Watanzania Makazini Huwa Tunatafakari...?

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Waungwana;

Nimekuwa natatizwa na jinsi huduma zinavyotolewa kwenye taasisi (hasa za umma japo na za binafsi nimeona kitu kile kile). Hivi huwa tunajiuliza mantiki ya kufuata utaratibu fulani? Natoa mifano ifuatayo:

1. Kuna siku nilinyimwa huduma benki moja (niliandikiwa hundi na mwajiri wangu ambayo ni "open"), sikuwa na kitambulisho cha kazi ila nilikuwa na pasipoti. Yule mfanyakazi wa benki hakuwa tayari kunilipa kwa kutumia pasipoti yangu kwa kuwa "taratibu inasema uje na kitambulisho cha kazini kwako au shahada ya mpiga kura" (hata walipokuja "supervisor" na meneja wake wa tawi walikuwa na msimamo kama huo).

2. Nilikuwa nafanyiwa "interview" ya kazi ambayo sifa iliyotakiwa ni angalau shahada ya kwanza. Nilikuwa "disqualified" kwa kuwa sikuja na cheti cha kidato cha nne na sita pamoja na "University Degree", mimi nilikuwa na "Academic Transcript" - ambayo ukurasa wake wa nyuma unaonyesha nilichaguliwa kujiunga na chuo kikuu kwa vigezo vipi.

3. (Hii inamhusu mtu mwingine japo niliishuhudia mwenyewe) Mstaafu mmoja alikuwa ana hundi yake "open" benki. Hakuwa na kitambulisho (ukistaafu unamrudishia mwajiri kitambulisho chako) ila alikuwa na pasipoti ila imeisha muda wake wa matumizi. Hakupewa huduma kwa kuwa pasipoti yake "ime-expire".

Nawauliza waungwana; kuna uhalali wowote wa maamuzi ya namna hii?
 
Case 1 ni bullshyt, hivi hizi benki zinataka biashara au hazitaki? Kina Kingunge wanaiba mamilioni kwa mamia na wala hawaulizi, mtu unakuja na hundi na kitambulisho maswali kibao.

Case 2 ni bullshyt pia, what's next? Watataka color picture book yako ya nursery school? In any case mtu anayetumia muda mwingi kuangalia paper qualification bila kuweka umuhimu kwenye actual achievements zako namdharau sana tu.

Case 3 labda kidogo wanaweza kuwa na ground, kwamba huwezi kupeleka expired document kama identification, Hata hapo pia mtu unaweza kumuambia mstaafu kistaarabu tu aende u renew passport na tatizo litakwisha.

Hivi kitambulisho cha kazi na shahada ya mpiga kura on one hand na passport on the other hand, kipi kina uzito zaidi hapo ? Unaweza kusafiri nchi za nje ukajitambulisha kwamba wewe ni mtanzania kwa kitambulisho cha kazini au shahada ya mpiga kura ?
 
Back
Top Bottom