Wataalamu wa Kiswahili: Kuna ngeli ngapi za nomino katika kiswahili?

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,133
659
Wandugu naomba msaada wenu katika hili! Nimebishana na baadhi ya waalimu,wanadai kuna ngeli 8 za nomino ktk kiswahili.Kuna kamusi moja imetaja ngeli 12 za nomino ikiweo YA-YA,I-I na U-U ambazo waalimu wamezipinga vikali.Naombeni msaada kwa wanaozifahamu vizuri.
 
Idadi ya Ngeli inategemea na mkabala unaozungumzia ngeli hizo. Tatizo kubwa ni kuwa walimu wengi wanasoma kitabu ki1 na wanang'ang'ania mtazamo mmoja. Ngeli zinapangwa katika mikabala 2. Wanamapokeo na wana usasa. Pia yategemea unaainisha vipi hizo ngeli. kwa mfano, M-WA mwaingine atakuhesabia kuwa M ni 1 na WA ni ya pili.
 
Wandugu naomba msaada wenu katika hili! Nimebishana na baadhi ya waalimu,wanadai kuna ngeli 8 za nomino ktk kiswahili.Kuna kamusi moja imetaja ngeli 12 za nomino ikiweo YA-YA,I-I na U-U ambazo waalimu wamezipinga vikali.Naombeni msaada kwa wanaozifahamu vizuri.
Taab ya watz ni kujua kuzungumza kiswahili lakini hawajui kuwa hawajui kiswahili sanifu. Wataalamu wa lugha ya kiswahili na watusaidie kwa hili la nomino
 
Inategemea unataka zipi kwani zipo za WANAMAPOKEO na WANAUSASA.
mfano: kwa wanamapokeo zipo 9.
 
Wandugu naomba msaada wenu katika hili! Nimebishana na baadhi ya waalimu,wanadai kuna ngeli 8 za nomino ktk kiswahili.Kuna kamusi moja imetaja ngeli 12 za nomino ikiweo YA-YA,I-I na U-U ambazo waalimu wamezipinga vikali.Naombeni msaada kwa wanaozifahamu vizuri.
umepotea njia nenda jukwa la lugha.hapa 2najadili mustakhabar wa elimu sio lugha kjana..
 
Kuna mikabala miwili ya uanishaji wa ngeli upo ule wakimapokeo na ule wa kisasa(kisintakisia) ambao una ngeli tisa(9) na wakimapokeo(maumbo) una ngeli kumi na nane(18)
 
Inategemea unazungumzia kigezo gani kaka. coz kila kigezo kinakupa idadi tofauti za ngeli, yaani
kigezo cha KIMOFOLOJIA,KISEMANTIKIA & KISINTAKSIA
 
Back
Top Bottom