Watanzania Tujitambue,Tubadilike na Tusonge Mbele Tujenge Nnchi..!

Tanzaniaist

Senior Member
Nov 29, 2011
161
156
Habari Ndugu zangu..,
Leo napenda kutoa la Mayoni Pamoja na Maoni Kuhusu sisi Watanzania na Nnchi yetu Iliyojaawaliwa kila aina ya Rasilimali Pamoja na Watu waliojaaliwa upendo,Amani na Umoja!

Kwanza Watanzania lazima tuondoe dhana ya neno "Kichwa cha mwendawazimu",lazima tujiamini kwamba tunaweza kwenye kila jambo,Tusiogope kudhubutu! Umaskini sio sababu ya kila siku Tanzania ni kuwa ni nnchi yenye matatizo!
Uchaguzi umeshapita mwaka 2010..,.,sasa tujenge nnchi nawaomba viongozi wangu wa CCM,CUF na CHADEMA huu ni muda wa kushirikiana sio muda wa kutafuta umaarufu wa kisiasa,kulipuana na kunyoosheana vidole! LETS BUILD OUR COUNTRY TANZANIA
Tuna changamoto mbalimbali barabara,umeme,ajira,elimu,uchumi pamoja na uhufadhi wa rasilimali...
Napenda niseme kwamba kila raia wa Tanzania ana jukumu na wajibu katika kulitumikia Taifa lake...,IF YOU AR A TANZANIAN KNOW THAT UR COUNTRY NEEDS YOU!
Iwe mwanasiasa,mwanamichezo,msanii,madaktari,mainjinia,waalimu,mapolisi,maaskari na watu mbalimbali ambao wana jukumu kulitumikia Taifa Lao...,Na jukumu kubwa ni kwa viongozi wetu kwaanzia Raisi,mawaziri,wabunge pamoja na viongozi wa dini na kwenye asasi mbalimbali za kiserikali...,Majukumu yao wanayajua vizuri mfano wanauona kwa nnchi mabalimabli mfano jirani yetu RWANDA ambayo juzi kati ilikuwa ni kisima cha mauaji ingawa watu wanasema kwasababu RWANDA ni ndogo ndio lazima iendelee..hiyo sio factor bali the factor is GOOD GOVERNANCE AND LEADERSHIP..mbona BURUNDI NA DJIBOUTI au GAMBIA ni nnchi ndogo lakini bado ni maskini..

Ifike muda Serikali ipunguze gharama zake za kila siku ikiwamo posho,magari ya V8 vitu ambavyo ni mzigo mkubwa serikalini HAINA MAANA KUNUNUA SUTI YA LAKI TANO WAKATI UNA SHINDIA MLO MMOJA KWA SIKU,.... tuelekeze katika kushughulikia matatizo ya wananchi na kuwa na VISION YA MIAKA ISHIRINI sio kuplan kitu cha miaka mitano!

Kwa wale waliofika Dubai...mji wao wameuwekea vision ya miaka 20 ijayo! sisi watanzania wataalamu tunao ingawa pesa ni kidogo lakini tujibane! Serikali yetu ina changamoto kubwa sana ikiwamo uadilifu,Usimamizi,Uthubutu na Mipango bora kwa wananchi wake...
Na kwa wale Watanzania wenye vipaji kama wanamichezo,wasanii,kazeni buti,..nawapa big up wasanii wachache kama A.Y,LADY JD,ALLY KIBA kwa kuitangaza vizuti nnchi yetu pamoja na waigizaji kama Kanumba! ila wenzetu wanasoka kazeni buti atleast nizar khalfan anatuwakilisha marekani...,pia niwapongeze baadhi ya wasomi kama mtoto wa bob makani aliyepata tuzo juzi kule marekani!..hii ni changamoto kwa watanzania wenye vipaji...

Na mwisho huu ni muda wa kuchapa kazi...,wengi wetu hatuna time management! tuelekeze muda mwingi katika mambo yenye maendeleo tupunguze siasa ndugu zangu watanzania! tunaona ndugu zetu wachina wanavyofanya kazi kama sisimizi...hili ni jukumu letu sote! kama mkulima fanya juhudi..iwe mhasibu,manager,na nk..tuchape kazi tujenge nnchi jamani tuisapport serikali yetu kwa mapato zaidi ili serikali yetu ipate kodi zaidi na fedha zipelekwe katika miradi yenye kutuletea maendeleo!

NAPENDA KUWASILISHA...samahani nini kwa thread ndefu...
 
huu si mda wa kuchapa kazi kama unavyotaka kutuaminisha,huu ni mda wa kuwaweka pembeni wale wote ambao tumekuwa tukichapa kazi lakini wanafaidi wao na familia zao hizo kazi.In short ni mda wa kuweka magamba pembeni ndo tuanze kuchapa hiyo kazi.FREEDOM IS COMING TOMORROW......
 
Mwandishi umeongea ukweli lakini mimi naona kuna matatizo makubwa mawili au matatu

1. Utamaduni: Watanzania tuna utamaduni wa kuongea kuliko kutenda mfano mzuri ni swala la umeme kila kiongozi anaongea miaka nenda rudi lakini mpaka sasa kuna mgao
2. Ubinafsi: Watanzania wengi hasa walioko madarakani hawna uchungu na nchi hivyo kuna vitu vingi muhimu vya kimaendeleo havifanikiwi kwasababu ya ubinafsi wa kujifikia wenyewe bila kujali taifa.
3. Uongozi: Tanzania hatuna viongozi wazuri na tunachagua viongozi kwa ushabiki na kujulikana bila lkujua kama wana uwezo wa kuongoza. Vilevile kuna uzembe sana kwenye sheria kwani watu wengi hawapati adhabu hata pale wakijulikana wamekula rushwa!. Viongozi Tanzania wanahamishwa sehemu kama wamekula rushwa lakini wengi hawafukuzwi.
4. Serikali: Serikali Tanzania ni tatizo kubwa sana kwani imepewa nguvu na wanaitumia kudidimiza wananchi na maendeleo mfano Kujenga ni njia kubwa sana ya kukuza uchumi lakini ni vigumu sana kupata kibali cha kiwanja Tanzania kwasababu ambazo mpaka leo hazieleweki vizuri. Watanzania wengi wamejitahidi wanataka kujenga lakini wanazungushwa na viwanja kucha bila kujua mbele wala nyuma. Hili swala linarudisha sana nchi nyuma kwani hapa tatizo si watu ni serikali.Vilevile kuna swala kama la elimu je ni kwanini serikali inaruhusu shule za binafsi za sekendari zifanye kazi bila walimu na zinafellisha kila siku lakini serikali sasa inafikiria ada tu badala ya elimu!
Kama Tanzania haitapata viongozi kama magufuli au Kagame wa Rwanda badala yake ni viongozi wa kuchekeana na upole wa kinafiki nchi yetu haitabadilika. Imefikia wakati kwamba kula rushwa ni sifa na serikali haifanyi lolote na kama sheria ya rushwa haina nguvu hakuna lolote litakalofanyika kwani watakaopata bishara ni wajuanao na kama hakuna ushindani basi hakuna capitalism.
 
Back
Top Bottom