Watanzania milioni moja – One –MT project ni sawa na NICOL?

I suggest you read through the relevant thread post by post while paying close attention to what one "Matiksa" wrote. It is my belief that this individual together with "zeenam" and the thread starter (among others) colluded with each other in a joint effort to introduce "reasonable doubt" in the court of public opinion against Mr. Chenge.

One "Matiksa" and "zeenam" could be one and the same! Your belief of their collusion shows incredible naivety for a man (woman) of your age for anyone can sign up in this forum with multiple names without verifying their true ID. Therefore I don't see any "reasonable doubt" whatsoever, not even a shred of it.
 
Mama,

Tatizo letu bado linarudi kwenye kutaka mambo kwa urahisi, kuacha kufuatilia na kusubiri wengine wafanye kazi.

Kwenye hiyo issue ya UMOJA na hata NICO, ni watu wangapi walisoma proxy na addendum ambazo zilijenga hizo FUND?

Je ni wangapi wanajua haki zao kwa kusoma articles za incoporation na makbrasha mengine kuhusu kuundwa kwa Funds hizi, uongozi wake, maamuzi yake, mgawanyo wa mapato na mambo mengine ya kisheria ili mtu alinde mtaji na investment yake?

Sasa kama mtu alikimbilia kuchangia mfuko kwa kuwa alisikia kuwa atajipatia hela marudufu katika miaka miwili lakini hakusoma vile vipengele vya kisheria kuhusu wajibu wake na haki yake kwa dhati, basi tunabakia kuwa wadandiadi miradi, mithili ya Upatu kwa kuwa tumeweka mbele TAMAA ya kupata pesa na si kujifunza kwanza ni wapi tunaweka pesa zetu na zitatuzalishia nini na kwa muda gani na manufaa yake ni nini!

Kila kitu na mradi una mipango, sheria au mkataba. je ni kazi gani ngumu kupitia mkataba na mipango kabla hujamwaga fedha zako ndani ya kisahani cha SADAKA?

Watanzania wachache sana wanasoma terms and conditions, na ndicho ninachosababisha hata tunaingia mikataba ya kutumaliza. Ikiwa mawaziri na wanasheria wetu hawajui kusoma between the lines kwenye mikataba, leave alone the negotiation capacity yao, je mwananchi wa kawaida?

Lakini umefika wakati wa kuhoji yale mamilioni yaliyokusanya na umoja fund yamefanya nini? Ni kwa nia njema kabisa ili tujue pros and cons hata mradi mwingine ukitaka kuanzishwa basi iwe rahisi kujiweka sawa.
 
Suala ni kuwa hawajui/hatujui kusoma au hawataki/hatutaki kusoma terms na conditions za kila kitu wanachotia/tunachotia sahihi?

I have no problem kwenda kuhoji UMOJA na NICO kujua mambo niaje, lakini nikifuata thinking ya Nyambala, na kuona reaction ya watu, napata hofu kama iko siku tunaweza kujiinua kwa nguvu za utashi wetu wenyewe na kuanza kupaa kiuchumi na kimaendeleo.
 
One "Matiksa" and "zeenam" could be one and the same! Your belief of their collusion shows incredible naivety for a man (woman) of your age for anyone can sign up in this forum with multiple names without verifying their true ID. Therefore I don't see any "reasonable doubt" whatsoever, not even a shred of it.

It is my understanding that you are a grown up girl (boy). That said, its your prerogative to believe in whatever you happen to be comfortable with as far as your convictions are concerned. The Member list shows that the two individuals you've mentioned have only been interested in contributing to Chenge related threads and shown themselves to be die-hard vocal supporters of Chenge.

Otherwise I ask you not to intentionally misquote and distort what I wrote previously, as when you provide the following baffling statement:
I don't see any "reasonable doubt" whatsoever, not even a shred of it.
 
Watanzania milioni moja – One –MT project

Nimekaa nikifikiria kuhusu ujasiriamali nikajikuta naona mradi madhubuti ambao kama kweli, kwa nia moja na thabiti isiyo na chembe ya ufisadi inaweza kubadili kabisa mustakabali wan nchi yetu.

Watanzania milioni moja katika mradi huu kila mmoja anatakiwa kutoa US $ 1000, that sums up to US$ 1,000,000,000. Nikiwa kama mhandisi miradi niliyesimamia miradi mingi na yenye thamani mpaka kufikia US $ 400,000,00 ntajaribu kuiweka hoja yangu katika mtizamo huo.

Ieleweke kwamba tangu nchi yetu ipate uhuru hakuna mradi hata mmoja uliowahi kujengwa kwa gharama ya one billion US dollars na si hapa tu hata katika nchi zote za Africa miradi hiyo inahesabika. Hivyo basi that is a huge amount of money!!!!!!! Kumbe watanzania milioni moja……

1.Tunaweza kujenga barabara ya lami ya kisasa kabisa kutoka Dar mpaka Mwanza.

2.Tunaweza kimiliki Liganga – Mchuchuma kwa asilimia 100.
3.Tunaweza kujenga shule za kisasa kabisa say kwa US $500,000 each elfu mbili.
4.Tunaweza kujenga hospitali bora na za kisasa kabisa say kwa US $1, 000,000 each elfu moja.
5.Tunaweza kujenga bomba la maji kutoka Mwanza mpaka Dodoma na mikoa ya jirani
6.Tunaweza kujenga reli kutoka mtwara mpaka makambako.
7.Tunaweza kujenga PP’F towers 200
8.Tunaweza kujenga bandari zote tatu kubwa – sea ports (Dar, Tanga, Mtwara)
9.Tunaweza kumiliki mabasi yoote Tanzania.
10.Tunaweza kujenga mijengo ya Balali kwa bei halali kama mitano hivi.
11.Tunaweza kumiliki migodi yote iliyopo Tanzania kwa sasa
12.Tunaweza kujenga gas - power station Kubwa kuliko zote in East ,Central and Western Africa.
13.Tunaweza kuweka lami barabara zote za jiji la Dar.
14.Tunaweza kujenga viwanja vya michezo mithili ya ule wa mpya wa taifa kila moka
15.Tunaweza kuwa na capital kuliko fisadi yeyote hapa nchini.
16.Tunaweza kutoa ajira hizo milioni zilizo ahidiwa na JK.
17.Tunaweza kuunganisha mikoa yoote ya pembezoni mwa TZ kwa lami.
18.Tutakuwa tuna hela nyingi kuliko hata zile alizotoa Joji kichaka.
19.Tunaweza pia kununua Man U, Arsenal na Chelsea.
20.Tunaweza kufanya mengi tuuuuuuuu Kubwa zaidi hata yale Ambayo serikali imeshindwa kabisa kuyafanya toka tupate uhuru.

Truth: Watanzania milioni moja wanaoipenda nchi yao wanaweza kuiboresha nchi yao kwa mengi.

Challenge: Inawezekana kweli kukusanya watu milioni moja kuwauzia hii hoja ikakubalika na kutekelezeka?Who Hill manage this Project? Sounds not really uhhhh!!!!!

Ok let’s work it out this way- Katika watanzania milioni moja, nusu yake yaani laki tano wawe ni govt fund. The remaining laki tano gawa kwa kumi = 50,000. Hivi haiwezekani kupata watanzania 50,000 wenye $10,000 kila mmoja tukatekeleza hii One –MT project (One million Tanzanians project).

Nakaribisha mawazo na njia mbadala, we can work thru One –MT project. Ninaamini tunaweza kufanya makubwa yasiyotarajika. Kama sikosei akina Mosha na ile NICO ni the same idea!!!!!!! Well but this is One –MT project.

Nawakilisha.

Ku-spice majadiliano nitapingana na wewe. Kwanza tuanze na historical facts. Unaposema kuwa Tanzania haijawahi kuwa na mradi wa bilioni moja za kimarekani hiyo ni kweli kabisa.

Lakini ukichukulia billioni moja kwa thamani ya sasa na kama sio namba billioni moja, kuna uwezekano mkubwa ipo miradi iliyofika billioni moja.

Mradi wa TAZARA ulikuwa ni millioni 500 USD miaka ya 70. Na thamani yake kwa sasa inaweza kuzidi billioni moja USD.

Mradi wa ujenzi wa makao makuu Dodoma hauna hesabu za kueleweka lakini ukichukua time frame, kazi zilizofanywa za kujitolea na michango ya wananchi umezidi billioni moja USD.

Tukirudi kwenye mada. Analysis yako ni nzuri lakini kuna uwalakini mkubwa. Analysis nzima ime-base kwenye perception kwamba vitu hivyo vinawezekana. Lakini ukichukua kalamu na kufanya analysis ya watanzania wanaoweza kukupatia hizo 1000 USD na jinsi watakavyochangia hizo pesa, unaweza kuwa nyuma sana na matarajio yako. Na ukiangalia kwa undani sana, fikra zako hazina tofauti na yule aliyefikiria kuwa akiwaweka watu katika vijiji vya ujamaa watatoa mchango mkubwa wa kijiendeleza wenyewe na matokeo yake hakuna kilichofanyika.

Wapo zaidi ya watanzania 1,000,000 wanaotengeneza zaidi ya dollar 1,000 kwa mwezi au kwa mwaka. Lakini hizo pesa ni hizo hizo wanazotumia kuendesha familia zao na sio pesa za ziada au zilizopo katika akaunti ya akiba ambazo ungeweza kuzitumia kwenye miradi uliyotaja.

Umesema umeshawahi kusimamia miradi ya US $ 400,000,00 (I guess US $ 400,000,000). Ni uhakika kati ya miradi hiyo, ipo miradi iliyoendesha kwa mikopo kutoka benki. Kwa mtaji huu ningekuomba uachane na watanzania millioni moja na utueleze kama ungepewa mkopo wa dollar billioni moja ungeweza vipi ku-implement moja ya miradi uliyotaja na kuweza kuliletea taifa faida na kulipa mkopo?

Vilevile miradi mingi inakuwa underestimated na inapomalizika gharama zinakuwa kubwa kuliko kiwango cha mwanzo. Kwa mfano, Euro Tunnel kuunganisha UK na Ufaransa ulikuwa ni mradi wenye makadirio ya Paundi chini ya 5 Billioni. Na ulipomalizika ulitumia Paundi Billioni 10. Na kwa sasa hivi faida inayopatikana katika mradi huu haiwezi kulipa interest ya deni la mradi huu.

Kwa mfano wa Euro Tunnel. Ikitokea kwamba umechukua pesa za watanzania millioni 1, lakini katika ya maendeleo ya mradi au pale mradi unapomalizika inaoneka kuwa pesa zilizotumika ni mara mbili au tatu kuliko makadirio yako ya mwanzo ni njia gani utatumia kuondoa matatizo yatayojitokeza kama vile madeni?
 
It is my understanding that you are a grown up girl (boy). That said, its your prerogative to believe in whatever you happen to be comfortable with as far as your convictions are concerned. The Member list shows that the two individuals you've mentioned have only been interested in contributing to Chenge related threads and shown themselves to be die-hard vocal supporters of Chenge.

Otherwise I ask you not to intentionally misquote and distort what I wrote previously, as when you provide the following baffling statement:

I am a grown ass man.

And two individuals don't qualify as a whole bunch of Wasukuma. Get it Njabu?
 
Mama,

Suala ni kuwa hawajui/hatujui kusoma au hawataki/hatutaki kusoma terms na conditions za kila kitu wanachotia/tunachotia sahihi?

I have no problem kwenda kuhoji UMOJA na NICO kujua mambo niaje, lakini nikifuata thinking ya Nyambala, na kuona reaction ya watu, napata hofu kama iko siku tunaweza kujiinua kwa nguvu za utashi wetu wenyewe na kuanza kupaa kiuchumi na kimaendeleo.

Nadhani watu wameshakuwa na hofu kwani watu huwa wanatoroka hata na michango waliyochangiwa kwa ajili ya harusi na misiba! Kwenye vyama vya kuweka na kukopa ndio ufisadi uko mwake......Baadhi ya watanzania wametokea kuwa wabinafsi kupindukia, kila mtu anafikiria kwanza yeye kama yeye atanufaika vipi?

Mfano, tulichanga michango ya kutengeneza barabara ya kiwango cha lami na mitaro mtaani kwetu, badala ya kuweka lami ikawa moram tu kwa vile mweka hazina, mwenyekiti na katiu walijikatia cha juu bila kujali tulishafanya bajeti na kuwa tulichanga kila mwezi kwa muda wa miaka mitatu hivi. Kamati ikiwauliza ni maneno mengi tuuu hakuna cha maana.
 
