Watakaotangaza nia Shinyanga Mjini kukiona

Mawazo na imani za kishirikini karne hii zisipewe nafasi. Ni aibu kwa mleta thread kujenga hoja dhaifu inayopambwa na ushirikina ambao mzizi wake ni ujinga!
 
Kazi kweli kweli....uchawi upo ni kweli, lakini kama kuna mtu analoga wenzake bila makosa, atakayetakakugombea ubunge shinyanga mjini asitangeze hadharani, anitafute nimuelekeze sehemu ya kwenda, akirudi shinyanga hatakufa na kama atapigiwa kura na wananchi, atashinda...dawa ya mchawi siyo kumloga, ni kujizindika, akija kichwa kichwa anatangulia mwenyewe....habari ndiyo hiyo....
Ama kweli shule za kata zinaiua nchi hii, hivi kweli wasomi mnaotumia computer mnweza kujichimbia katika imani za kijinga kiasi hiki? poleni sana vijana!
 
Waheshimiwa uchawi upo. Sasa ili kumdhibiti mchawi unachotakiwa kufanya ni kumwamini YESU yaani KUOKOKA. Amini usiamini mchawi atakaye jaribu kutuma ndumba zake zitamrudia yeye mtumaji na hakika atadhalilika vibaya mno hii ikiwa ni pamoja na kumkuta uchi wa mnyama mchana kweupee...! Hivyo Watarajiwa wagombea wa ubunge jimbo la Shinyanga mjini msihofu zingatieni ushauri huu unasaidia sana.
 
si swala la kupuuza
Ni suala la kuupa kwa nguvu zote. Kumbuka yule mnajimu maarufu Africa mashariki na kati alisema atakayesimama kumpinga mgombea fulani atakufa , mbona watu walimpinga na bado wapo mpaka mnajimu mwenyewe akatangulia mbele za haki,
 
Ama kweli shule za kata zinaiua nchi hii, hivi kweli wasomi mnaotumia computer mnweza kujichimbia katika imani za kijinga kiasi hiki? poleni sana vijana!

Acha kuropoka mkuu hebu soma maandiko haya kutoka kwenye BIBLIA;
Kutoka 7:11-12
Daniel 5:15
Matendo 13:6
Ufunuo 22:15
baadaye ukihitaji nitakupa maandiko zaidi kutoka vitabu vitakatifu; yaani Biblia na Qu'ran.
 
Uchawi upo, hata uzushi ni habari ? Sasa kwanini Usalama wa Taifa hawamchukulii hatua huyu jamaa !
 
I can agree with statement on the ground that two people died while contesting against Shashu Lugeye. Mkuu kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa Shashu alikuwa mkuu wa wilaya ya KIBONDO, na wapinzani wake katika uchaguzi mkuu walikuwa wanakufa kabla ya kura kupigwa.

1. John Mgeja (aliyekuwa katibu mwenezi wa CCM) alifariki kabla ya kura za uchaguzi mkuu kupigwa na jimbo likastopisha uchaguzi wa wabunge mpaka CCM itakapopata mgombea

2.Aliyepatikana kumrithi Mgeja baada ya kifo chake naye alifariki kabla ya uchaguzi kufanyika

3. CCM wakaamua kumuweka mtanzania mwenye aili ya kiasia ambaye alitangazwa mshindi na tume ya uchaguzi.

In general matukio kama hayo ni lazima yataleta hisia zisizo za kawaida kwa wananchi. Japo tunakataa kuwa hii tread ni very low(Masanilo), etc ila ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa on ground wananchi wa Shinyanga wanasema kuwa Masele alimuua Shelembi Magadula, na hii mimi siyo nimeisoma hapa JF ila nimeisikia kwa wazee watatu tofauti Shinyanga ambao wao hawajui hata maana ya internet ni nini, Ukiwauliza hivi nani alishinda Shinyanga wanakwambia Magadula ila walimnyima na Masele kamuua kichawi. Sasa kama wananchi local people wanakuwa na hisia hizo ambazo ni za kiimani zaidi kulingana na mtu anavyofikiri basi ni wazi kuwa Maselle ana tatizo jimboni mwake na ninahisi kuwa kama angekuwa mtu wa kawaida yale mauji ya vikongwe ya zamani shinyanga kwa tuhuma za uchawi yangemuwinda.

Sasa kama na Kanumba alitangazza nia ya kugombea kwa chama kilichoshinda uchaguzi kihalali CDM mwaka 2010 ni wazi kuwa anayeshikilia Jimbo atakuwa na hofu kuu hasa kama mtu huyo anachukulia ubunge kuwa ni ajira ya kumuwezesh kuishi badala ya kutumikia wananchi.

