Watanzania hatukuupigania Uhuru wetu, tuuchukue sasa kutoka kwa CCM

Revolutionary

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
456
86
Tofauti na nchi nyingine za Afrika na duniani, Tanganyika,Zanzibar ama Tanzania uhuru kutoka kutoka utawala wa mkoloni haukupiganiwa na wengi (mass movement).

Watanganyika wachache ambao ni wanaTANU (kwa Tanganyika) wakiongozwa na Julius K. Nyerere ndio walionegotiate deal kutoka utawala wa kigeni wa malkia wa uingereza na Wachache zaidi wakiongozwa na Karume Kule Zanzibar. Tofauti na nchi kama Kenya ambako kulikua na mass movement kama Mau mau ambapo raia wote waliokua na hasira na ari ya kimapinduzi walipigania kwa pamoja, au Ghana, au South Africa baada ya mapambano ya kiujumla ya miongo kadhaa na kujitoa muhanga kupata uhuru wa wengi pamoja na kwingineko Afrika.

Sasa sijui watanzania kwa ujumla wetu tulikua waoga au wapenda amani hii hii ya woga kama ilivyo sasa sina hakika.

Ninachotaka kusema leo ni kwamba kitendo cha kukosekana kwa MASS MOVEMENT au MASS STRUGGLE katika kupigania UHURU Tanzania Kumefanya UHURU HUO UMILIKIWE NA WACHACHE na kufanya tuliobaki (kutokana na woga wetu au kutegea)tuwaabudu wapiganaji hao! Kiuhalisia UHURU huo unahodhiwa na wachache hao kwani kwa ESSENCE YA. UHURU ni kwamba FREEDOM BELONGS TO THOSE WHO FOUGHT FOR IT!

Maana ya UHURU tuliyopata inahodhiwa na CCM (toka enzi hizo za TANU naa ASP) ndio maana Tanzania tuna katiba za kidikteta toka enzi za Mwl Nyerere, litakalosemwa nao kwetu ilokua ni hewala yaani ilibidi kama tuwaabudu hivi na wao ni kama Miungu watu hadi sasa utawala wa CCM kiuhalisia ni wa kifalme ama kidikteta hadi leo, tunayaona haya kwa namna CCM inavyoendesha siasa zake serikalini hadi bungeni tangu enzi za chama kimoja tena kwa kupotosha dhana ya semokrasia na 'mandate' , hushangai kwanini hakuna accoutability TZ?.

Wadanganyika tuliobakia tunashindwa hata kupigania chochote kwa msimamo thabiti, maandamano yetu yote ya kuelekea ikulu huishia Mnazi Mmoja kama si Buguruni hali ambayo ni tofauti na nchi ambazo UHURU wao ulipiganiwa na na wote. Huko viongozi huwajibishwa kama si na serikali basi wananchi wenyewe. Amini nawaambia Serikali tuliyonayo ni sawa kabisa na kifalme au Kidikteta.

Leo hii naona tunathubutu kiasi kupigania uhuru wetu wenye kama wananchi kupitia CHADEMA ili kurudisha nguvu ya Nchi kwa UMMA kama inavyobidi. Hakika tusizembee na kijiweka nyuma katika vita hii tupigane bega kwa bega pamoja na CHADEMA tusiwaache wao peke yao (ili isije kuwa Uhuru huu ukamilikiwa na CHADEMA pekee)hadi UHURU wa nchi tuumiliki sisi waTanzania, kuanzia
Hapo sisi wananchi tutatawala mamlaka ya nchi na kuwa na nguvu ya kuwawajibisha viongozi kama misri na Tunisia kwani sisi ndio muhimili wa NCHI!

BILA MASS STRUGGLE, NCHI ITAENDELEA KUMEGWA NA WACHACHE!

Asanteni, Nawasilisha hoja kimapinduzi ya kweli!
 
Back
Top Bottom