Watanzania msiipigie kura CHADEMA 2015

Unaumwa sana wewe..yaani hii thread hata mke wako kaiona? Kama ndivyo nadhani ni mvumilivu sana kuishi na mtu mwenye matatizo ya ubongo yanayojionyesha kwa wazi kabisa.
 
Kwa Afrika ni nadra upinzani kuleta maendeleo. Mfano halisi angalia Kenya ambapo hao raia waliouweka upinzani madarakani uliwasbabishia matatizo makubwa na hatimaye umefikia hatua ya kuwafukuza wafanya kazi wa sekta ya afya. Hii haikubaliki, mfano tizama jinsi chama cha mapinduzi kinavyo fanya mambo kwa kufuata sheria na ni chama kivumilivu. Nasaha zangu, watanzania msibabaishwe na vyama vya upinzani. Tujenge nchi na CCM!!

Kwanza angalia avatar yako. Unamaanisha nini na hiyo avatar yako? Mbona umeipenda mpaka umeitumia. Mabadiliko yanahitajika ili kuweka mambo sawa.
 
Humu JF watu wengine wanatakiwa wakatibiwe. Mtoa hoja ana tatizo la njaa na anatumwa abwabwaje ili jioni apate sahani la pilau na maji ya kunywa. Kama anafuatilia mada za ukombozi duniani kote swala sio ukongwe kwani hata dola ya kirumi ilikuwa kongwe na kuangushwa kwa kutokujali watu wake. Mifano iko mingi tu: mfalme wa Ufaransa na hii ya karibuni katika bara la Afrika. Tena ukongwe ndio unawafanya watawala wajisahau na ndiyo sababu tosha ya kuwaondoa ili wananchi wapate huduma siyo maneno. Wengi wa magamba wanaiogopa CDM kama ukoma kila wakiamka, wakilala hawapati picha. Mtoa mada aende Arumeru akaongelee ***** wake ajue watu wamebadilika na mwendo ni mdundo hadi hapo watu watakapopata fursa ya kufaidi raslimali lukuki za Tanzania. Hofu ya mabadiuliko kwa magamba ni kuwa ukombozi ukija watatakiwa kujibu mashtaka na kurudisha mali walizopora. Mfano wa karibuni na jirani zetu Zambia. Wakamwulize Banda moto anaopata na jamaa zake kwa Cobra Michael Sata. Linakuja na mnalo!
 
uko sawa kabisa ccm kwa ukongwe wake kinatakiwa kuwapitisha wakonge ili wagombee kwa sababu kwa akili yako ukongwe ndiyo dawa.

ccm impitishe kingunge ngombale mwiru kuwa mgombea urais,waziri mkuu awe peter kisumo.

mawaziri wastaafu wote jumuiya ya afrika mashariki kwa sababu hawa machekbob walioishika ccm na upinzani hawafai.

Siipendi CCM, Lakini jamaa amesema kweli. Vyama vya upinzani hapa TZ bado sana kupewa nchi. Bado sanaa.
 
Inawezekana kabisa ukawa na sababu nzuri na muhimu. Kisayansi huwezikuthibitisha jambo/hoja kwa kutumia
mfano mmoja tu kama unavyofanya.
Africa ni moja lakini kuna mataifa mengi, makabila mengi hulka tofauti. Kila nchi ina historia tofauti na mapito tofauti
yaliyoifikisha hapo ilipo. " we first make our habits and then habits make us" Kila jambo lina chanzo. Watakao unga mkono
hoja wanasababu hata hao watakao ipinga wanasababu. Tuje na sababu zishindanishwe. Naomba kuwasilisha.
 
Kwa Afrika ni nadra upinzani kuleta maendeleo. Mfano halisi angalia Kenya ambapo hao raia waliouweka upinzani madarakani uliwasbabishia matatizo makubwa na hatimaye umefikia hatua ya kuwafukuza wafanya kazi wa sekta ya afya. Hii haikubaliki, mfano tizama jinsi chama cha mapinduzi kinavyo fanya mambo kwa kufuata sheria na ni chama kivumilivu. Nasaha zangu, watanzania msibabaishwe na vyama vya upinzani. Tujenge nchi na CCM!!