Ukiangalia karibia 90% au more ya wanasiasa ni wateja wazuri sana wa Kalimanzila. Kama hamuamini subirini wakati wa mkutano mkuu wa CCM mwaka huu kwenye uchaguzi wao wa ndani muone watu watakaotiririka Dodoma. Wanasiasa wengi ni washirikina whether ukubali au ukatae. Ila midomoni wanakwambia serikali haiamini uchawi ila wao kama individuals wanashiriki kikamilifu kwenye imani hii ya giza.

Aliyeteuliwa kugombea baada ya Mgeja alikuwa ni Mohamed Biku, alishinda akafariki siku chache baada ya kuapishwa akiwa anakula raha Zanzibar!
 
Mawazo na imani za kishirikini karne hii zisipewe nafasi. Ni aibu kwa mleta thread kujenga hoja dhaifu inayopambwa na ushirikina ambao mzizi wake ni ujinga!

Kwahiyo unapingana na aliyepo "site"?.Shy sio Ukonga wala Masaki.Unalijua jiji la "GAMBOSHI"?.Kama huamini nenda katangaze nia,na dunia itakupa majibu,maana utapelekwa Gamboshi city bila kupenda.
 
Habari imeeleza kuwa yeyote atakaye tangaza kugombea ubunge jimbo la shinyanga mjini hatari ipo mbele yake, hii inatokana na mmliki wa Jimbo hilo Mh steiven Masele kujipanga kuhakikisha ana wamaliza wabaya wake wote kwa ndumba.

Alianza na Shelembi mtu ambaye si tu kwamba alipendwa sana mjini Shinyanga pia ndiye aliyeshinda ubunge wa hilo jimbo mwaka 2010 lakini hakutangazwa, baada ya muda mfupi alifariki dunia na tetesi zinasema aliuwawa na mganga wa Steiven Masele ambaye anaishi huko Mwamadulu ambaye ni mama yake na mbunge huyo kijana anayeendekeza sana ushirikiana. Kifo cha Shelembi kimetokea karibuni mwaka mmoja sasa umepita na CHADEMA mkoa wa shinyanga wako kwenye maandalizi ya kumbukumbu yake.

Muda si mrefu Kanumba alichukua kadi ya chama cha demokrasia na maendeleo kwa msaada mkubwa wa mwenyekiti wa BAVICHA John Heche, ana Heche alikuwa anampigia chapuo kwa viongozi wa chadema taifa ili awe mgombea wake kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 kwa ngazi ya ubunge mjini Shinyanga.

Mtoa habari hizi amedai kuwa baada ya bwana masele kugundua kuwa popularity ya bwana kanumba ni kubwa njia pekee ni kumuondoa duniani, wengine wanaotajwa kwa majina kuwa wako kwenye orodha ya kutangulia mbele ya haki kama tu watatangaza nia au watajaribu kugombea jimboni humu wameonywa, ndugu Tumbo ambaye siku za karibuni amekuwa akipigana kumbo na viongozi wa mkoa hapa shinyanga kwa lengo la kugombea uenyekiti wa mkoa ili baadaye aje ajiteuwe kuwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo.

Mwingeine ni Rachel mashishanga ambaye ni mbunge wa viti maalum amabye naye kwa kutumia wapambe wake amekuwa akuhusishwana hizo tetesi za kutaka kugombea na aliwahi kusikika katika mkutano wa kampeni kata ya masekelo akiwasihi wananchi wamchague diwani wa Chadema ili wampe moyo wa yeye kugombea hilo Jimbo, mara tu baada ya kauli yake hiyo siku mbili baadaye alianza kuumwa miguu kiasi amabcho alishindwa hata kutembea na sidhani kama bado ana hiyo nia.

Vijana wengine wa Shinyanga pia wameshatangaza hizo nia wengine kupitia mitandao ya kijamii, kuna huyu mmliki wa forum ya shinyanga tunayoitaka ameshatangaza kuwa atagombea kupitia ccm lakini hana madhara kwa ndugu masele ndiyo maana bado anaishi, Huo ni muendelezo wa siasa za kichawi kanda ya ziwa.

Ikumbukwe kuwa jimbo la solwa ambalo ni jimbo jirani na shinyanga mjini mwaka 2000-2004 liliwahi kuuwa wabunge wanne na dawa hiyo nasikia ndiyo iliyohamia mjini shinyanga kilimalizia chanzo cha taarifa hiyo

YETU MAcho

We usipende kutisha watu mi nahisi umetumwa na huyo bwana ili kutisha watu wasijitokeze kugombea, naomba umrudishie jibu kuwa hatudanganyiki ng'oo na 2015 sidhani kama ataendelea kuwa MB - Gamba wee!!!!
 
Serious mazee! Ona eti alishnda ubunge kwa kura 1 can u imagine?
its wonderful..u cant believe magic power,ila kwa mtiririko ulivyo na kwa ushindi wa kura moja,i can believe it.labda kama hayajakukuta.
 
kuna thread humu iliwahi kumripoti kanumba kuandaliwa kugombea ubunge shy cdm nkaconect dots na maelezo ya ndugu kuwa alikua ameshatangaza kua ana mpango wa kugombea ubunge 2015 napata point sasa! Masele ni mchawi mana shelembi alikufa cku 2 kabla ya hukumu ya kesi yao!
 
Habari imeeleza kuwa yeyote atakaye tangaza kugombea ubunge jimbo la shinyanga mjini hatari ipo mbele yake, hii inatokana na mmliki wa Jimbo hilo Mh steiven Masele kujipanga kuhakikisha ana wamaliza wabaya wake wote kwa ndumba.

Alianza na Shelembi mtu ambaye si tu kwamba alipendwa sana mjini Shinyanga pia ndiye aliyeshinda ubunge wa hilo jimbo mwaka 2010 lakini hakutangazwa, baada ya muda mfupi alifariki dunia na tetesi zinasema aliuwawa na mganga wa Steiven Masele ambaye anaishi huko Mwamadulu ambaye ni mama yake na mbunge huyo kijana anayeendekeza sana ushirikiana. Kifo cha Shelembi kimetokea karibuni mwaka mmoja sasa umepita na CHADEMA mkoa wa shinyanga wako kwenye maandalizi ya kumbukumbu yake.

Muda si mrefu Kanumba alichukua kadi ya chama cha demokrasia na maendeleo kwa msaada mkubwa wa mwenyekiti wa BAVICHA John Heche, ana Heche alikuwa anampigia chapuo kwa viongozi wa chadema taifa ili awe mgombea wake kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 kwa ngazi ya ubunge mjini Shinyanga.

Mtoa habari hizi amedai kuwa baada ya bwana masele kugundua kuwa popularity ya bwana kanumba ni kubwa njia pekee ni kumuondoa duniani, wengine wanaotajwa kwa majina kuwa wako kwenye orodha ya kutangulia mbele ya haki kama tu watatangaza nia au watajaribu kugombea jimboni humu wameonywa, ndugu Tumbo ambaye siku za karibuni amekuwa akipigana kumbo na viongozi wa mkoa hapa shinyanga kwa lengo la kugombea uenyekiti wa mkoa ili baadaye aje ajiteuwe kuwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo.

Mwingeine ni Rachel mashishanga ambaye ni mbunge wa viti maalum amabye naye kwa kutumia wapambe wake amekuwa akuhusishwana hizo tetesi za kutaka kugombea na aliwahi kusikika katika mkutano wa kampeni kata ya masekelo akiwasihi wananchi wamchague diwani wa Chadema ili wampe moyo wa yeye kugombea hilo Jimbo, mara tu baada ya kauli yake hiyo siku mbili baadaye alianza kuumwa miguu kiasi amabcho alishindwa hata kutembea na sidhani kama bado ana hiyo nia.

Vijana wengine wa Shinyanga pia wameshatangaza hizo nia wengine kupitia mitandao ya kijamii, kuna huyu mmliki wa forum ya shinyanga tunayoitaka ameshatangaza kuwa atagombea kupitia ccm lakini hana madhara kwa ndugu masele ndiyo maana bado anaishi, Huo ni muendelezo wa siasa za kichawi kanda ya ziwa.

Ikumbukwe kuwa jimbo la solwa ambalo ni jimbo jirani na shinyanga mjini mwaka 2000-2004 liliwahi kuuwa wabunge wanne na dawa hiyo nasikia ndiyo iliyohamia mjini shinyanga kilimalizia chanzo cha taarifa hiyo- HUU NI UKWELI ATUNA MUDA WA KUSEMA UONGO ILI USAIDIE NINI?
 
Huwa nawashangaa sana watu wanaojifanya wanamwamini Mungu halafu wanakataa uwepo wa uchawi, wkt ht Biblia inatambua uchawi, wachawi na nguvu zao.
i.e. Bar Jesus, Simon the Magician, wachawi wa Farao dhidi ya Musa.
Wachawi wapo na wana nguvu.
Ni wale watu wenye imani kubwa sana na ucha Mungu ndiyo hawawezi kudhuriwa na wachawi, lkn wengi wetu wenye imani za majina na kurithi, mchawi akiamua kukunyoosha, unanyoosheka kiulaini tu.
 
Back
Top Bottom