Watanzania ni vipofu na viziwi

rastaman

Member
Nov 1, 2010
41
0
Jamani watanzania wenzangu. Naomba tusijifanye vipofu na viziwi wa kutokuona na kusikia na kuchambua mambo. Hii inaonyesha ni kiasi gani watanzania wengi tulivyo na udhaifu wakuchambua mambo. Hatuangalii mambo kutoka kona tofauti, kutafakari na kujua ukweli uko wapi. Hii ndo imenipelekea kuandika thread hii. La sivyo tunafata tu ushabiki au kutokuwa na elimu yakutosha hivyo tunakurupuka tu kutoa lawama kwa kundi fulani katika jamii.

Mimi kwa kuona kwangu tukubali tusikubali Tanzania si swali kabisa. hilo halina Mjadala. Kuandika Habari za wabunge wa chadema kutoka nje ya Bunge wakati Kikwete alipokuwa akianza kuhutubia bunge si dhani kuwa ni kitendo ambacho mtu mwenye akili ya uelewa wa siasa anaweza akaliona kama ni kosa. Nashangaa kuona hata vyombo vya habari kuandika kwa ushabiki tu kutaka kuwashambulia wabunge wa chadema. Tanzania ni yetu sote.. hicho wanachadema wanachokipigania si kwa ajili yao na familia zao. ni kwa ajili ya wantanzania wote( mimi wewe na watoto wetu).
Hapa tujaribu kuangalia chanzo cha matatizo haya nini, ndipo tuongelee kitendo cha wabunge wa chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge. Kwa mtazamo wangu Chanzo cha matatizo kinajulikana. ni Kwamba CCM wamekuwa wakandamizaji wa jamii. kwa kujiona wao tu ndo wenye haki ya kuingoza nchi kitu ambacho si kweli. CCM wanaogopa challenges; ndiyo maana haya yanatokea. Kama watanzania wenzangu mnafuatilia, DR. Slaa alisema wao wanchotaka ni kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi, na Katiba ibadilishwe kwani katiba tuliyo nayo haiendani na hali halisi ya siasa ya vyama vingi.
Cha ajabu CCM na baadhi ya watanzania wenzangu kuona kuwa hivi vitu viwili ndicho chanzo cha matatizo, watu kama Makamba anaropoka tu.. ohoo tutawatungia sheria wafukuzwe bungeni. (wewe Baba kama huna welewa wa mambo au shule uliyonayo ni ndogo; elimu haina mwisho nenda shule usome labda utaongeza upeo wa kujua mambo.)

Kama Kama kuna mtu yuko Karibu na Kikwete na anatembelea hii forum, basi amfikishie ujumbe huu. Tusisubiri mpaka damu imwagike ndipo washinikizwe na mataifa ya nje kubadili katiba. au kuunda tume huru. Demokrasia ya Tanzania iletwe na watanzania wenyewe siyo mataifa ya kigeni.
Baba Kikwete mbona wewe ni msomi mzuri tu? Kwa nini unakuwa mgumu kuelewa?
Kama mnavyo tangaza kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani basi muonye kwa vitendo. wasomi siku zote wanakubali challenges, mimi nitasikitika kuona msomi kama wewe hutaki challenges katika uongozi wako. Wasikilizeni wapinzani. siasa siku zote zinaenda na wakati baba. kubaliana na hilo. Tusisubiri kushuhudia machafuko wakati muda na uwezo wa kuchukuwa taadhali kuyaepuka hayo tunayo.


Peace and Love
 
Back
Top Bottom