Watanzania na Ubunge wa EAC

victor11

Member
Feb 24, 2011
67
7
Ndugu wana JF,

Jana katika harakati za kampeni za uwakilishi wa Tanzania katika bunge la EAC, Mh. Mwakyembe alitoa hoja nzito sana bungeni, Nazani ni wakati mwafaka sasa kwa walio wahi kuwa wabunge EAC kutoka Tanzania kujitathimini. Ni muhimu sasa wakatuthibitishia aliyoyasema Mh. Mwakyembe kama ni ukweli au uongo kuwa huwa wanafunga midomo na kuingia chini ya meza na kuwaachia Wakenya na wengineo wakitamba.
Pia itasaidia wabunge wapya kujifunza na kujipanga kwa ajili ya uwakilishi uliotukuka na wa uwajibikaji katika bunge lijalo.


Hongera wote mliochanguliwa, Watanzania tunawatengemea.
 
Back
Top Bottom