Watanzania tumeshindwa na wakenya wameandamana kupinga ufisadi???

As a matter of fact, kwa wakenya ni zaidi ya ufisadi kunaissue nyingi zinachanganyika. Kwanza bado wanaishi kichuga chuga kutokana na athari za baada ya uchaguzi na hata baada ya kazi ya kuwasuluhisha bado kuna watu hawajakubali matokea na visasi vimejaa humo.

Kwa kuwataka watanzania kuandamana kwa sababu wakenya wameandamana, kwanza watake radhi watanzania kwani matatizo yao sio sawa na Kenya. Ziko bifu za kikabila hapa bongo lakini sio kama Kenya, vyama vyenyewe vinasuguana sio kivile ndio maana hata Dr. Slaa unaona yuko chadema mkewe CCM kenya hili haliwezekani.

Lazima mkubali mfumo wetu wa kupambana na matatizo yetu sio kututaka tubebe kila kitu kutoka nje. Kama ipo haja ya kuandamana tuandamane kivyetu na zipo njia nyingi za kupinga ufisadi si bora tusiwape kura mafisadi au tucopy ya china wakikutia hatiani wanakutoa roho.
 
Hoja yangu siyo kwamba tukopi lakini nia yangu iko pale pale kwamba wanaharakati wetu wanatuangusha kwa uoga. Nilishuudia wananchi wana andamana kumpongeza na kumpokea CHENGE NA LOWASA walipo jiuzuru nilitegemea tungeandamana kuitaka serikali iwafunge haraka kwani imethibitika wameliingiza taifa ktk hasara kubwa.

Ukabila wa kenya tuwaachie wenyewe lakini ktk kupambana na ufisadi na wizi wa mali ya umma lazima tukubali sisi tunasinzia tu wakati wenzetu wameisha amka!!
 
Mahakama za Bongo si ndiyo kungine huko kulikojaa usanii wa hali ya juu na rushwa ya kutisha. Umeshasikia zile kesi za mafisadi wa EPA zikitajwa hivi karibuni!? Baada ya jamaa kushinda tena kwa kishindo hapo October 2010 zile kesi zote za zitafutwa.

Bubu your statement is too prejudicial be careful !!!!!!!!!!!
 
"WATANZANIA NI WAJINGA,WAVIVU WA KUFIKIRI NA WANA WIVU WA KIKE" by former president BWM

Uandamane utaanzia wapi wakati sifu zenu zinajulikana.
 
Tunapenda mepesi mepesi,maandamano ambayo yanaambatana na pilau na pesa ndio yanayotuvutia zaidi.Haya mengine ambayo huambatana na gari la upupu,mabomu ya machozi,virungu etc etc tunayaogopa kwani tuliisha aminishwa kuwa Tanzania ni nchi ya amani na utulivu.
 
Back
Top Bottom