Mkuu wangu hata kwa kujumuisha Muhindi, mwarabu na mzungu huo sio UBAGUZI ila zote hizi ni karama za mwenyezi Mungu ktk kutuwezesha sisi kutambuana toka ktk tafauti hizi..Hatukuumbwa kwa tofauti zetu isipokuwa kwa sababu ya kutuwezesha sisi kutambuana, kutofautisha baina ya Zomba na Mkandara, Zomba huyu na Zomba Mwarabu, mhindi au mzungu mana leo tuko billioni ngapi?. Kama sisi sote tungekuwa sura moja, rangi moja kama Wachina nani angeweza kukutofautisha Zomba wangu na Mkandara?.Cha kushangaza ni pale kila unapozunguka mbuyu unarudi kuainisha kuwa tuna Ubaguzi wa Ujinga. Kwanini iwe Mwaarabu au Mzungu au Mhindi? au yeyote yule? kwanini isiwe Mwaafrika? iwe kwa jina lolote liwalo, kama ni kigezo tu cha kujuwana kuwa huyu ni Zomba yule ni Mkandara. Kwanini iwe hivyo?
Kwanini siwasikii wasomi waliosomeshwa hizo shule za kujazwa ujinga zikifundisha kuwa Mwaafrika (au jina lolote alilokuwa nalo kabla ya kupachikwa huo Uafriti) ndio alikuwa mtawala wa mwanzo huko bara la Asia? kama ni hivyo, ni wapi niliposoma mimi kuwa Mwaafrika aliitawala Asia? or is it Arabia? siamini kama kulikuwa kuna nchi inaitwa au inajiita Arabia kabla ya mwaka 1932. Jee, wewe hujui kuwa kuna Mwaafrika alitawala Asia kabla ya Waalimu wako kukufundisha kuwa Waarabu na Wazungu walikutawala? Jee, hao Waalimu wako walipokufundisha ujio wa Vasco Da Gama walikufundisha walikuta utawala upi pale Kilwa na Sofala? Jee, kuna uhusiano wowote na Utawala wa Kiafrika uliotawala mpaka Asia?
Raptha iko wapi?
Jiulize kisha ujaribu kueleza Ubaguzi wa Ujinga. Umeugusia mwisho mwisho wa makala yako, Jee, hiyo ndio elimu tuliyopewa? ya kujazwa ujinga? hatukufundushwa nidhamu? nataka kuamini hivyo ndivyo ilivyo lakini sikubali kuwa ni ujinga wa kuwa ni wajinga naamini ni Ubaguzi wa Ujinga.
Pili, Swala Africa sielewi wewe umelipata wapi lakini nijuavyo miye majina hata ya nchi hatakuanza juzi bali karne na karne wala sii kutoka sehemu moja. Mkuu wangu hakuna watu walostaarabika na kuwa kutangulia ELIMU kama Wamisri. Historia zote za Biblia na Quran zinatuonyesha ustaarabu wa Wamisri toka karne na karne.. na pengine wao ndio watu wa kwanza kujua kuandika.Na kwa lugha yao neno MOTHERLAND linatamkwa AFRI-UKA, hiki sii kiarabu bali Kimisri, na ndio asili na jina la bara letu, kama unabisha google. Na unaweza kurudi nyuma zaid hata ktk hadith za mitume utamkuta malikia Sheba alokwenda Uyahudi na kuolewa na Suleiman alijulikana kama Queen of Ophiria hiyo tunazungumzia mwaka 950 BC.. Sasa haya ya AFRIT hata sielewi yametokana wapi ikiwa hao waarabu (badui) wenyewe Ustaarabu wameletewa na Mtume..
Hakuna watu walokuwa nyuma na washenzi kama waarabu na sijui kama unaelewa kwa nini waliitwa Badui, na hata mtume kuteremshwa kwao Mwenyezi Mungu alikuwa na sababu kubwa sana maana ktk watu waloshushiwa mitume wao na Wayahudi ni kama vile walokuwa wamelaaniwa, tazama Sodoma na Gomola, hawa watu waliwatongoza hata malaika,sasa leo huwezi nambia huu ni ubaguzi ilihali hulka zao ndizo zilowatambulisha wao kuwa walivyo.
Halafu haya maswala ya Sofala na Kilwa sielewi yanahusu nini? hawa wote kina Vasco dagama, Speke, Livingston, Carl Steve na Masultan wote walikuwa explorer walokuwa wakisaka utajiri kutokana na historia ama hadithi za vitabu..Walikuja Afrika wakitaka kutafuta machimbo ya mfalme Suleiman na hivyo haituhusu sisi wanapoweka majina ya miji yetu ama ramani kwa sababu hayo majina ilikuwa ni ktk kumsaidia yeye kuzitambua nchi zetu kwa mipaka na ramani yake ili kesho akija mtu mwingine atajua pa kafika wapi na anaelekea wapi..
Mkuu wangu si unaelewa wazi ya kwamba Chrstopher Columbus alipofika ghuba ya Marekani, yeye katika fikra zake alifikiri amefika India? na akaiita nchi hiyo Amerika wakati yuko upande mwingine kabisaa wadunia. Hivyo yasikupe homa wewe haya majina swala kubwa ni wewe unajitambua vipi na uko wapi. Hivyo ikiwa wewe mwenyewe hujitambui upo wapi, umetoka wapi na unakwenda wapi, then You got a problem! lakini haya wanayotusema ama kutuita majina hayana maana yoyote na tuyapuuze...
Nachosema tu ni kwamba sisi tumepewa elimu ili tuendelee kuwa wajinga, na ndio maana tunarudi sana kutaka kujua Historia ya kina Vasco dagama kiuhusu Kilwa na Sofala badala ya kujifunza kuhusu nchi iloitwa Azania kiina Abushir, Mkwawa, Mirambo na wafalme wetu ambao leo walitakiwa kuwa sehemu ya makumbusho yetu badala ya wapanda milima ya Kilimanjaro..I mean sikuelewi na nitaendelea kuuliza haswa nini lengo la mada hii ikiwa sisi wote wajinga na wenye ubaguzi wa kijinga kutokana na Ujinga tulokuwa nao kama haitakuwa muendelezo wa Ujinga ule ule.