Watanzania na chuki dhidi ya viongozi wao

gollocko

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
2,945
2,275
Katika kipindi cha dakika 45 cha ITV jana nilimsikia mh. Job Ndugai (Naibu spika) akisema kuwa watanzania tuna tabia ya kuwachagua viongozi wetu leo halafu kesho yake tunaanza kuwachukia! Je hii ni kweli? Na iweje leo tuwapigie kampeni na mara waingiapo madarakani tuwachukie, hii imekaaje wanajamvi?

R.I.P Regia Mtema(Jembe la uhahika!)
 
wapiga kura wanadanganyika wakati wa kampeni na vijihela kofia,khanga,wakishachagua wanagundua walichagua mabogus wanaanza hatred
 
sio sisi tunawachukia viongozi wetu, Ni wao wakishachaguliwa wanaacha kuwa viongozi wanageuka watawala na watafutaji, na wakwapuaji wa kutisha. Tutawapendaje watu wasiotutakia mema
 
we nadhani kwa wale watakokuwa wamemuona naibu speaker ni wazi watamchukia kuanzia hiyo jana.
Mtu anajiita mwakilishi wa wananchi lakini wakimuuliza basi twambie unalolijua analeteta unafiki wake. Ni wazi kuwa alivyokuwa anaomba kura aliwahahidi wananchi wake kuwaeleza ukweli na kwa vile hajafanya hivyo hakuna jingine zaidi ya kumchukia!
Katika kipindi cha dakika 45 cha ITV jana nilimsikia mh. Job Ndugai (Naibu spika) akisema kuwa watanzania tuna tabia ya kuwachagua viongozi wetu leo halafu kesho yake tunaanza kuwachukia! Je hii ni kweli? Na iweje leo tuwapigie kampeni na mara waingiapo madarakani tuwachukie, hii imekaaje wanajamvi?

R.I.P Regia Mtema(Jembe la uhahika!)
 
tatizo sio kuchukiwa na wananchi viongozi wetu anapenda mno sifa za kijinga, wakiambiwa ukweli kuwa hawawezi wanakuwa wakali
 
rais alichaguliwa na watanzania milioni 5 kati ya milioni 45 hapo utasema ni watz au kabila lako?
hata akichukiwa si waliomchagua bali ni wale milioni 40 ambao hawakumchagua.
 
Wivu tu ndo unawasumbua.

Mtazame Kiongozi Mkuu - kwa kweli wivu unatutsumbua!

ru76er.jpg

Duh !
 
Kwahiyo wanataka kupendwa hata kama hawawafanyii wananchi yale wanayotakiwa/waliyoahidi kufanya?

Kupenda mtu kunaendana na kuridhika nae, in this case kuridhika na utendaji wake. Kama utendaji wake umedorora kila anaeathiriwa na hilo lazima amchukie mtendaji.
 
This is very true. Ukiona kiongozi yoyote anadai kupendwa, anapenda publicity kwenye vyombo vya habari ambayo haimstahili, ujue kuna walakini mkubwa, kwenye uongozi wake. Viongozi wa namna hii wanafanya kila hila ili wabaki madarakani kwa mbinu za ujanja ujanja, na muda wao ukiisha wanahakikisha wanaacha vibaraka wao.

Just do your job and let people judge you.
 
rais alichaguliwa na watanzania milioni 5 kati ya milioni 45 hapo utasema ni watz au kabila lako?
hata akichukiwa si waliomchagua bali ni wale milioni 40 ambao hawakumchagua.
Hizi data umezipatia kijiwe gani mzee. Maana naona siku hizi kura za urais zinahesabiwa kwenye vijiwe vya msuba.
 
Katika kipindi cha dakika 45 cha ITV jana nilimsikia mh. Job Ndugai (Naibu spika) akisema kuwa watanzania tuna tabia ya kuwachagua viongozi wetu leo halafu kesho yake tunaanza kuwachukia! Je hii ni kweli? Na iweje leo tuwapigie kampeni na mara waingiapo madarakani tuwachukie, hii imekaaje wanajamvi?

R.I.P Regia Mtema(Jembe la uhahika!)

kama malengo yao hayajatimizwa lazima wamchukie. viongozi wanatoa ahadi za maisha bora, badala ya kuwa maisha bora yanageuka kuwa bora maisha na ufisadi juu, kwanini hawa viongozi wasichukiwe.
 
99% Hawaonekani kwenye majimbo yao hadi siku ya kampeni. Viongozi wanaojichanganya na wananchi wa kawaida ni wachache sana.
Chuki inatokana na kuuziwa mbuzi ndani ya gunia.

RIP Regia Mtema.
 
Viongozi wengi cyo wakweli. Hawapendi kuwaambia hali halisi wananchi pindi wanapotafuta kura.Wanaahidi vitu ambavyo viko juu ya uwezo wao kiutekelezaji ndiyo maana wanaposhindwa kutekeleza wananchi hawawaelewi na matokeo yake ni kuwachukia.Kwa hiyo asitafute sympathy kwenye vyombo vya habari wananchi wenyewe watahukumu juu ya ahadi za uongo na utekelezaji wake.
 
Back
Top Bottom