Watanzania naombeni tumuunge mkono Rais kwa hili.

Nero

Member
Apr 24, 2012
93
21
Mara kadhaa niliwahi kumsikia mhe. Rais akisisitiza ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu-Loliondo-Mugumu road, sambamba na kuwepo pingamizi toka kwa watu/mataifa mbalimbali. Baada ya watu wengi au mataifa mbalix2 kupinga ujenzi wa barax2 hii 'The serengeti high way' basi mkuu wa nchi aliafiki kwamba barax2 hii itajengwa na itaishia Loliondo badala ya kukatiza Serengeti. Ndugu zangu nimeleta thread hii mbele yenu ili tumuunge Rais mkono kwa hili. Nasema hivyo kwa sababu moja kubwa (ziko nyingi), tatizo la usafiri kwa wananchi/watanzania wa wilaya ya NGORONGORO. Hakika hii ni wilaya ambayo kwa tanzania bado ipo nyuma sana kimaendeleo pamoja na kuwepo rasilimali mali asili nyingi, mashirika makubwa ya umma mfano: NCAA, makampuni ya kitajiri like: OBC, SERENA, ANDBEYOND etc.lakini imekuwa ikiwanufaisha wachache (mafisadi). Hivi majusi nilipata kushuhudia wananchi wanaosafiri kwenda Loliondo wakitezeka kusubiri usafiri wa kwenda huko kwa takiribani masaa 12 bila mafanikio(pale stendi Arusha karibu na uwanja wa S.A.karume). Nilijaribu kudadisi nikapata taarifa kuwa barax2 kwa sasa ni mbovu na karibu mabasi yote yanayokwenda huko yamekuwa yakiharibika njiani. Zaidi nikapata habari kuwa barax2 za ndani nazo hazipitiki. Mfano:mwananchi toka tarafa ya ngorox2 akitaka kwenda makao makuu ya wilaya(Loliondo) inabidi akalale wilaya ya Monduli ndipo apande mabasi ya kwenda Loliondo kupitia ziwa Natron. Ombi langu, watanzania tuunge mkono ujenzi wa barax2 hii kwani itapunguza matatizo ya watanzania wenzetu na kuwaletea maendeleo. Karibuni
 
Asante kwa thread, ila nakupongeza wewe kwa kuwa na moyo wa huruma kwa watz wenzako. Waache waonje utamu wa ccm naamini 2015 watapata akili. Nauunga mkono mtu d....u kwa 100 percent.
 
Hahahahaaa!!!!ccm mwisho wenu, hamna haja kuwaunga mkono. Mmevulia kwa sana
 
Kwa hiyo unataka tumuunge mkono katika kuboresha mawasiliano ya kwenda hotelini kwake huko Serengeti??? Unataka tumsapoti kunogesha biashara zake na waarabu ili twiga waendelee kusafirishwa kinyemela!!!????
 
Kwa hiyo unataka tumuunge mkono katika kuboresha mawasiliano ya kwenda hotelini kwake huko Serengeti??? Unataka tumsapoti kunogesha biashara zake na waarabu ili twiga waendelee kusafirishwa kinyemela!!!????
Hi kali nimeipenda, mleta mada hope ni mtoto wa mtu dhaifu kaja na mbinu ya ukosefu wa miondombinu ktk wilaya tajwa.
 
Siwezi kumuunga mkono Mh wenu huyo,Serikali waimalishe miundombinu yake wasiwatese wananchi.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom