Watanzania tubadilike sasa

African

Member
Oct 22, 2008
95
4

ASKOFU mkuu wa kanisa la full gospel bible fellowship.Zacharry Kakobe, ameibuka na kuwataka watanzania kutoogopa kufanya mabadiliko ya utwala wan chi kwani ndiyo siri ya mafanikio kote duniani
Akitoa mahubiri kwa waumini wa kanisa hilo jana mjini Dar es Salaam, Askofi Kakobe alisema mabadiliko ndiyo njia pekee ambayo inaweza kumtoa mtu kweny hali moja kwenda hali nyingine
“Nawaambia waumini wangun na watanzania kwa ujumla kwambaa msiogope kufanya mabadiliko kwani ndiyo siri ya mafanikio duniani yaliyojjificha…watu hatupaswi kuogopa mabadiliko kwani maendeleo huja baada ya majaribio” alisema Askofu Kakobe
Akitoa mfano,Askofu Kakobe alisema nchi nyingi zikiwemo Marekani,Uingereza,Ufaransa,Kenya,Ghana na Zambia zimethubuti kufanya mabadiliko kwa maendeleo yao.alisema wanasiasa wamekuwa wakitumia uelewa mdogo wa wananchi kuwalisha siasa nyepesi kwa manufaa yao.
Alisema wanasiasa wamekuwa wakitumia uelewa mdogo wa wananchi kuwalisha siasa nyepesi kwa ajiri ya manufaa yao.
Akifafanua zaidi, Askofu Kakobe alisema siyo kweli kama inavyoelezwa kwamba wapinzani wakishika madaraka, amani ya nchi inaweza kutoweka na kusisitiza kuwa si kweli kwani hizo ni siasa nyepesi za wanasiasakutukima ujinga wa wananchi.
Mbona Obama(Rais wa Marekani)ameingia madarakani baada ya miak 222 ya uhuru wa taifa hilo,mbona amani haikutoweka…nadhani mtu akiondolewa na kukaa pembeni kwa miaka mitano atajuta,lakini taifa linasonga mbele.
Wengine wanadai amani itatoweka hili halina ukweli,chanzo kikuu ni viongozi kukataa matakwa ya wengi,alisema Askofu Kakobe katika sehemu ya mahubiri yake
Akasema hata wale wanaobedha ahadi ya mmoja wa wagombea kwamba kama akisinda atatoa elimu,afya bure yote hiyo ni siasa nyepesi kwani enzi za hayati baba wa Taifa wanafunzi akiwemo yeye kusoma bure
Licha ya askofu Kakobe kutotaja jina la mgombea aliyemkusudia,lakini mgombea urais katika uchanguzi mkuu ujao,mwenye sera hiyo ni Dr.Willbrod Slaa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Ndugu waumini nakumbuka enzi za mwalimu Nyerere tulikuwa tunasoma bure, mimi ni shahidi wa hili ilikuwa mwanafunzi anatoka Bukoba(Kagera) anakwenda Masasi (Mtwara) akifika ndani ya basi anaonyesha karatasi ya serikali (school warrant)anapanda gati….hata shuleni maisha maisha yalikuwa mazuri wakipata kila kitu(free of charge)…iweje leo waseme haiwezekani? Alihoji Askofi Kakobe.
Alisema kupanga ni kuchagua,hivyo akawataka waumini wake na watanzania kwa ujumla kufanya maamuzi sahihi ili wasije kujuta baada ya kipindi cha miaka mitano.
Nawaambieni kupanga ni kuchagua,siasa hizo nyepesi zikibaki kwenye ujinga wetu tutaendelea kuumia na hakutakuwa na wa kumlaumu hata Mwenyezi Mungu hawezi kulaumiwa kwa sababu amewapa akili kama wanadamu kuchagua viongozzi wa kuwaongoza
“Hakuna uzoefu katika urais,Obama aliingia akiwa hana uzoefu wowote,hata Nyerere wakatu anakabidhiwa nchi kutoka kwa wakoloni pia hakuwa na uzoefu na hata Nelson Mandela,hivyo hakuna kiongozi anayeingia madarakani na uzoefu lazima tuwe makini” alisema Askofu Kakobe
Akifafanua kuhusu usafi wa wagombea,alisema kuna aina mbili za usafi ukiwemo wa kiroho na kisiasa,lakini akawataka waumini wake kumchagua kiongozi mwenye kipaji atakayeleta mabadiliko bila kujali kama ana mke au hana kwa sababu suala hilo halimo kwenye kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Hatuchagui malaika wa kutuongoza,kwa sababu tukizungumzia ugoni,wapo wenye vipaji vya kuwatoa wananchi kwenye matatizo kama alivyofanya Nelson Mandela aliyewatoa wananchi wa Afrika Kusini kwenye ubaguzi wa rangi…angalia nchi hiyo ilivyoendelea,hata ikafikia hatua ya kuandaa fainali za kombe la Dunia suala amabalo ni gumu kwa wazungu” alisema Askofu Kakobe
Kwa kuzingatia hayo,uchaguzi ni kitu muhimu kwa wananchi katika kuleta mabasdiliko wanayotaka,hivyo kwa vile uchaguzi mkuu utafanyika jumapili ya oktoba 31,Askofu Kakobe amefuta ibada kwa siku hiyo na siku moja kabla ya zoezi la kupiga kurandiyo kanisa lake litafanya ibada.Alisema katika uchunguzi wake alioufanya amebaini kitendo cha uchaguzi kufanyika jumapiliwaumini wengi hawapigi kura,ndiyo maana mwaka 2005 zaidi ya watu milioni 5 ambayo ni sawa na asilimia 30 hawakujitokeza kupiga kura.
 
Back
Top Bottom