Watanzania tumejipangaje na umaskini, bajeti mpya?

JE NI SAWA KILA KIJANA WA KITANZANIA KUJIFUNZA KILIMO?


  • Total voters
    2
Ni kweli kabisa unayosema. Ubize wa mtaani una-reflect hali ya uchumi ya mahali hapo. Tukumbushane mitaa kama Tunduma, Tukuyu, Soweto ya Mbeya, Kongo Kariakoo n.k. Pitapita Ilivyokuwa mwaka wa jana imepungua sana mwaka huu. Ukipanga hata nyanya na vitunguu haviuziki. Raha ya kijijini ukute watu wako bize na skill zao. Ukute seremala, mwashi, fundi cherahani n.k. wako kila mtu hapa au pale wakiingiza kipato. Kwa sasa kila kitu kiko at stand still. Kuna mshtuko fulani (shock). Shock kuu ni ya kisiasa ambayo inatokana na makaripio na matamko ya mara kwa mara. Kukosekana kwa semina elekezi kumefanya wateuliwa wengi kubaki bila kujua la kufanya zaidi ya kufoka na kutishana. Shock ya pili ni hii hali ya hewa. Mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo mwananchi analaumiwa zaidi kama kisababishi, hajaletewa majibu na serikali ya nini kifanyike mbali na utawala mzima kuongelea upandaji miti. Tatu ni mtindo wa ukusanyaji kodi ambao ume - paralise system nzima. Halmashuri zimeachwa bila kitu. Raia wa kawaida anapata hamasa anapoona halmashauri yake inafanya vitu vya maendeleo kila uchao. Sasa hivi kila kitu maamuzi yanatoka top notch. Viongozi wa local government kazi yao ni kutuhumiana na kufungana. Kweli hatutafika.
 
Hayo mawazo Kama vile Ni rahisi Sana kwenye utekelezaji ,kuna sehemu maji ya kunywa Ni mpaka mvua inyeshe ,ukifika huko utakuja ufute thread yako,,kilimo ,kilimo Ni sawa,kilimo nacho kinahitaji nyenzo ,mtaji n.k,Kama upo mbeya tukuyu Na maeneo mengine yenye hali ya hewa nzuri kwa kilimo usifikirie kwa sehemu uliopo tu,waulize Wenzako wa simiyu ,kagera Na kigoma Na singida hata Dodoma Na Lindi ,wanawezaje kuyafanya yote hayo?

Kuna Mazao yanayostahimili ukame Na pengine hata kilimo cha umwagiliaji,hivyo visima nan kavichimba?sio kila mtanzania anaishi kando kando Na mto.

in reality kinaweza kutukomboa,but as for now it's too late bado mifugo haijafa kwa njaa,kumbuka mifugo inakula kuliko binadamu Na inategemea malisho Na mfuko wa mwanadamu,au umwagiliaji hadi wa Nyasi ufanyike??

Green house sio rahisi Kama ufikiriavyo,Ni expensive.anyway mawazo yako Ni mazuri but jaribu Fanya analysis ya environment ,capital Na and other prerequisites .
 
Back
Top Bottom