Watanzania nani katuloga ?

Mzee Muganyizi, ukisoma toka mwanzo utaopna hotuba ya Mkapa ndiyo ilisema kuwa mwaka 2010 ni 50% wanawake 50% wanaume. Kama alikuwa nataka usawa huo mbona kwenye madini alikuwa kichwa ngumu? 97% wazungu/mawaziri na 3% percent ya nchi lakini kati ya hiyo 1.9% ni za Stelwart Mwingereza yaani 3%-1.9%=1.1% ndizo fedha halizi za watanzania. Upo hapo mzee Muganyizi??

hapa ndipo ninakubaliana na Mkwawa kuwa mzee kipra alikuwa anafuata ya mama. yeye Rais wa Wanaume mama rais wa wanawake!



CHA AJABU JK AMESEMA ATAENDELEZA YOTE YA MKAPA. SASA HUKO KUPITIA MIKATABA NI DANGANYA TOTO MAANA HIYO HAIKUWA SERA YAO BALI YA cuf NA CHADEMA. KWA HIYO CCM ITWASHINDA MAANA HAWANA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WAKE.


kwa kuwa anaendeleza yote ya Mkapa sasa lawama zote ni kwake maana watanzania mwaka jana walimchagua yeye na siyo mkapa. KAMA ALIKUWA NAKUJA KUENDELEZA YOTE YA MKAPA NA WALA SIYO MAZURI BALI YOTE. JE MI KWANINI CCM HAWKUACHA MKPA AENDELEEL KUGOMBEA URAIS?

NINAOMBA JIBU.
HADI MLE MAJANI NDEGE ITANUNULIWA TU!!!!
 
Mkuyuga wale jamaa ni wamarekani si waingereza. Ila neno moja ambalo nimekubaliana na wewe ni kwamba hatukua na haja ya kuchagua Rais ama CCM hawakuwa na haja ya ksuema mabadiliko kwa kuwa JK sasa baada ya kukwaa ufalme anasema anafanya yaleeeeeeeeeeee ya Mkapa.Sasa sitaulizia tena madini wala mikataba maana si sera ya CCM hii wala Mkapa hakuwa na mpango wa kutangaza mambo hadharani na kwa kuwa JK ni chapa Mkapa basi mimi nimenawa naenda kucheza bao tu .
 
Hapo kaazi kweli kweli! yaani ndege nyingine inanunuliwa and at the same bodi ya mikopo inasema haina hela za kukopesha wanafunzi wote wanaopata nafasi katika vyuo vyetu. This is ridiculous!
 
Wanabodi ,

Ndio maana kichwa cha habari cha hii mada niliuliza ni nani aliyetuloga watanzania ? Yaani JET ya pili serikali inataka kununuliwa wananchi wamekaa kimya tuu , vyama vya upinzani mko wapi kwa nini msitumie hii ishu ya kununua ndege na kukatwa kwa mikopo kwa wanavyuo kwa manufaa yenu.

Jamani ni jambo la kusikitisha sana wakati waziri mkuu wa uingereza moja ya nchi tajiri duniani anapanda BA katika shughuli zake mbali mbali, sisi watanzania tunafikiria kununu JET ya pili ! Jet ya pili kusudi wafanyie nini ? kwa nini hawa viongozi ni maselsfish kiasi hiki .

Mzee ES siulisema JK hapendi kuitumia hiyo ndege kwa sababu ya running cost ! Mimi nimeishiwa nguvu na sasa naona nikijiusisha sana na siasa za nyumbani unaweza kupata matatizo ya akili .
 
Wanabodi nimesoma hii habari kuhusu mpango wa serikali kuwakopesha wanafunzi waliopata division one kwa wanaume na division one na two kwa wasichana tuu ! Mimi bado aiingii akilini kabisa inawezekana vipi kwa mtanzania wa kawaida kuweza kumsomesha mtoto wake pale chuo ?

Hivi ni taifa gani hawa viongozi wanategemea kulijenga? Hivi hawa viongozi hatambui ya kuwa kima cha chini cha mshahara ni shs 60,0000?



Tutashauri serikali itoe mikopo kwa wote’

2006-08-16 08:35:15
Na Haji Mbaruku

Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo kwa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, Bw. Nimrod Mkono, amesema bodi yake inaendelea kuishauri serikali ili iweze kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaoihitaji.

Bw. Mkono ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, alisisitiza kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete, wakati akizindua shule mpya ya kisasa huko Musoma wiki iliyopita, kuwa serikali haina fedha za kusomesha wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu.

”Serikali imesema kuwa haina fedha, tunaendelea kutafakari suala hili kwa vile linajadilika,” alisema.

Alikuwa akiongea na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kuhusiana na malalamiko ya wanafunzi kuhusu utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Hivi karibuni Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, wakati ikiwasilisha makadirio na matumizi ya bajeti yake bungeni, ilisema kuwa mikopo ilitolewa kimakosa, hivyo kuanzia sasa, watakaopewa mikopo ni wale watakaofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kwa wanaume na kiwango cha daraja la kwanza na la pili kwa wanawake.

Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na BBC walipinga kauli hiyo ya serikali, wakisema kuwa kusomesha wanafunzi kwa misingi hiyo, kutaua maendeleo ya elimu nchini.

Pia, wanafunzi wanadai kuwa kutoa mikopo kwa vigezo hivyo kunaweza kuleta ubaguzi na kwamba Taifa litashindwa kuwapata madaktari, wanasheria, wakandarasi, wahandisi na watafiti wa kutosha.

Mmoja wa wanafunzi wanaosoma mchepuo wa Sayansi katika shule moja ya sekondari, Said Jumanne, alisema kuwa mara nyingi wanafunzi wa masomo ya Sayansi, hufaulu kwa kiwango cha daraja la pili na kuendelea, hivyo wengi wao watashindwa kupata mikopo kwa vigezo vya serikali.

”Kwa sababu wanafunzi wengi sasa watakimbilia kwenye masomo ya Sanaa, ambako wanaweza kupata daraja la kwanza na wanafunzi wa masomo ya sanaa hawawezi kusomea udaktari hata kidogo,” alisema mwanafunzi huyo.

Aliiomba serikali ifikirie upya suala la utoaji wa mikopo.
Ale2roga ni mwenge wa uhuru kwani kimsingi kaziyake mini?
 
Back
Top Bottom