukiambiwa umtaje huyo paka ni nani unajua? Mi nimemaanisha paka mnyama, kwani nchi hii haina paka? Kama umeelewa vibaya kalagabaho na uboza wako.
 
Ukiwa unafuga paka nyumbani kwako jaribu kumchunguza. Ukiona paka wako hakamati panya akiwaona anakimbia mpeleke kwa wataalamu wa tabia za wanyama. Inawezekana huyo siyo paka bali ni mnyama mwingine anaye fanana na paka. Basi! Inabidi umfukuze nyumbani kwako kwa sababu hana faida tena. Ukimuacha labda utakuwa umeamua awe paka wa urembo. Panya wanateketeza hazina ya mwenye nyumba ambaye ni paka, lakini anashindwa hata kuwatisha tu hao panya. Mpaka paka wadogo wadogo wapige kelele kule kwenye jumba lao kuu la mikutano. Aina hii ya paka hata akishikiwa panya hatamla. Maana amebadilika na kuiga tabia za paka wa kizungu. Nimejaribu kuweka fumbo ili MODS msije mkaifyekelea mbali japo ni nyepesi tu.

Too late hayo sasa majungu, tunachosubiri sasa ni Baraza jipya la Mawaziri, umbea huu ungeuandika kabla CC ya CCM haijakaa. Ndiyo maana Tanzania ni mfano wa kuigwa katika mfumo mzima wa uongozi. Rais hawezi kukurupuka kutoa maamuzi wakati na yeye ana Chama kama ilivyo kwa Vyama vingine, lazima akitaarifu chama chake azma ya kufanya mabadiliko. Hongera Jk kwa busara zako.
 
Wewe mwenyewe unajiita kenge. Inamaana wewe ni kenge kweli, Paka ni jina lenye sifa kuliko kenge. Sisali ijumaa, juma mosi, wala jumapili. Wewe hujui ushairi, ukiambiwa umtaje huyo paka ni nani unajua? Mi nimemaanisha paka mnyama, kwani nchi hii haina paka? Kama umeelewa vibaya kalagabaho na uboza wako.
Ni mnyama kweli ila KIBOGOYO!
Uzi wako umenifurahisha
 
Too late hayo sasa majungu, tunachosubiri sasa ni Baraza jipya la Mawaziri, umbea huu ungeuandika kabla CC ya CCM haijakaa. Ndiyo maana Tanzania ni mfano wa kuigwa katika mfumo mzima wa uongozi. Rais hawezi kukurupuka kutoa maamuzi wakati na yeye ana Chama kama ilivyo kwa Vyama vingine, lazima akitaarifu chama chake azma ya kufanya mabadiliko. Hongera Jk kwa busara zako.

Duh! Aisee hii kali, Tz ni mfano wa kuigwa! Unazungumzia utawala bora upi? Nilitegemea baada ya maamuzi ya CC waliotajwa kwa ubadhirifu wangeanza kuachia ngazi wenyewe. Sasa subiri hilo baraza lako jipya la mawaziri.
 
Back
Top Bottom