Watalii Wafurika SERENGETI kushuhudia NYUMBU wakirejea NYUMBANI toka Mapumzikoni KENYA

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3]WATALII WAFURIKA SERENGETI KUSHUHUDIA MSAFARA WA NYUMBU UKIREJEA NYUMBANI HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI WAKITOKEA MAPUMZIKO YA MWEZI MMOJA KENYA[/h]

Msafara maarufu duniani unaojulikana kama 'Annual animal Migration' unaohusisha wanyama aina ya Nyumbu umeanza kurejea katika makazi yao ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakitokea mapumziko ya mwezi mmoja katika nchi ya jirani ya Kenya, hususan kwenye mbuya ya Masai Mara.

Kila mwaka, nyumbu pamoja na wanyama wengine kama pundamilia na swala hufanya mzunguko maalum unaochukua miezi 12 ya mwaka ambapo miezi kumi kati ya hiyo huwepo nchini katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na iliyobaki hutumiwa na wanyama hao katika eneo la Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.

Mwaka huu msafara huu unaohusisha wanyama zaidi ya Milioni Moja na Nusu na ambao hutembea katika mzunguko wa takribani Kilometa 1,000 umewahi sana kurejea nchini ukitokea mapumziko.

Kwa mujibu wa taarifa za kitaalamu hali hii inatokana na kuwahi kunyesha kwa mvua katika eneo la Serengeti ambapo imesababisha kuwepo na nyasi nzuri ambazo ni chakula muhimu kwa wanayama hawa.

Changamoto kubwa wanayokutana nayo msafara huu mara unaporejea nyumbani ni tukio la kuvuka Mto Mara ambao umejaa wanyama wakali aina ya mamba na viboko ambao nao huwa ni msimu wao wa kujipatia chakula kwa kuvizia na hatimaye kuwakamata wanyama hawa mara wanapovuka mto.

Watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakifurika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushuhudia tukio hili adimu la kuvuka Mto Mara ambalo wengi wao wamekuwa wakiliona kupitia filamu mbalimbali zilizotengenezwa katika eneo hili.

Michuzi Blog
16511139-401852281759718538

Wanatembea km 1000 then wanakaa Masai mara then wanarudi,Je kumaliza hizo km 1000 kwenda na kurudi si zaidi ya miezi 2 kweli?
 
Hii niliiona katika CCTV africa mwezi july. Hakika Kenya wanajua kutangaza utalii. Penia karibe mtanfazaji wa CCTV alikuwa nairusha kwa wiki nzima na ilikuwa imevutia watalii wengi sana . Asante sana China kuitangaza hii safari ya Nyumbu katika TV Yao. Matokeo yake Kenya na Tanzania tumepata watalii wengi sana na hivyo kuboresha pato la utalii.
 
Tunafaidika na nini kwenye hii serengeti? Mafisadi wakuu mmemaliza kila kitu. Pesa inayoingia hata hamtusaidii kuwanunulia watoto kalamu sioni kama snp inatufaidisha.
 
Wa Kenya wanatuchezea ndevu zetu sana!!JK juzi amewaambia tujipange sote kutangaza utalii,yaani kama anawaomba vile,wenzetu wamejipanga muda mrefu sana,na wanajua wanawalenga wapi hao watalii.....sisi tunasubiria huruma ya watalii wenyewe waulize ndio waambiwe nenda Tanzania utaona hiki,na hiki na kupanda mlima Kilimanjaro
 
ah kweli tuna hazina za ajabu sana.sasa me nilikuwa na wazo naona kama wanapata shida kuvuka huo mto kwanini tusiwajengee daraja kubwa kabisa ukubwa wake uwe kama daraja la kigamboni hivi??
 
Tunafaidika na nini kwenye hii serengeti? Mafisadi wakuu mmemaliza kila kitu. Pesa inayoingia hata hamtusaidii kuwanunulia watoto kalamu sioni kama snp inatufaidisha.

watakuambia mapato yanaingia serikali kuu wakati budget yetu ni tegemezi kuna tangazo linalotushawishi tuipigie Tanzania kura kwenye mambo ya utalii kwa sababu hii sitadhubutu kupoteza pesa yangu kuipigia TZ mpaka mafisadi yaondoke madarakani!!!
 
heri yetu sisi tunapata Kimolo.....tunawasubirije hapa Robanda wapite........naanza kuchukua order.......kwa anaehitaji.....
 
Wanyama kuamua kurudi mapema kuliko ilivyozoeleka ni ishara ya kuwa adverse weather, tunapashwa kujiandaa na hilo, kumbuka wakati wa tsunami kule indonesia wanyama walionekana muda mfupi kabla ya tukio wakihama kwa makundi kuelekea milimani, kumbuka kuwa wanyama wana extra telepathic sense inayowajulisha ujio wa kitu kisicho cha kawaida nao huhamia mahali salama zaidi.
 
Mie nilipita serengeti mwezi wa tano mwanzoni,hao wanyama walikua wameishaanza hiyo Migration,nilipiga picha kwa simu ya mchina sasa inagoma kuwaka.nikifanikiwa ntapost.
 
Hawa wanyama wangejua bora hata wangebakia huko masai mara, maana huku watapandishwa QATAR AIRWAYS mda si mrefu
 
Magazete ya udaku ya kenya yameanza kuwalalamikia 'masangoma wa kimasai' wa Tz kwa kuwarudisha nyumbu serengeti mapema zaidi hivyo kuwakosesha 'mapato' ingawa wao (kenya) ndiyo wanao watangaza zaidi kimataifa nyumbu hao kuliko wa TZ!
 
Hawa wanyama wangejua bora hata wangebakia huko masai mara, maana huku watapandishwa QATAR AIRWAYS mda si mrefu

Wakenya walisha tangaza kuweka kizuizi pindi yatakapoingia masai ili yasirudi tena serengeti
 
watakuambia mapato yanaingia serikali kuu wakati budget yetu ni tegemezi kuna tangazo linalotushawishi tuipigie Tanzania kura kwenye mambo ya utalii kwa sababu hii sitadhubutu kupoteza pesa yangu kuipigia TZ mpaka mafisadi yaondoke madarakani!!!

Gys we must wake up na kuachana na na biashara ya kupakwa sifa ambazo hazina tija. Tunapoongelea Serengeti ecosystem tunamaanisha nini! Mfano nani anamiliki Ngorongoro mahesabu yake yanakwenda wapi? In short ncaa ni mali ya ccm no quiz! Grumet Sasakwa ni mali ya nani! Huyu Jones kaingiaje hapo, then wakawafukuza wenyeji waliokuwa wanajipatia protini tangu Adam na Hawa kwa kuwaita porchers, ok waliondolewa je wamepelekwa wapi? Maisha wanayoishi ni chaguo lao au ni 'toka ondoka nenda uendako' Grumet sasa ni nchi nyingine kina Mawala associate ndo wanatumaliza Watz wenzao. Yapo mengi ya kuhoji tuamke na siyo kushabikia gnu wamerudi je unawakatiaga majani au unawachanjaga dawa?
 
Wenzetu kenya wameanza kugawana hifadhi yao kwa ajili ya malisho na kujenga camp site nyingi ndani ya hifadhi yao. Imekuwa ni usumbufu mkubwa kwa nyumbu ndio maana wanakatisha safari yao na kurejea serengeti bila kujali wanakuja kuwafaidisha watu wachache.Nazo mvua msimu huu zimewahi sana ukanda wa serengeti na kuwa neema kwao.mungu ibariki tanzania mafisadi waokoke ili tufaidi raslimali zetu
 
Safi sana sera nzuri na utekelezaji safi wa ilani ya CCM.Kidumu chama cha mapinduzi
 
Back
Top Bottom