Wataalam wachunguza homa ya mafua ya nguruwe

Gudboy

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
867
77
Waandishi Wetu.

SERIKALI imesema imeanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu homa ya mafua ya nguruwe.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Blandina Nyoni, kuafutia kulazwa kwa watoto wawili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakichunguzwa homa hiyo.

Habari zilizopatikana jana zilisema hali za watoto hao ambao ni wanafunzi, zinaendelea vizuri.
Nyoni alisema alikiri kuwa ofisi yake imepokea taarifa kuhusu wanafunzi kufanyiwa uchunguzi wa homa ya mafua ya nguruwe, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Serikali imeanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo,taarifa za awali zilipatikana baada ya mama mmoja kuja na mwanaye mwenye dalili za ugonjwa huo,alisema Nyoni.

Alisema baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina, mtoto huyo alibainika kuwa na ugonjwa huo na kupewa tiba kamili.

Alisema hali hiyo iliwalazimisha watalaam wa afya kwenda katika shule anayosoma mtoto huyo, ili kufanya uchunguzi wa kina.

Mkurugenzi wa huduma ya tiba katika hospitali hiyo, Profesa Andrew Swai, alisema watoto hao wamekuwa ni Watanzania wa kwanza kuugua ugonjwa huo tangu ulipogundulika Julai 8 mwaka huu.

Swai alisema mtoto mmoja miongoni mwa hao, amethibitika kuwa na ugojwa huo na wa pili ana dalili zote na kwamba hatua za kumpima zaidi zinaendelea.

Mtoto wa kwanza alifikishwa hospitalini hapa Jumamosi ya wiki iliyopita na wa pili alifikishwa jana (juzi) asubuhi, huyu wa kwanza anaendelea vizuri kulingana na vipimo vyake alisema
Vipimo vyake bado havijathibitisha, ingawa anadalili zote za ugonjwa, tunategemea kupata majibu kamili leo hii baada ya majibu kutolewa alisisitiza Profesa Swai.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo, alikataa kutaja shule wanayosoma watoto hao, akichelea kukiuka maadili.
Mwananchi ilifanikiwa kufika katika shule ya Dar es Salaam Independent School (DIS) waliyokotoka watoto hao na kuweza kuzungumza na Mkurugenzi wa shule Susan Huxtable ambapo alikubali kuwa watoto hao wanatoka katika shule hiyo.

Huxtable alisema, baada ya ugonjwa huo kutokea walituma barua kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ili kuchukua tahadhari za afya kwa wengine.

Naye mkurugenzi wa shule hiyo, awali alichukua hatua ya kutuma barua kwa Waziri wa Afya ili kutoa taarifa za wanafunzi waliogundulika kuwa na ugonjwa huo, lakini mpaka sasa hawajapatiwa majibu yoyote kuto katika wizara hiyo.

Tulipoona idadi inazidi kuongezeka tulituma barua kwa waziri wa Afya lakini mpaka sasa hatujapata majibu yoyote kutoka kwake wala ofisi yoyote wizarani hapo, alisisitiza mkurugenzi huyo.
Habari hii imeandaliwa na Jackson Odoyo, Minael Msuya na Thomas Ludovick

MWANANCHI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom