Watanzania je tunajua maana ya blog

Dear

Member
Nov 18, 2009
46
3
Salaam wanaKijiji wenzangu,
Mwanzo wakati blog zinaanza hapa Bongo nilikuwa siko interest kabisa,baadae nikaanza kuwa na interest taratibu baada ya kusimuliwa sana na watu habari mbalimbali zinavyotolewa humo.
Mwanzo blog moja tu ndio ilikuwa maarufu na inajulikana sana lakini baadae zikafumuka blog mbali mbali na nyingi sana,na kila mtu sasa akijiona wamjini kidogo na anacamera tu anaanzisha blog yake,
mimi kwa uelewa wangu ambao naomba wanakijiji mnieleweshe kama sielewi,
mimi nilivyoielewa hii blog nikama gazeti(mtandao gazeti)gazeti ni chombo cha kutoa habari za jamii kwa wanajamii,ziwe za kisiasa,burudani,michezo na kadhalika.
sasa cha ajabu kuna blog zingine ambazo mimi ninahisi zinapoteza muelekeo,utakuta mtu anafungua blog then anatoa mambo na mume wake wamemfanyia nini usiku,au mume wake kamletea zawadi gani,au kama anamchukia mtu anamtoa picha yake then anaachia comment za kumchafua uyo mtu zionekane ili mradi tu amuabishe.
Kinachonikera zaidi kama ile story ya miss Tz kubakwa,magezti na vyombo vingine vya habari vilitoa kuwa kuna miss TZ kabakwa lakini hawakutaja jina,lakini cha kushangaza kuna blog ya mdada kaolewa na mzungu juzi juzi basi alifanya mambo ya ajabu na kutojua maana ya habari ya kama ubakwaji uwa hawatoi majina wala picha za wabakwaji ili kutomuumiza muathirika kisaikolojia,basi yeye katoa kabisa na picha na victim na jina kamilli,na kuacha watu wakitukana na kukomenti pasipo na pazia.(sijali kama story aliyebakwa ni ya kutengeneza au la je wewe ni nani kutaja jina na kumtoa muathirika wa kubakwa jina hadi sura,je unajua uandishi wa habari ni nini na mipaka yake.
kuna vitu vingi sana nafikiri havifahi kuwekwa kwenye blog,nafikiri mambo yako personal yafaa kuwa kwenye Facebook,myspace,Hi5,Twitter nk.
mwisho wa siku unatafuta Haters pasipo na sababu yoyote.
Kama kuna mtu anamawazo tofauti na Blog naomba aniambie
Asanteni
 
ulichosema ni sahihi kabisa,unapotoa habari fikiri kwanza.Muathirika wa habari yako aweza chukua hatua za kisheria.
 
Pole kwa hilo Braza! Laikini matumizi ya blog when it started ilikua ni Internet Diary, space ya mtu kuandika kuhusu maisha yake ya kila siku... Katika boom ya blog ikagundulika ina weza kutumiwa katika mambo mengine tofauti na ndiyo kama ulivyo sema kutoa habari, kuelimisha etc.
 
Hata mimi ile Blog post ya kubakwa ilinidisturb kusema ukweli, kwani Tanzania hakuna sheria za kulinda identity ya victim? Nadhani inabidi achukuliwe hatua kama zipo.

Nadhani kuna ukosefu wa "class" kwa baadhi ya wanablog. Kama blog ya JD aliweka picha za watu wamechinjwa chinjwa barabarani bila warning yoyote.
 
nafikiri kuanzisha blog hakuhitaji elimu ya uandishi. hapo ndipo linapo anza tatizo la kwanza.
tatizo la pili, wenye blog nyingi hawana 'common sense' ya kujua kuwa habari hii ni kumdhalilisha mtu ninaemuweka hapa ( case ya mtu kufungua kesi ya kubakwa na kuandikwa jina na picha yake blogini)
tatizo la tatu kubwa nafikiri watu wenye blog hizi wengi hawana au kujua `manners`, sasa hapa usishangae mtu kutumia blogosphere kuchochea ugomvi na kadhalika.

sidhani kama serikali inaweza kuchukua hatua hapa, lakini tabia kama hizo zinaweza kukoma pale `aliye dhalilishwa` atakapofungua mashtaka mahakamani.
 
Most of those wanaoanzisha blogs with an exception of the few hawajui maana yake na hata kama wanaijua wanaabuse the meaning and reasons of kuanzisha blog na kuiown na etc.

Huyo mwanamke aliyeolewa na mzungu aliyemtoa huyo mshiriki wa miss tz na issue yake ya kubakwa wasnt proper kabisa hajui kanuni na masharti ya uandishi ni kukurupuka tu. it was the same blog sometime nyuma niliipitia nikakutana na horrible pictures of snakes and how their skins are used to make viatu pochi mikanda etc. yani alionyesha the whole process from kukamatwa mpaka kupata pochi au kiatu. sikuweza kula that day and i was scared to death. nikajuta kwa nini niliingia.

Dear, nadhani ni mambo ya kukopi teknolojia za wenzetu na sie tuonekane hatuko nyuma. tusijue kuwa kuna vigezo mbalimbali vya kufuata kabla ya kuanzisha. besides sidhani kama kuna sheria za blogginh hapa nyumbani ambazo zinaeza kumbana mtu anapozikiuka. pia, seems kuanzisha blog ni rahisi sana ni uwe tu na inetrnet inayoeleweka nadhani.

If i was that girl huyo (mshiriki wa miss TZ) i swear I WOULD SUE big time the blog owner huyo mdada na awe example to the rest of bloggers................
 
JS
Umeleeza vizuri na kufafanua zaidi,
Mimi siku ile natazama ile post nilitamani sana uyu dada aliyebakwa amshitaki mwenye Blog,wewe embu fikiria uyu dada sasa almost waTZ wengi tumeshamjua kuwa ni yeye ndio aliyebakwa unafikiri sasa hivi anaishi vipi na hata uko mbele itakuwaje.

Hata iyo ya Nyoka niliiona ni ya kikatili mno,na hata yeye pia anaonekana ni katili sana,Sema tu huku Bongo hatuna watu wa Haki za wanyama,lakini wangekuwepo Naamini wangemshitaki na kuandamana Blog yake ifungwe.


Utu ni kitu cha Bure Kabisa Jamani
 
Back
Top Bottom