bigcell
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 219
- 60
Wakuu kwema? usiku wa kuamkia leo wakati narejea home kutoka kuwapa pole wahanga wa mabomu ya gongo la mboto,niliikuta radio inatumbuiza miziki laini,meseji za kuwaliwaza wafiwa,wahanga Walionusurika na milipuko ya mabomu ya g.mboto. Ila kitu kimoja ambacho nilishindwa kumuelewa mtangazaji wa kipindi Gadna James a.k.a King G, wakati akitafsiri au kuuelezea asili ya wimbo,nilimnukuu akisema ' kuna wakati fulani miaka ya zamani kulitokea tetemeko kubwa sana duniani,ila sikumbuki ni nchi gani na mwaka gani,ndipo walipojikusanya wanamuziki wengi na kuamua kutunga wimbo wenye urefu wa dk 7 kwa ajili kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi. Namaliza kumnukuu.Wimbo ukaanza ni 'We are the world' ambao ulitungwa na Michael Jackson na Lionel Richie na kuwashirikisha wanamuziki 45.Wimbo ulitungwa jan 1985 na kurekodiwa mach '85, mahususi kwa ajili ya baa la njaa lilotokea afrika kuanzia mwaka 1982-85 barani afrika ktk baadhi ya nchi esp Sudan,Ethiopia na somali.Naomba aelimishe uma wa tz.