Kumbe kweli jamaa wewe ni mtanzania? Nakumbuka miezi kadhaa iliyopita ulisema wewe ni mkenya na tena ulikuwa unatuomba kuja kuishi tanzania. Unakumbuka miongoni mwa watu waliokutilia mashaka ngosha? Unakumbuka ulisema hujui hata tafsiri ya ID yako?

Huu si uwendawazimu? Binafsi sina tatizo na ushauri wako, ila nina tatizo na mshauri mwenyewe. Huwezi ukajifanya wewe sio mtanzania(sijui kwa nini) halafu leo hii utushauri nini cha kufanya kuhusu tanzania yetu. Wewe mbona unaionea aibu?
Hebu rudi ukajipange upya bwana mdogo.
 
kuiweka ccm mpaka 2015 ni maafa,nina uhakika haitafika 2015 ikiwa madarakani!umeona jk ameogopa kuongea leo?
 
wakati wa uchaguzi huwa hakuna chama caha upinzania au chama tawala vyote vinakuwa vyama shindani,nakushauri urekebishe hoja yako hii,chama kikishawekwa madarakani kinaisha kuwa chama pinzani,ccm ni kweli inajenga nchi lakini siyo nchi ambayo tunaitaka watanzania.Mwenyezi Mungu Akusamehe kwasababu unashindwa kuitumia akili njema aliyokupa,hapa tulipofika hatujiulizi kama ccm itakufa au haitakufa ni wazi kwamba chama cha mapinduzi kinajifia swali ni lini?(jibu unalifahamu baki nalo)
 
Wewe bado unashabikia CCM Dunia hii,hujui kuwa matatizo yote ya migomo nchini chanzo ni CCM mikataba mibovu ya RICHMOND,KAGODA,MLEMETA,BOT by DAVID BALALI,badala ya kuungana na makanda ili kutokomeza UFISADI unapotosha husitahili kuigwa na jamii ya leo.
 
huna uwezo wa kufikiria zaidi na CCM. ni sawa na kipofu aliyebahatika kuona siku moja kila mfano ata refer hicho alichoona.

HUNA MAWAZO ZAIDI YA CCM bora hata Nyerere aliliona hilo na kushauri mfano wa vyama vingi kuliko wewe KIDUKU uliyegota.
 
Binafsi na wasiwasi na upeo wako wa kufikiri, huwa ni kwa mujibu wa utafiti au fikra zako za kimagamba? Kama ni utafifti take reference to Ghana wanakuza uchumi wao kwa kutumia raslimali zao za ndani huyo ni John A> Mills, Zambia wanaanza vizuri. Kuhusu Kenya yawezekana hufahamu vizuri KANU ndiyo CCM au TANU ya Tanzania leo kiko wapi??????
Tuletee hoja za msingi na si uporojo wako hapa au rudi class yawezekana tunajibu hoja za kikayumba primary schools.
 
Mtoboasiri, sikiliza! Ukilinganisha upiznani wa hizo nchi ni stable, hwezi kulinganisha na upinzani wa TZ ambao wamejaa njaa (mfano David Kafulila alikuwa na haja gani ya kupiga magoti na kulia ili asamehewe?) na CHADEMA ni chama kilicho jaa migogoro ya hapa na pale, labda kikiundwa chama kingine chenye mlengo na dhamira ya dhati ya kusikiliza matatizo ya watanzania walio wengi na kisiwe na migogoro

Ng'wanachu wewe ni punda! Labda CDM walikuwa na mgogoro na mkeo!
 
Ule ugonvi wako na CDM bado haujesha?
Mbona hizi campaign umezianza mapema?
Umeona eeh CDM ni chaguo la wengi 2015?

Mafisadi wanahangaika hadi wewe wanakutumia?

Kazi kwelikweli!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom