Watanzania KWAHERINI YA KUONANA.

Ndugu Zangu,

Ni matumaini yangu kwamba mu-wazima kwa kujiangalia. Natambua kutokana na sababu nitakazotoa baadae si rahisi kujua kama wewe ni mzima au la. Hata waliotoka Loliondo wanasema 'wamepata nafuu'.

Mimi namshukuru Mungu nimeweza kuwasha simu na kufungua jamvi letu siku ya leo. Namshukuru Mungu kwa sababu ina maana simu yangu ina charge na nina salio. Pia kwa sababu simu yangu inafaa kwa matumizi ya internet.

Wengine watahoji, sasa Albert, wakumshukuru si Raisi wako wa nchi na serikali? Inakuwaje tena unamshukuru Mungu? Sababu zitajulikana.

Ila, kuwaka kwa simu yangu kila siku kunanikumbusha aidha kimoja kati ya hivi au vyote, UMEME na MAFUTA. Haiwezi kuwaka bila kuwa na charge. Siwezi kucharge bila UMEME au MAFUTA ya generator. Hasira kumbe zinaanzia mara tu ninapowasha simu.

Ndugu zangu, hali hii ni ya kila siku. Kila siku iendayo kwa Mungu. Sasa nitawezaje kumshukuru Raisi wangu? Namshukuru Mungu kwa sababu HASIRA zangu zinabaki kuwa hasira, UVUMILIVU unachukua nafasi kubwa zaidi.

Kama HASIRA zinasababishwa na Raisi wangu UVUMILIVU napewa na Mungu siamini kama nakosea kumshukuru.

Yeye aliyetuumba alituagiza tuheshimu na kutii mamlaka za nchi. Ndio maana anatupa UVUMILIVU.

Lakini, HASIRA zikizidi kutokana na hali kuwa ile ile kila siku UVUMILIVU si unapotea?

Mhhh! Nimekumbuka. Mtu mwenye NJAA ni mtu mwenye HASIRA. Ukimwangalia anaweza akakubwatukia 'unamwangalia nani'? Amesahau unamwangalia yeye. NJAA.

Nadhani imetosha kusema kwanini namshukuru Mungu na sio Raisi wa nchi kwa simu yangu kuwaka leo asubuhi.

Madhumuni ya ujumbe wangu wa leo ndugu zangu ni kuwaaga. Kwa herini ya kuonana.

Ndugu zangu, UVUMILIVU umefika mwisho. HASIRA zimezidi. NJAA imepitiliza. Usalama wangu mwenyewe na wale wanaonizunguka uko mashakani.
Wao wana hali kama yangu hakuna wa kumfariji mwenzake.

WanaJF, mtakubaliana nami kwamba tulikuwa na wenzetu, wengi tu humu jamvini ambao tulifanana. Lakini UVUMILIVU wao ulipofika mwisho na HASIRA zao zilipozidi na NJAA zao zilipopitiliza wametuacha.

Sasa hivi wanatubeza. Wengine wanatuonya. AMANI na UTULIVU. Wengine wanasema sisi WACHAWI wa upinzani. Wengine wanasema hatuipendi nchi yetu kisa hatukatiwi umeme na hatujui kero hiyo.

Ni wengi mno jamani. Wao wameondoka bila kuaga. Naamini kama wangeaga wangeshauriwa. Wangefarijiwa na kutiwa moyo wawe na SUBIRA hata kama UVUMILIVU umefika mwisho na HASIRA zimezidi.

Wakatudanganya. Ooh, nipo 'around' 'nachekicheki mazingira hapa nje'. Tumeendelea kuamini kwamba bado wapo. Kumbe walishaondoka siku nyingi wametuachia kichungi cha sigara juu ya meza kutuaminisha kwamba bado wapo.

He! Namshukuru Mungu tena. Kumbe kichungi cha sigara huwa kinazimika. Kimezimika sasa tunajua hawapo tena. Walishaondoka. Ule moshi ulikuwa geresha tu. Mungu mkubwa.

Sasa hivi tunawasikia majukwaani. Kwenye vyombo vya habari. Wanatoa matamko. Wanawasemea wenye HASIRA, NJAA na waliokosa UVUMILIVU. Wanachosema sio kile cha hao wanaowasemea.

Sasa, nani anatishia AMANI na UTULIVU? Kila mwenye akili timamu atapatia jibu la swali hilo.

Basi jamani, nisiwachoshe. Mimi naaga. Imetosha naenda zangu. Niko kwenye hatua za mwisho kuuza kilicho changu niende zangu kusikojulikana. Ninachosubiri ni vitu vifuatavyo kabla sijaondoka;

1. Kitambulisho cha Taifa

2. Cheti cha Umilikaji Ardhi kijijini kwangu - MKUKUTA, MKURABITA nk.

3. Matokeo ya vijana wangu baada ya kumaliza elimu ya msingi na sekondari - MEM n.k

4. Kipimo na ripoti ya daktari kutoka kituo cha afya cha Kata. Tunasubiri maabara ikamilike, mpimaji amalize kusoma na vifaa vinunuliwe.

Katiba na malipo ya Dowans sitasubiri. Mimi si mrushi, najua kama mwananchi hata kama sikufaidika sana na umeme waliozalisha Dowans mchango wangu si zaidi ya elfu 5 kwani tupo Mil. 38+. So nitamkabidhi Mtendaji Kata sh. 5,000 kabla sijaondoka.

Vinginevyo kwaherini ya kuonana. Mkumbusheni Raisi kuhusu maneno yenye herufi kubwa asijidanganye na maneo yaliyo kwenye mabano;

NJAA (eti mwana malegeza) .

HASIRA (eti hasara).

UVUMILIVU (eti huleta mbivu).

SUBIRA (eti ya vuta heri).

Pia, sio wote wataamua kuondoka kama mimi. Wengi watabaki. PATATOSHA kweli?

Wasalaam,

AGM.



GREAT GREAT THINKING! Wenye Akili tu ndo watajua umeongea nini!!Mpaka unaondoka nchi itakuwa paradise!!
 
Mkuu Msando nliweka ahadi ya kuondoka na sikuwa na sharti lolote isipokuwa nlisubiri Treni za rais wangu za mwendo kasi,ila mpaka leo bado,nikapata ahadi ya kasi zaidi,nguvu zaidi n.k kumbe sikujua kuwa ni kasi ya kupandisha gas,umeme,nauli,maji na dowans. Leo hii mpira wa kona utapigwa na Nssf,sijui atafunga nani goli safari hii. Zipo kamati mbili zmejipanga goli lifungwe na mpira uwekwe kati,hapa watz watashika masikio. Siku yangu ya kuondoka niliimbiwa nyimbo ya kuniaga ambayo ilifanya badala ya kuondoka nikae jamvini,nikaweka mkuki chini,nkavua koti,nkalegeza msuli na kurudi chumbani. Mpaka leo nko sebuleni jamvini,napanga safari ya pili mpaka safari7 za alfu ulela ulela,au siku elfu na mia. Nyimbo yenyewe ni: ... Karudi baba mmoja,kutoka safari ya mbali...kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili...watoto wake wakaja ili kumtaka hali...wakataka na kauli iwafae maishani...'Kama mnataka mali mtaipata shambani...'. Hapa nliogopa nkaona bora nibaki nife kiume. Mke mdogo akaja na wimbo.."nirudi kwetu nyumbani,nakufa hapa kwa nini!..." mjomba mchungaji akanijia na story ya mwana mpotevu. Akanionya nsijerudi Tanganyika namlilia baba Tanganyika. Hapana namg'angania baba tupate haki sawa kama Kaini na Abeli. Mkuu vuta huko nivute huku tumfinye mchawi! Mchawi wa upinzani ni mchawi,na mchawi wa taifa ni fisadi. Kaa jamvini mkuu.
 
kaka ninachojua upo na kumbuka kua mabogini wanakusubili umeingia nao mkataba wa miaka mitano umechukua utu wao sijui ila sawa kobe huenda na nyumba yake ila kulukaluka kwa maharagwe ndio kuiva kwake
 
kaka ninachojua upo na kumbuka kua mabogini wanakusubili umeingia nao mkataba wa miaka mitano umechukua utu wao sijui ila sawa kobe huenda na nyumba yake ila kulukaluka kwa maharagwe ndio kuiva kwake

nzom, sasa wewe ndio umemaliza kabisa. Nimesoma nikajikuta nasita na kupata huzuni kubwa moyoni. Umeongelea 'utu' nimeguswa sana. Utu wa mtanzania wa leo......
 
Back
Top Bottom