Ku-spice majadiliano nitapingana na wewe. Kwanza tuanze na historical facts. Unaposema kuwa Tanzania haijawahi kuwa na mradi wa bilioni moja za kimarekani hiyo ni kweli kabisa.

Lakini ukichukulia billioni moja kwa thamani ya sasa na kama sio namba billioni moja, kuna uwezekano mkubwa ipo miradi iliyofika billioni moja.

Mradi wa TAZARA ulikuwa ni millioni 500 USD miaka ya 70. Na thamani yake kwa sasa inaweza kuzidi billioni moja USD.

Mradi wa ujenzi wa makao makuu Dodoma hauna hesabu za kueleweka lakini ukichukua time frame, kazi zilizofanywa za kujitolea na michango ya wananchi umezidi billioni moja USD.

Tukirudi kwenye mada. Analysis yako ni nzuri lakini kuna uwalakini mkubwa. Analysis nzima ime-base kwenye perception kwamba vitu hivyo vinawezekana. Lakini ukichukua kalamu na kufanya analysis ya watanzania wanaoweza kukupatia hizo 1000 USD na jinsi watakavyochangia hizo pesa, unaweza kuwa nyuma sana na matarajio yako. Na ukiangalia kwa undani sana, fikra zako hazina tofauti na yule aliyefikiria kuwa akiwaweka watu katika vijiji vya ujamaa watatoa mchango mkubwa wa kijiendeleza wenyewe na matokeo yake hakuna kilichofanyika.

Wapo zaidi ya watanzania 1,000,000 wanaotengeneza zaidi ya dollar 1,000 kwa mwezi au kwa mwaka. Lakini hizo pesa ni hizo hizo wanazotumia kuendesha familia zao na sio pesa za ziada au zilizopo katika akaunti ya akiba ambazo ungeweza kuzitumia kwenye miradi uliyotaja.

Umesema umeshawahi kusimamia miradi ya US $ 400,000,00 (I guess US $ 400,000,000). Ni uhakika kati ya miradi hiyo, ipo miradi iliyoendesha kwa mikopo kutoka benki. Kwa mtaji huu ningekuomba uachane na watanzania millioni moja na utueleze kama ungepewa mkopo wa dollar billioni moja ungeweza vipi ku-implement moja ya miradi uliyotaja na kuweza kuliletea taifa faida na kulipa mkopo?

Vilevile miradi mingi inakuwa underestimated na inapomalizika gharama zinakuwa kubwa kuliko kiwango cha mwanzo. Kwa mfano, Euro Tunnel kuunganisha UK na Ufaransa ulikuwa ni mradi wenye makadirio ya Paundi chini ya 5 Billioni. Na ulipomalizika ulitumia Paundi Billioni 10. Na kwa sasa hivi faida inayopatikana katika mradi huu haiwezi kulipa interest ya deni la mradi huu.

Kwa mfano wa Euro Tunnel. Ikitokea kwamba umechukua pesa za watanzania millioni 1, lakini katika ya maendeleo ya mradi au pale mradi unapomalizika inaoneka kuwa pesa zilizotumika ni mara mbili au tatu kuliko makadirio yako ya mwanzo ni njia gani utatumia kuondoa matatizo yatayojitokeza kama vile madeni?

Bin Maryam,

Now this is much better as far as constructive criticism, goes.

Nyambala katoa Fikra, Umetoa utaalamu pinganifu, let the game begin.

Your analysis puts us into thinking mode on how to realize this Dream of Nyambala. Huku ndiko kulikuwa kunahitiajika ili kujenga mradi madhubuti na si kuanza kuogopa na kutafuta visingizio kuwa mradi hautafanikiwa.
 
Nadhani watu wameshakuwa na hofu kwani watu huwa wanatoroka hata na michango waliyochangiwa kwa ajili ya harusi na misiba! Kwenye vyama vya kuweka na kukopa ndio ufisadi uko mwake......Baadhi ya watanzania wametokea kuwa wabinafsi kupindukia, kila mtu anafikiria kwanza yeye kama yeye atanufaika vipi?

Mfano, tulichanga michango ya kutengeneza barabara ya kiwango cha lami na mitaro mtaani kwetu, badala ya kuweka lami ikawa moram tu kwa vile mweka hazina, mwenyekiti na katiu walijikatia cha juu bila kujali tulishafanya bajeti na kuwa tulichanga kila mwezi kwa muda wa miaka mitatu hivi. Kamati ikiwauliza ni maneno mengi tuuu hakuna cha maana.

Watanzania tumelea utamaduni mmoja mbaya sana wa kuachia dhuluma na uhalifu uendelee kupeta bila wasiwasi.

Huyo mwenyekiti wa kijiji chenu amefikishwa mahakamani kwa ubadhirifu? kama hajafikishwa mahakamani au kwenye kamati ya kijiji, kuhojiwa, kijiji kinasubiri nini?

Ikiwa tunashindwa wajibu huu kuanzia nyumbani, mtaani, kijijini, je tutaweza kwenye uwanja wa kitaifa?
 
Mama,

Suala ni kuwa hawajui/hatujui kusoma au hawataki/hatutaki kusoma terms na conditions za kila kitu wanachotia/tunachotia sahihi?

I have no problem kwenda kuhoji UMOJA na NICO kujua mambo niaje, lakini nikifuata thinking ya Nyambala, na kuona reaction ya watu, napata hofu kama iko siku tunaweza kujiinua kwa nguvu za utashi wetu wenyewe na kuanza kupaa kiuchumi na kimaendeleo.

Rev. Kishoka,

Hiyo ya watu wote kuwa na uwezo wa kusoma na kuelewa hayo makabrasha ya NICO au UMOJA fund sahau. Hata wenzetu huku nje hawana uwezo huo wa kusoma hayo makabrasha na badala yake wanategemea zaidi corporate governance kuwasaidia kuhakikisha namba wanazoziona au statements wanazoziona zina make sense.

Tatizo kwa TZ ni hao ambao wana elimu na wanatakiwa kuwasaidia mamilioni ya Watanzania kufanya informed decisions ndio hao hao majambazi. Wanaweza kuandika chochote ili kutengeneza faida zao binafsi.

Si umeona akina prof. Ndullu walikuwa kwenye board lakini hata hawakujua watu wanachota mapesa. Hata huko Enron ilikuwa hivyo, watu wa kawaida pamoja na wafanyakazi ambao ni wasomi, bado hawakuona hatari kwamba inakuja.

Kwa Tanzania miradi kama NICO, kuna watu watakuja kulia hasa. Uwajibikaji huko nyumbani ni mdogo mno. Kama watu waliua makampuni ya umma, kweli watashindwa kuua hizi funds?

Ni muhimu mno kuwa na corporate governance rules ambazo zina meno na wanaokiuka kuwajibishwa hasa. Juzi hapo nimesoma gwiji mmoja anaandika positive analysis ya Safaricom ya Kenya na huku hapo hapo anataka kusimamia uuzaji wa share za kampuni hiyo hiyo kwa wananchi. Conflict of interest iko wazi lakini serikali na watu wanaotakiwa kusimamia maslahi ya sisi wananchi, walikaa kimya utafikiri hawaoni.
 
Watanzania milioni moja – One –MT project

Nimekaa nikifikiria kuhusu ujasiriamali nikajikuta naona mradi madhubuti ambao kama kweli, kwa nia moja na thabiti isiyo na chembe ya ufisadi inaweza kubadili kabisa mustakabali wan nchi yetu.
.....
Nakaribisha mawazo na njia mbadala, we can work thru One –MT project. Ninaamini tunaweza kufanya makubwa yasiyotarajika. Kama sikosei akina Mosha na ile NICO ni the same idea!!!!!!! Well but this is One –MT project.

Nawakilisha.

kwanza nakupongeza kwa kutenga muda wako na kufikiria constructively jinsi ya kutatua matatizo ya nchi yetu. baada ya hapo naomba nichangie ifuatavyo:

1. Wazo ni zuri, lakini kama ulivyoona katika uchangiaji wa mawazo hapa JF, unapata aina ya mseto ambao unakupa picha kamili utakayokutana nayo huko field. lakini ni kweli kwamba lazima project yoyote izingatie hali halisi ya nchi yetu. watu hatuna moyo wa kujituma as such. wengi wana historia mbaya juu ya miradi yoyote ya uma au ushirika, na taratibu zetu na kanuni katika uendeshaji wa vitu kama hivi bado ni underdeveloped. Awareness ya watu ni ndogo, hilo limesemwa tayari, hivi kutoa mwanya kwa waroho.

2. sasa katika mazingira kama hayo, napendekeza kwamba tuhamasishe watu wafanye vitu vyao wenyewe katika vikundi, ili wapate uzoefu wa jinsi ya kuwa innovative, kuanzisha mradi, kufanikisha mradi, kufuata sheria na kanuni,kudhibitiana wao kwa wao. watu ambao tayari wana uzoefu katika kazi hizi ni rahisi zaidi kuwashirikisha katika umoja mkubwa zaidi, kuliko kudeal na mtu ambaye hajui a wala b ya umoja. kwa sasa ukianzisha project na watanzania 10, ukipata 3 ambao mnaongea lugha moja kuhusu business yenu, shukuru. wengi utakuta wanaendekeza majungu, hawafuati taratibu za kibiashara, wanaheshimu zaidi ukabila na ushirikina, badala ya business diligence. wanajali zaidi know-who badala ya know-how. kufanya kazi na idadi kubwa ya watu kama hao ni kujitafutia ugonjwa wa moyo kabla ya siku zako, kama uko serious. kama unataka kuwaibia tu, then no problem.

3. Napendekeza mtoa mada aanze kwa kuwa na NGO inayoshauri vikundi hivi, ili apate uzoefu wa down to earth juu ya jinsi Tanzanian Business environment ilivyo. kuna mlolongo mwingi wa sheria na kanuni ambazo zimepitwa na wakati au zinatakiwa mpya ili kuweka mazingira mazuri ya mtanzania kufanya business ikafaulu. Naambiwa kwa mfumo wa kodi wa sasa ni vigumu kutokwepa kodi, bora ulipe hongo ili ukwepe kodi. emphasis kwa muda mrefu imekuwa katika kufanikisha mazingira bora kwa "mwekezaji" wa kutoka nje [na "tumewekezwa" kweli kweli], na sio mtanzania wa kawaida. sasa kujua mazingira haya itasaidia katika kupigia kelele mambo ya kurekebishwa ili kutoa mazingira bora zaidi.

4. tunahitaji vikundi vingi viwe active katika kuadress business environment, ili kutoa transparency na pia kupanua wigo na kuruhusu vichwa mbalimbali vifanyie kazi tatizo moja. si vizuri wote tukaingia kwenye one gigantic MT project kwa kuanzia. hiyo inabidi iwe ni hatua ya mwisho ambapo tayari kuna critical mass ya watanzania wenye hasira ya kutosha na wenye practical understanding ya uendeshaji wa biashara, na wanaojua maana ya appointment, maana ya time, maana ya responsibility, maana ya agreement, contract, n.k.
 
nadhani ushahidi mnao wa kutosha, watingisheni hao mafisadi wa mtaa wenu kwa pilato!! kutokufanya hivyo ni kulea tabia mbaya na ndio mwanzo wa kujirudisha nyuma kimaendeleo.
kwanini 'vijisenti' ulivyovitolea jasho viliwe na mtu mwingine bila sababu? imagine kama mtu mwingine akija na idea ya kujenga youth center yenye after school programs kwa watoto wenu(a good thing), haitafanikiwa kimichango kwasababu ya hii xperince....kwanini iwe hivyo? watoleeni mfano hawa jamaa,ili tabia hii ikome!!.

Tatizo watanzania hatuko tayari kutoa muda wetu kufuatilia litigation measures kama hizi. sababu ziko nyingi. ya kwanza utakuta waliofanya hivyo wanafahamika, ni mjomba wa fulani, ni babu ya fulani, ni baba mkwe wa fulani... basi inakuwa taabu nani aonekane "mbaya wao". ndio maana huko mitaani utakuta kitoto kimebakwa lakini wazee wanajadili na kuamua yaishe.

Sababu nyingine ni mfumo wetu wa sheria ambapo wewe unayetaka haki na yule aliyefanya makosa, wote ni chakula halali katika mfumo mzima tokea polisi wa chini, makarani mahakamani, wazee n.k. bila kutaja gharama nyingi tu za mawakili na kesi kuchukua muda mrefu ikiahirishwa kila leo. Justice delayed...

