WaTanganyika baada ya kuona Forodhani Park imekuwa na hadhi ya kimataifa nao ?

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Darcityaskari.jpg
Wapi kwa wapi jamani Zanzibar wapo mbele sana ila matatizo ya Muungano ndio yameididimiza ,ona hawa baada ya kusikia kuwa ile sehemu ya aina yake ya kujipumzishia pale Mjini Unguja imekuwa kama Ulaya tayari eti nao wameanza kujaribu ,mtapata tabu sana lakini hamfiki mbali kila kitu kitakauka kwani roho ya baaadhi yenu hawaitakii Zanzibar maendeleo hivyo wakilaniwa wao basi nchi nzima ya Tanganyika nayo italaanika ,sasa hapa haijulikani hata wanafanya nini ,ni wizi tu huo ,ukiuliza hela inayotumika hapo ni zaidi ya bajeti ya Tanzania nzima ,au uongo ?
 
We Mwiba wakati mwingine!!! sasa hiyo forodhani inahusiana nini na picha hii!!! Na, kama si Aga Khan, Karume au CUF wangeweza kukarabati Forodhani?
 
WaTanganyika baada ya kuona Forodhani Park imekuwa na hadhi ya kimataifa nao ?
WaTanganyika ndo watu gani? sisi ni wa-Tanzania, ukitaka kutofautisha na visiwa tuite wa-Tanzania bara.
 
We Mwiba wakati mwingine!!! sasa hiyo forodhani inahusiana nini na picha hii!!! Na, kama si Aga Khan, Karume au CUF wangeweza kukarabati Forodhani?
Wewe hebu uliza huyo Agha Khan amelelewa wapi ?

Na ukweli ndio huo baada ya kusikia ndio nao eti wameanza kupnda na kupalilia barabara ,hivi barabara za bongo si unazijua kama nywele za mtu mwenye kipara ,hazijulikani kama zina bustani au zina vichaka ,basi pandeni japo michungwa katikati ya njia ,si mnaona Zenji wameshaanza kupanda mnazi kitamli kwenye barabara zake hizozhizo chache lakini wamezifanya ni sehemu ya bustani na zinapendeza sana. Wananchi wamepata moyo na kupandisha mori wa kuihuisha nchi yao iliyoambukizwa kensa na Muungano huu uliojaa wezi.
 
WaTanganyika ndo watu gani? sisi ni wa-Tanzania, ukitaka kutofautisha na visiwa tuite wa-Tanzania bara.

Ha ha ha mnaanza kulia hata bado !!! Hakuna WaTanzania ndugu kuna waTanganyika na WaZanzibari sasa kama mnaona aibu kujiita WaTanganyika ,hilo ni lenu ,hata juzi nilikuja kutengeneza pasi yangu mpya ya kusafiria kwa ajili ya kwenda South Afrika kutazama world Cup ,jamaa wa hapo Dar aliniambia wewe Mzanzibari mbona unakuja kutengeneza pasi hapa huko wamekunyima nini ? Nikamwambia nataka kuchukua uraia wa Tanganyika basi alicheka sana na kuonekana mwenye furaha maana cheti changu cha kuzaliwa nimeandika nimezaliwa Tanga wakati nimezaliwa Chanja njawiri.
 
waPemba mnamatatizo ninji! sisi ni raia wa Tanzania, tumeambiwa hivyo toka tunazaliwa, tumejifunza hivyo mashuleni, tumejitambulisha hivyo duniani kote, hivyo sisi ni waTanzania.
 
kama ningekuwa Mipango miji hii sanamu ningelingoa na kulipeleka Mnazi mmoja au kule wizara ya Ulinzi its an eye sore kusema ukweli
 
Darcityaskari.jpg
Wapi kwa wapi jamani Zanzibar wapo mbele sana ila matatizo ya Muungano ndio yameididimiza ,ona hawa baada ya kusikia kuwa ile sehemu ya aina yake ya kujipumzishia pale Mjini Unguja imekuwa kama Ulaya tayari eti nao wameanza kujaribu ,mtapata tabu sana lakini hamfiki mbali kila kitu kitakauka kwani roho ya baaadhi yenu hawaitakii Zanzibar maendeleo hivyo wakilaniwa wao basi nchi nzima ya Tanganyika nayo italaanika ,sasa hapa haijulikani hata wanafanya nini ,ni wizi tu huo ,ukiuliza hela inayotumika hapo ni zaidi ya bajeti ya Tanzania nzima ,au uongo ?

Sasa na hapa napo una lalamika nini?
 
Wazanzibari uta waweza? Wao kila siku kuilalamikia Tanganyika tu ila bado Kwenye Muungano wapo tu.
 
