Watanzania 27 wanamiliki mabilioni Uswisi

Sawa kabisa Dr. Ndungulile. Tujue kama kwa kipato halali kunanuwezekano mtumishi wa umma au mwanasiasa akawa na 90 billion kwen akauntu binafsi?

Fikiria tu mbunge ambaye anachukua 12m per month kwa mda wa miaka mi5 asipotumia hata sumni ina maanisha atasave 720m,bil90 haiwezekani uipate kihalali wengi walihongwa na makampuni ya madini na mafuta!
 
mkuu umesahau WANYONGWE hadharani.!

hilo la kunyongwa nililikumbuka sana,ila sasa tatizo mkuu wa kaya ana-promote haki za kibinadam kwa mafisad,,,hujawah kumsikia bungeni akinena hayo???hadi sitta akamwambia na mafisadi nao wanaviolate human rights
 
Tatizo lako wewe ni Chadema Addicted kila sehemu unaleta ushabiki wa vyama unadhani watanzania wote ni wafuasi wa vyama vya siasa hapa tunaongelea maslahi ya Taifa.
mkuu wewe ndio mchochezi kwa kuleta udakau wa kwenye magazeti hapa jamvini
 
Hapa imetokea mtu kuwazidi kete wenzake ndio tunaona wizi wa 2005 unasemwa leo.
Wezi wetu wanapoanza kutajana basi ukombozi hauko mbali, tayarisha panga au mshale vikae karibu akikimbilia kwako unafyeka miguu.
 
Wanabodi,

Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.

Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012
hapa ndo hua mnaniboa. sa si muwataje tu tujue!
 
Hii nchi kweli shamba la bibi mpaka wakati wa Nyerere napo watu wamefanya ufisadi, tatizo muandishi kaficha majina.

Sipo kisiasa sana,
But Ritz Leo ukweli umenishangaza sana!!
Siamini kama ni wewe ulieweka hii thread, hata kama ume-copy!!

Anyway,
 
Nakumbuka clearly kwenye mahojiano ITV, alikuwepo Dr Slaa, Sita na some other guys, Dr. Slaa akaonyesha jinsi gani fedha zimeibiwa na kuonyesha evidence mpaka za receipt na scanned letters.

Sita, wakati huo akiwa speaker, akasema haya ni makaratasi ya mtandaoni, hatuwezi kufanya kazi kwa maratasi ya mtandaoni. Serikali ya CCm ipo imara na hakuna wizi wowote.

Sasa hivi nikimuona Sita anajifanya mpambanaji nasikia kichefuchefu kabisa......wanasiasa hawa wa CCM wanatakiwa kunyongelewa mbali.

There you are MKUU, mambo ya maigizo tu ya kujaribu kujijenga kisiasa by all means - hooks or crooks everything goes! Mimi binafsi nina imani kwamba JK ana nia thabiti ya kukomesha janga hili la ulaji wa kupindukia - tatizo ni kwamba sasa hivi ana wakati mgumu wa kujuwa amuamini yupi ahache yupi, akipata ushahidi wa kutosha hata huwe rafiki yake kivipi atakutia ndani - mifano tunayo; wakati wa enzi za Kambarage sio kwamba ubadhilifu haukuwepo - ulikuwepo sana lakini sikuwahi kumsikia anamtia former Waziri au katibu mkuu mahabusu au kumfungulia mashitaka! Swali ni kwa nini? sana sana alichokuwa anafanya ni kuwahamisha hamisha na wakati mwingine kuwatelemsha vyeo basi.

Chukulia mfano wa vita vya wahujumu uchumi, nini kilitokea baada ya kukamatwa ndugu yangu marehemu Mzee Barongo, Nyerere kahamuru the late Sokoine amuachie huru Barongo mara moja bila ya kutoa sababu za kulidhisha kwa wananchi, wananchi walipo mzonga zonga Nyerere kuhusu suala la mzee Barongo kuachiwa huru, Nyerere alijibu "Hee ban hee, yaani mtu ukipewa gari kuendesha kwa kasi kwenye barabara ya mashimo atafanyaje? si lazima upunguze mwendo unapofikia kwenye mashimo" kaulihiyo ya Nyerere ilikuwa na dhamila ya kumkingia kifua rafiki ya Barongo!! Nafikili jibu hilo lilimkata maini Mzalendo Sokoine akapunguza kasi ya kushughulikia suala la uhujumu uchumi.

Mimi nikisikia watu wanasema JK ni dhaifu nashanga sana! Hivi angekuwa dhaifu au mtu ambaye hawezi ku-make decision mbona Mh. Lowassa ambaye ni rafiki yake wa karibu na JK angukuwa bado ni Wazari mkuu, wewe unafikili JK angechukuwa simu akampigia SITA kwamba hataki suala la Richmond lijadiliwe Bungeni angeshindwa kuzima hoja ya R'mond? nini kilicho tokea kwa akina Yona, Mlamba, Mgonja na sasa hivi Mzee Iddi Simba - Nani anaweza kutoa ushahidi wa kuonyesha kwamba Marais walio mtangulia JK waliwahi kuwashughulikia marafiki zao bila woga, hakuna.

Nimezungumza mengi kidogo hili wakati mwingine tunapo walahumu watu tujaribu kulinganisha na historia ya tawala zilizo pita.
 
sidhani hata wakitajwa kutakua na tija yoyote, kwa serikali hii.
 
Tatizo lako ukiwa na njaa ndio unakua mzalendo, ukishiba tu tatizo unaanza kuhesabu kesi zilizoko mahakamani na kusifia serika kwamba ni sikivu! Kuwa mzalendo wa kudumu kutetea nchi yako kwa maslai ya vizazi vijavyo, angali isije kutokea vizazi vijavyo vikafukua makaburi yetu kupima upeo wetu wa kufikiri ulikuaje.

Mkuu Idawa,
Heshima mbele. Sina cha kuongeza.

Nakala:
Ritz

TUMBIRI (PhD, University of Hull - HULL City, UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Back
Top Bottom