Watanzania tulipotoka,tulipofika na tunapokwenda tusisahau haki na wajibu wetu

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Watanzania tulipotoka ,tulipofikia na tunapokwenda tuna hitaji umakini katika maamuzi magumu ya kubadilisha mfumo mzima wa uongozi wetu ili ulete tija kwa ustawi wa taifa na watu wake.Tumekuwa mabingwa wa kulalamika bila kuwajibika katika kuhakikisha tunatumia dhamana yetu vizuri ya kusimika viongozi wetu.

Siku zote haki huenda na wajibu na huwezi kwenda kushoto tu,lazima huende kushoto kulia na ndivyo inavyotakiwa haki wajibu.Tunatumia haki yetu vibaya kila tunapopata fursa ya kuchagua viongozi wetu lakini tunasahau wajibu wetu ni kuimarisha Uongozi wa nchi kwa kuchagua viongozi wazalendo wenye uchungu na nchi yao.

Tukikubali kununuliwa na kupangiwa bei kwa kila mpiga kura tujue tunaipeleka nchi sivyo ndivyo.Leo hii wapiga kura wetu wanathubutu kutumia wajibu na haki yao kununuliwa kwa thamani ambayo haitoshi hata mlo mmoja kwa siku.Nini hatari yake,hatari yake ni kurudisha kwanza gharama na kupata faida ndipo hukumbukwa mlalahoi huyu mpiga kura kwa kuwa tu alikubali kufanywa sehemu ya biashara ya kiongozi huyo aliyechaguliwa.

Mchezo huu na biashara chafu ya kununua uongozi itamalizika pale tu wananchi watakapo jua haki na wajibu wao katika hatima ya uongozi wa nchi hii.Matokeo ya uongozi mbovu ni kuhamisha pesa za nchi na kuzificha kwenye mabenki ya nje huku watanzania wakikosa dawa,madaktari waliopewa dhamana ya afya ya taifa kugoma na watoto wetu kusoma ili kupata bora elimu.

Nini tufanye kuinusuru hali hii,hali hii itanusurika tu mara tutakapo weza kujitambua na kujua wajibu wetu katika mustakabali wa mapinduzi ya uongozi dhidi ya watawala dhalimu wanao kula bila kunawa.Kimebaki kipindi kifupi awamu ya nne imalizie muda wake,je Watanzania tumejifunza nini kutokana na utawala huo uliojaa migomo na wizi kila kona ya nchi hii.Taifa linapoteza nguvu kazi yake kwa kupoteza watu wanao kufa kutokana na mgomo wa madaktari ilihali rais wa nchi akikwea pipa kwenda nje ya nchi.

Uoga huu ambao ni silaha dhaifu isiyo ugopwa na watawala utatutoka lini miongoni mwetu.ahitaji degree kujua nchi yetu inaliwa na makupe wachache wanao jaribu kutugawa kwa itikadi za kidini na kikanda.Movement for change isishie kwa vyama vya kisiasa bali iwe ndiyo kauli mbiu halisia ya kujikomboa miongoni mwetu na kuacha ile dhana hata hawa tukiwachagua watakuwa kama hawa tu.

Serikali dhalimu siku zote ni matunda ya wanachi madhalimu ambao wasio wazalendo ambao wamekubali kuulea udhalimu huo kwa kuwabakisha madhalimu hao madarakani ili hali wameshindwa kutuonyesha nchi ya kuweza kupata unafuu wa maisha.Viva Watanzania viva,ukombozi wa kweli hautaongozwa na vyama vya siasa bali tukijikomboa na kujitambua,tutafanya maamuzi ya kizalendo kwa kuwaweka wazalendo wa kweli na kuwafikisha mbele ya sheria wale waote waliogeuka kupe na kunyonya mali za Watanzania

 
Nadhani ktk kuyafikia yote hayo ni jukumu letu waTz wote kwa pamoja kuwa wamoja na kuhakikisha elimu hii ya kuitambua haki yetu na M4C anaipata kila mTz then kitakachofuata itakuwa ni kama kumsukuma mlevi ktk kuwang'oa hawa kupe
 
Watanzania tubadilike,hata vitabu vitakatifu vinaonya,ole wake anayeikana haki yake Mungu atamnyima baraka.
 
Back
Top Bottom