Darcityaskari.jpg
Wapi kwa wapi jamani Zanzibar wapo mbele sana ila matatizo ya Muungano ndio yameididimiza ,ona hawa baada ya kusikia kuwa ile sehemu ya aina yake ya kujipumzishia pale Mjini Unguja imekuwa kama Ulaya tayari eti nao wameanza kujaribu ,mtapata tabu sana lakini hamfiki mbali kila kitu kitakauka kwani roho ya baaadhi yenu hawaitakii Zanzibar maendeleo hivyo wakilaniwa wao basi nchi nzima ya Tanganyika nayo italaanika ,sasa hapa haijulikani hata wanafanya nini ,ni wizi tu huo ,ukiuliza hela inayotumika hapo ni zaidi ya bajeti ya Tanzania nzima ,au uongo ?

Unajua siyo lazima uanzishe thread wakati unajua kabisa huna la maana ila labda umejikuta huna cha kufanya. JF siyo mahali pa wewe ku-refresh mind yako kwa kuandika ujinga.... kakojoe ulale.
 
Na wajaribu kutoka waone....!!
Hivyo vitisho vya aliefumaniwa kunyatia mafuta ya Zanzibar,mkitaka msitake maendelo yalianza Zanzibar na yataendelea kuwepo hivyo hivyo ,maana hiyo Forodhani Park mnaiyonea gere eti nanyi mmeanza kufyeka na kusafisha masanamu ,sie sanamu letu tumelikarabati na sasa lina rangi ya fedha ,najua mida si mwingi nanyi mtaona mmepitwa.Sasa hao jamaa haijulikani kama walimia majani au wanatibua ,wizi tu hapo ,mkubwa ameshachota fedha ya kununulia vitendea kazi.
 
Watoto wa watumwa (wazanzibar) mna maneno ha ha ha ha

Na ujuaji wako Zanzibar hakuna aliefanywa mtumwa ,wala hakuna hilo ,kama ni mtumwa basi walitoka huko mabara juu ,milimani maporini ,halafu kama huifahamu Zanzibar kaisome historia ,huko utajiona kama wewe ndie ulinunuliwa kutoka misitu ya Kongo na Rwanda na kuletwa pwani na kuuzwa,kwa maana wewe uliekulia hapa pwani siku hizi ni kitukuu cha mtumwa sijui kama unalielewa hilo ,au umejua kuvaa suruali na shati na kufunga tai sasa unajiona kuwa ni mzalendo wa Nchi hii ,kama huelewi tarehe zako uliza watu wakuambie ,hebu nitajie kabila lako tuone kama hukutoka malawi au Zambia na hapo ndio itakuwa umebahatika kuna waTanganyika wana asili za huko zaire,wametua hapa na kuona bahari ndio sasa wana kiburi na kujiona kuwa wana haki ya kila kitu ,ndugu usichimbue historia utaumbuka.
 
Unajua siyo lazima uanzishe thread wakati unajua kabisa huna la maana ila labda umejikuta huna cha kufanya. JF siyo mahali pa wewe ku-refresh mind yako kwa kuandika ujinga.... kakojoe ulale.
Sasa wewe mwenye la maana tangu ujiunge hapa hivi umeanzisha TOPIC ipi ,maana hata unachochangia hakina kichwa wala miguu.
 
Hivyo vitisho vya aliefumaniwa kunyatia mafuta ya Zanzibar,mkitaka msitake maendelo yalianza Zanzibar na yataendelea kuwepo hivyo hivyo ,maana hiyo Forodhani Park mnaiyonea gere eti nanyi mmeanza kufyeka na kusafisha masanamu ,sie sanamu letu tumelikarabati na sasa lina rangi ya fedha ,najua mida si mwingi nanyi mtaona mmepitwa.Sasa hao jamaa haijulikani kama walimia majani au wanatibua ,wizi tu hapo ,mkubwa ameshachota fedha ya kununulia vitendea kazi.

Wewe na seif sharrif hamad mna mawazo sawa, ila yeye kakuzidi elimu na maarifa. Kama siku zote haja zako ni za aina hii basi nawaonea huruma watoto wako.
 
Ndio hivyo hivyo wewe na Makamba sawa sawa ila wewe umemzidi ujinga nauonea imani ukoo wako.
 
Darcityaskari.jpg
Wapi kwa wapi jamani Zanzibar wapo mbele sana ila matatizo ya Muungano ndio yameididimiza ,ona hawa baada ya kusikia kuwa ile sehemu ya aina yake ya kujipumzishia pale Mjini Unguja imekuwa kama Ulaya tayari eti nao wameanza kujaribu ,mtapata tabu sana lakini hamfiki mbali kila kitu kitakauka kwani roho ya baaadhi yenu hawaitakii Zanzibar maendeleo hivyo wakilaniwa wao basi nchi nzima ya Tanganyika nayo italaanika ,sasa hapa haijulikani hata wanafanya nini ,ni wizi tu huo ,ukiuliza hela inayotumika hapo ni zaidi ya bajeti ya Tanzania nzima ,au uongo ?

Yaani wewe Forodhani Park ndio maendeleo??
PLEASE GIVE US A BREAK!!
 
Back
Top Bottom