Sasa hapo mama kahesabu gharama, kaona bora tu mtu una cut losses na kusonga mbele kwa mbele.

ufumbuzi? inabidi tukomae! tusimwangalie nyani usoni, na kama kesi hizi zinapata publicity kubwa, na tukishirikiana, it can be done. kuwaachia hawa jamaa wafanye hayo with impunity, ni kujenga na kuimarisha ugonjwa huu wa ufisadi na rushwa zinazokithiri
 
Nyambala ninakushukuru kwa kuweza kufikiria wazo lako na kulileta hapa kwenye Forum. Ni ukweli usiopingika kuwa wazo lako ni zuri sana na ni changamoto kwetu sisi watanzania ambao tunaipenda na kuitakia mema nchi yetu.

Ili Tanzania iweze kuendelea na kupiga hatua za kimaendeleo haina budi kujengwa na watanzania wenyewe na si kutegemea misaada ya kutoka kwa wafadhili. Hapa kwenye forum hii mengi yameongelewa juu ya madhara yatokanayo na misaada ya ufadhili, kwa maana hiyo basi ili kupiga vita ufadhili hatuna budi kubuni njia ambazo zitatutoa katika dimbwi hilo hatari.

Nyambala umeanza, basi na sisi wengine tujaribu kuwa positive au kuleta constructive critisism ambazo Nyambala na wengine wote watakao kuwa positive wanahitaji katika kuboresha hoja zao.

Baadhi yetu bado tunadhani kuwa maendeleo ya nchi huletwa na serikali au vyama vya siasa au viongozi wao, la hasha, maendeleo ya kweli katika nchi huletwa na jumuiya (communities) mbalimbali ambazo zinaainisha matakwa yao katika maeneo yao na kubuni namna ya kutimiza matakwa hayo. Mfumo huu ni mfumo wa kujituma ndiyo unaotumika sana katika nchi zilizoendelea au nchi tajiri. Ni mfumo ambao upo katika kila ngazi ya maisha ukianzia ngazi ya familia hadi kitaifa.

Kwa mfano katika ngazi za familia, mkazo huwekwa katika kuhakikisha familia inajiwekea akiba (savings) au inanunua stocks. Au familia inaanza na kuimarisha biashara ambayo hufanywa nyumbani na hatimaye kuwa biashara ya mamilioni ya fedha au kuwa kampuni kubwa.

Vilevile yapo matakwa ambayo hufanywa katika ngazi ya mtaa/mitaa ambapo huangalia mahitaji yao na kufikiria jinsi ya kuyapa ufumbuzi kwa mfano labda wanahitaji Maktaba, kuimarisha ulinzi nk. nk. Hivyohivyo hali hiyo inaendelea hadi kufikia ngazi zingine.

Nikirudi kwenye wazo lako Nyambala, ninawasihi wale wote wenye nia ya kweli na wanaoamini kuwa maendeleo ya nchi yetu yako mikononi mwetu basi wajaribu kutoa michango itakayoboresha wazo hili.

Kabla sijahitimisha kwa sasa nisingependa kuwa mchoyo wa fadhila, ninawashukuru wachangiaji wote waliopita hasa Rev. Kishoka kwa kubakia na kuendelea kuwa chanya wakati wote.
 
Having a brilliant idea is one thing, but having to actually deliver it is another story.

If Tanzanians of different ethnic, religious, social and economic backgrounds in urban areas all over the country cannot be expected to pull their resources together and repair something so trivial and basic as dilapidated neighborhood roads, how the hell could anyone entertain the idea of locally led private initiative to plan and finance a billion dollar project of the magnitude sketched above? Pure wishful thinking if not day dreaming!
 
Nashukuru sana wakuu kwa mawazo yanayoendelea kutolewa, Enywayz nachojifunza hapa ni kwamba watanzania tumekuwa reduced to an extent of thinking kwamba taifa hili litabaki hivi hivi na zaidi litaendelea kudidimia. Well kama tatizo ni mafisadi how many are they compared to the rest of Tanzanian population. The idea into this project ni namna gani tunaweza kufanya kitu kikubwa kwa nchi yetu sisi wenyewe (Included projects highlight uwezo tunaoweza kuwa nao). Suala la kwamba mtu akitoa hiyo $1000 basi anakuwa hawezi tena kulipa karo za watoto, chakula na mahitaji mengine ndio mtego tunaojitega watanzania kila siku. Tukumbuke kwamba China wakati inajenga reli ya Tazara hali yake kiuchumi haikuwa nzuri kiasi hicho na kulikuwa pia na baa la njaa. Urusi pia ilipokuwa inatusaidia it wasn't based on surplus. Sasa kwa sisi wenyewe na faida yetu wenyewe tutashindwaje kujinyima??????. Kama una alternative solution is warmly welcomed. Let us think and live positive.

Big up Rev. Kishoka,Pundamilia na wengine woote.
 
In one of his Presidential Campaign meetings, Senator Obama quoted a famous phrase from the Dr. Martin Luther King Jr's speech 'I have a dream...' and Obama asked the audience, '...were just the words?'
 
Nashukuru sana wakuu kwa mawazo yanayoendelea kutolewa, Enywayz nachojifunza hapa ni kwamba watanzania tumekuwa reduced to an extent of thinking kwamba taifa hili litabaki hivi hivi na zaidi litaendelea kudidimia. Well kama tatizo ni mafisadi how many are they compared to the rest of Tanzanian population. The idea into this project ni namna gani tunaweza kufanya kitu kikubwa kwa nchi yetu sisi wenyewe (Included projects highlight uwezo tunaoweza kuwa nao). Suala la kwamba mtu akitoa hiyo $1000 basi anakuwa hawezi tena kulipa karo za watoto, chakula na mahitaji mengine ndio mtego tunaojitega watanzania kila siku. Tukumbuke kwamba China wakati inajenga reli ya Tazara hali yake kiuchumi haikuwa nzuri kiasi hicho na kulikuwa pia na baa la njaa. Urusi pia ilipokuwa inatusaidia it wasn't based on surplus. Sasa kwa sisi wenyewe na faida yetu wenyewe tutashindwaje kujinyima??????. Kama una alternative solution is warmly welcomed. Let us think and live positive.

Big up Rev. Kishoka,Pundamilia na wengine woote.

Nyambala,

Kwa Tanzania lazima tukubali kuanza na porojects ndogondogo ambazo zinaanzishwa na makundi madogo madogo ya Watanzania.

Sio rahisi kwa TZ kuwa na project kubwa namna hiyo na ikafanikiwa. Kuna factors nyingi sana ambazo zitatakwamisha zikiwemo ujinga wa watu wetu, ueleo mdogo, uvivu, ufisadi nk.

Hapo ndio maana ni muhimu kuanza na projects ndogo ndogo ili zile zitakazoonekana zinafaa basi watu wengi zaidi wanajiunga na zinaendelea mbele.

Angalia katika maendeleo ya dunia, projects zote za maana zilianzia chini na makundi madogo sana ya watu ukiachia zile projects za serikali. Faida ya kuanza chini ni kwamba kunakuwa na learning process. Unafanya makosa, unajifunza, unayarekebisha. Hata kwenye biashara ya nyanya kuna makosa utafanya tu, ila failure yake haiku cost mno, tofauti na mradi wa dola bilioni moja, ukichemsha, kuja kurudi hapo hakuna tena.

Imagine miradi kama ya Olympic nk. Kwa UK walikadiria bilioni karibu tatu, sasa wanasema mradi utachukua bilioni 10. Je imagine huo mradi ungelikuwa ni pesa za mtu mmoja mmoja, hapo hapo kila mtu angelikuwa anahangaika kuhamisha pesa zake.

Kufikiria ni jambo zuri, lakini kwa uzoefu wa wengine kusimamia projects, ni kwamba anza na projects ndogo ndogo.

Hata kwa Tanzania projects kubwa nyingi zimetushinda mno. Kwanini tunashindwa kutumia mifano kama ya mashirika ya simu TZ? Wengi walianza kidogo kidogo lakini leo karibu wapo nchi nzima.

Hata kwenye umeme, binafsi sikuona umuhimu wa kuleta Richmond badala ya kuanza kuangalia uzalishaji umeme kwa mkoa au kanda. Mfano wa nchi kama Scandinavia ambazo karibu kila wilaya au mkoa ina source yake ya umeme. Matokeo yake miradi inakuwa simple na rahisi kuitekeleza.
 
Back
Top Bottom