Watakaomzuia Lowassa kugombea urais kupitia CCM hawa hapa...

Hao wote uliowataja hakuna hata mmoja ambaye anafikia hata theluthi Kwa EL,kwa ufupi 2015 huyohuyo EL unaemuona lep hatoshi atatosha,kaa chini fikiria kwa makini,kisha fanya Uchambuzi wa kina utagundua haya ninayokwambia.
 
Lowassa ana nguvu ndani ya nyinyiem zaidi ya breakdown, lakini hana nguvu hata kidogo ya kupambana na Slaa mwaka 2015.
 
Lowasa kwa wapenda rushwa,Dr slaa kwa wanyonge wanapenda maendeleo,ccm mpitisheni mfalme wenu huyo aje kuumbuka mbele ya Dr slaa
 
Mkuu Pasco unataka kuzuga watu hapa jamvini lakini wengine tumekushakustukia siku nyingi. Sijui una ID ngapi hadi sasa za kumfagilia Kinara wa rushwa ndani ya magamba fisadi Lowassa.
Kila ukiona tuu ID mpya yoyote kumfagilia EL, ujue ni mimi!.
 
Kimsingi anayemzuia lowassa ni uchafu na ufisadi unaolizunguka jina lake na wasifu wake kama mwanasiasa.
 
Wana JF,

Nimefuatilia utendaji wa baadhi ya mawaziri wa sasa nikagundua kuwa wameweza kufanya maamzi magumu kama aliyokuwa nayo Lowassa. Lowassa anaamini katika maamzi magumu. Bahati mbaya kwake maamzi magumu ambayo amewahi kuyafanya yaliambatana na ufisadi na ubinafsi; wakati akiwa waziri mkuu alijitahidi kumbana magufuli ili asimfunike. Pia alijitahidi kumfunika rais JK. Lengo likiwa ni moja tu-urais 2015.

Sasa tunao mawaziri kama Magufuli, Mwakyembe, Muhongo, Kagasheki, Tibaijuka (?), wanafanya maamzi magumu tena katika mazingira magumu sana na wanafanikisha. Tofauti na lowasa ambaye alifanya maamzi magumu yakafanikiwa pakiwa na fedha za kutosha na akiungwa mkono vya kutosha na rais, mawaziri wa sasa wanafanya hivyo katika mazingira magumu sana na wanafanikisha; tofauti ya pili ni kwamba lowasa aliambatanisha maamzi hayo na maslahi yake binafsi.

Bahati mbaya kwa Lowasa, kukubalika kwake ni ndani ya chama cha mapinduzi tu. Hii ni kwa sababu huku vijijini ukitaja jina la Lowassa, mtu analii-equate na ufisadi. Tegemeo lake limebaki kwa wanaccm ambao nao hawashawishiki bila pesa lakini mawaziri hawa hawana kashfa za ufisadi. Hii sasa itawafanya waccm waanze kumsahau Lowassa kwa sababu mawaziri hawa nao wanafanya maamzi magumu kama yeye alivyofanya. Ikumbukwe kwamba Lowassa alipata umaarufu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mtu wa maamzi magumu.

Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa maadui wakuu wa Lowassa katika juhudi zake za kuwania urais kupitia CCM ni hawa mawaziri.

Sina Cha kuongezea ila nasema umenena muungwana. Niko na wewe kwa hili.
 
Mkuu Ngongo Waziri Magufuli,Membe,Sitta na Mwakyembe wameonyesha uwezo mkubwa sana nategemea yeyyeto kati ya ana uwezo wakutuongoza.Prof Tibaijuka mpaka sasa sijaona anachokifanya,Kagasheki ndiyo bure kabisa Muhongo kwanza si mwanasiasa kabebwa leo unasema anaweza kuongoza la hasha huyu hana lolote.

Mkuu Pasco ni kweli wapo baadhi ya mawaziri wanajitahidi sana bahati mbaya Mkuu Maseto kamsahau Samweli Sitta na Benard Membe.Mpaka sasa sijaona wa kumfikia Membe tatizo la mpaka baina ya Tanzania na Malawi Kikwete kamwachia alishughulikie ili aweze kukuza mtaji wake vyema.
 
Last edited by a moderator:
Kimsingi anayemzuia lowassa ni uchafu na ufisadi unaolizunguka jina lake na wasifu wake kama mwanasiasa.
Atasafishwa na kutakata kama theluji!. Atang'arishwa na kung'aa kama kioo!, atameremeta kama nyota!, atatoa nuru kama mbalamwezi na kutoa mwanga kama jua!, its only a matter of time!.
 
Mzee sita ni mnafiki mno.huyo hafai kwa kiwango kikubwa.Membe hana tatizo kubwa isipokuwa ni mvivu.pia anaposema anasubiri Mungu amuonyeshe maana yake yeye mwenyewe hajiamini kama anaweza.hata akija kuchemka akiwa rais ( Mungu apishe mbali) atasingizia Mungu kuwa hajamuönyesha cha kufanya

Aisee umempatia huyu Membe kweli kweli na kuna wengine hasa Mudhihiri Mudhihiri wana muita Joka la mdimu ambayo pia ni methali inayo sema JOKA LA MDIMU HULINDA WATUNDAO,maana yake ni huyu nyoka hukaa kwenye mti wa matunda kama ndimu,yeye hali ndimu ila anashambulia wanaotungua ndimu,Maana yake ni mtu mwenye roho ya kwanini.
Thank you! umempatia sana

mkuu umemsahau Mulugo Mzee wa Muungano wa zimbabwe na Pemba, aka three R,s Reading, Writing, and Arithmetics!
 
Wana JF,

Nimefuatilia utendaji wa baadhi ya mawaziri wa sasa nikagundua kuwa wameweza kufanya maamzi magumu kama aliyokuwa nayo Lowassa. Lowassa anaamini katika maamzi magumu. Bahati mbaya kwake maamzi magumu ambayo amewahi kuyafanya yaliambatana na ufisadi na ubinafsi; wakati akiwa waziri mkuu alijitahidi kumbana magufuli ili asimfunike. Pia alijitahidi kumfunika rais JK. Lengo likiwa ni moja tu-urais 2015.

Sasa tunao mawaziri kama Magufuli, Mwakyembe, Muhongo, Kagasheki, Tibaijuka (?), wanafanya maamzi magumu tena katika mazingira magumu sana na wanafanikisha. Tofauti na lowasa ambaye alifanya maamzi magumu yakafanikiwa pakiwa na fedha za kutosha na akiungwa mkono vya kutosha na rais, mawaziri wa sasa wanafanya hivyo katika mazingira magumu sana na wanafanikisha; tofauti ya pili ni kwamba lowasa aliambatanisha maamzi hayo na maslahi yake binafsi.

Bahati mbaya kwa Lowasa, kukubalika kwake ni ndani ya chama cha mapinduzi tu. Hii ni kwa sababu huku vijijini ukitaja jina la Lowassa, mtu analii-equate na ufisadi. Tegemeo lake limebaki kwa wanaccm ambao nao hawashawishiki bila pesa lakini mawaziri hawa hawana kashfa za ufisadi. Hii sasa itawafanya waccm waanze kumsahau Lowassa kwa sababu mawaziri hawa nao wanafanya maamzi magumu kama yeye alivyofanya. Ikumbukwe kwamba Lowassa alipata umaarufu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mtu wa maamzi magumu.

Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa maadui wakuu wa Lowassa katika juhudi zake za kuwania urais kupitia CCM ni hawa mawaziri.

hoja yako ina mashiko sana
 
Atasafishwa na kutakata kama theluji!. Atang'arishwa na kung'aa kama kioo!, atameremeta kama nyota!, atatoa nuru kama mbalamwezi na kutoa mwanga kama jua!, its only a matter of time!.

Pasco unanikumbusha hadithi ya binti chura, akaalikwa ngedere kwa sharti ajisugue uso wake hadi weusi usiwepo!!!! ngedere kwa hamu ya kuhudhuria harusi alitumia steelwool kujisugua, hee! alichubukaje bila mafanikio!!!! mchuuzeni lowasa. kama mnataka kushauriwa kamuulizeni Siyoi mtapata broad picture.
 
Last edited by a moderator:
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom