Nimesoma mada nyingi hapa, mtu akiandika mawazo yake kuhusu kiongozi anashushuliwa na kuanza kuambiwa kuwa analipwa na mafisadi.
Imefika wakati watanzania tuwe tunakubali kuambiwa ukweli hasa pale tunapokuwa tumekosea. Ukweli huu unaweza kuwa mchungu, ila kila mtu awajibike kwa yale anayoyafanya ama yawe mazuri au mabaya.
Akisemwa kiongozi hata kama kiongozi huyo ni wa juu kwa mfano Spika Sitta basi tukae chini na kujiuliza kwa nini asemwe? Hata kama kuna uhusiano na huyo anayesemwa say awe baba au mama yako, mume mke wako, mpenzi wako au jirani yako, uwe kwenye kambi yake au awe ni boss wako, inakuwa vizuri kutwanga na kupepeta ili kuhahakikisha tunatoa hoja zilizopembuliwa kiyakinifu.
Inatia woga kuona kiongozi anasema halafu badala ya kutetewa kwa hoja anatetewa kwamba anayemsema ni fisadi au habari inayomsema ina mkono wa fisadi.Tabia ya kuwaamini viongozi kwa asilimia 1000% kwamba wao hawajawahi kufanya ufisadi si mbaya pale inapokuwa na ushahidi uliokamilika kwa kuzipinga shutuma kwa vielelezo na sio kusema eti shutuma zinakuja kwa sababu ya chuki binafsi.
Tuamke, vita ni vita!