Elections 2010 Watakaoamua mpangaji wa Ikulu hawa hapa

cabhatica

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
1,081
480
Walioandikishwa kupiga kura milioni 19.6
Wanachama hai wa vyama vyote vya siasa takribani milioni 7.6
Wasiokuwa wanachama milioni 12(?). Hawa ndio deciding group. Huwa hawapigi kelele, wanaenda kimyakimya. Hawahitaji kushawishiwa maana wanaelewa.

Msitishwe na mashati ya kijani wala nyimbo za TOT . Ni sawa na kelele za chura mtoni. Hazimzuii ng’ombe kunywa maji.
 
Kwa taarifa yako mimi ni CCM lakini kura zangu zote ninawapa Chadema na sipo pekee yangu kwenye hili...................
 
Walioandikishwa kupiga kura milioni 19.6
Wanachama hai wa vyama vyote vya siasa takribani milioni 7.6
Wasiokuwa wanachama milioni 12(?). Hawa ndio deciding group. Huwa hawapigi kelele, wanaenda kimyakimya. Hawahitaji kushawishiwa maana wanaelewa.

Msitishwe na mashati ya kijani wala nyimbo za TOT . Ni sawa na kelele za chura mtoni. Hazimzuii ng’ombe kunywa maji.

Hilo kundi nimo.

Na nimesha amua. Dr. Slaa 2010
 
kila kona watu wanakiponda kile chama,

Wamiliki wasivoona mbele hawakati tamaa,

Utadhani mchezo wa kuigiza vile jamaa,

Shime wananchi tuungane tumbwage huyu bwana mkubwaa,

2010 Sote tumpigie kura yetu Rais anayetujali ambaye ni Dr Slaa.
 
kwa taarifa yako mimi ni ccm lakini kura zangu zote ninawapa chadema na sipo pekee yangu kwenye hili...................

mimi nilipigishwa kwata la halaiki kwa takribani miezi 6 wakati ccm inazaliwa mwaka 1977. Na baadaye kuwa mwanachama mwaminifu wa ccm.

Kutokana na maneno ya hayati mwalimu nyerere kuwa ccm ni korokoro kutimia kwa kuhalalisha ufisadi rasmi. Ili kuinusuru ccm isije kufutika katika ramani ya vyama vya siasa barani afrika kama ilivyotokea kwa chama cha kanu cha rais kenyetta wa nchi ya kenya, chama cha unip cha ras kaunda wa zambia n.k

nimeamua pamoja na kuipigia chadema nitafanya kazi ya ziada kuhakikisha wagombea wa chadema wanapita katika maeneo yangu pamoja na dr slaa.

Hizi ndizo salamu kwa kikwete anayekumbatia ufisadi!!!!
 
kila kona watu wanakiponda kile chama,

wamiliki wasivoona mbele hawakati tamaa,

utadhani mchezo wa kuigiza vile jamaa,

shime wananchi tuungane tumbwage huyu bwana mkubwaa,

2010 sote tumpigie kura yetu rais anayetujali ambaye ni dr slaa.

mimi nipo kwenye kundi la wasio na vyama utanithibitishia vipi kuwa slaa ndio anaetujali? Na ninatatizika na hili swala la udini ndani ya chama cha muheshimiwa slaa sijui nalo lina maelezo gani bila kusahau ukabila na mambo ya koo ndani chama cha chadema.

Ahsante sana.
 
mpaka sasa hata hiyo idadi ya wapiga kura milioni 19 ina walakini. bado tume ya uchaguzi haijaliweka wazi daftari la wapiga kura ili wapiga kura walihakiki kuhakikisha details zao. kuna tetesi kwamba idadi ya wapiga kura haizidi milioni 16 na hiyo milioni 19 ni kwa ajili ya uchakachuaji. ili kuondoa hiyo hofu wakati umefika sasa kwa tume ya uchaguzi kuliweka hadharani daftari la wapiga kura, wengi tulitegemea lingekuwa hadharani mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika.
 
Mimi kura yangu ni kwa mgombea anayeweza kuhutubia wananchi kwa zaidi ya 40 munites akiwa amesimama bila usaidizi!
 
mimi nipo kwenye kundi la wasio na vyama utanithibitishia vipi kuwa slaa ndio anaetujali? Na ninatatizika na hili swala la udini ndani ya chama cha muheshimiwa slaa sijui nalo lina maelezo gani bila kusahau ukabila na mambo ya koo ndani chama cha chadema.

Ahsante sana.
If you dont have anything to say, dont say it here!
 
mi kwangu kuna kura 6 kwa Dr.Slaa,mpaka babu mlinzi wangu ,tar 31 mkono kwa mkono nampeleka kupiga kura ndo warudi kunywa chai..sitaki utani kabisa katika hili
 
Ukingalia hata CNN ambavyohuwa wanafanya analysis zao za uchaguzi huko Ulaya, huwa wanaweza kabisa kutabiri mshindi kwa kutumia analysis kama hii. Na usually watu ambao huwa hawana vyama ndio mwisho huja kuamua nani ashinde. Analysis kama hizi ndizo zinafaa kuzifanyia kazi.
 
Mimi ni mtanzania na nitatumia haki yangu kwa kumpa kura yangu DR Slaa. Ni kiongozi anayemaanisha anachosema, tena huyatoa yote kichwani bila kukosea. Namchukia yule ambaye hata kwenye kampeni tu ametayarishiwa hotuba ili atusomee, nadhani ni uongo ule ule tuliozoea. hapati kura hata katika familia yangu. Kwi kwi kwi kwi
 
Walioandikishwa kupiga kura milioni 19.6
Wanachama hai wa vyama vyote vya siasa takribani milioni 7.6
Wasiokuwa wanachama milioni 12(?). Hawa ndio deciding group. Huwa hawapigi kelele, wanaenda kimyakimya. Hawahitaji kushawishiwa maana wanaelewa.

Msitishwe na mashati ya kijani wala nyimbo za TOT . Ni sawa na kelele za chura mtoni. Hazimzuii ng’ombe kunywa maji.

"Education makes a people easy to lead, but difficult to drive; easy to govern, but impossible to enslave.
kazi yote 31
 
Wasiokuwa wanachama milioni 12(?). Hawa ndio deciding group. Huwa hawapigi kelele, wanaenda kimyakimya. Hawahitaji kushawishiwa maana wanaelewa.

Mimi sina chama na nipo kwenye kundi hili, nataka mgombea kama sifa za Nyerere alivyotaka. Mimi naamini kuwa Mwaka huu lazima mabadiliko yatatokea tu. mwaka huu najua ni lazima wabunge zaidi watapatikana. Mwaka huu watu wamefunguka macho.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom