Ndetirima
JF-Expert Member
- Oct 4, 2011
- 1,008
- 784
Kama ni kweli, ukisikia watu wanasema mwanaume kaolewa ndiyo kwa staili hiyo. Hapo Mume sio kichwa kama wanavyofundisha na kusisitiza misikitini na makanisani hapo mume ni vidole kama sio kucha kabisa. Na hao ndugu za mume wako wapi wanashindwa nini kumsaidia kaka yao kama tayari madawa yameshamuharibu? Kwa upande mwingine inaweza kuwa Mume anapenda hiyo hali iendelee hivyo hivyo huwezijua labda anafaidi zaidi huko nje anakolala. Pia anaweza kuwa anawashughulikia hao ndugu za mke wake kwa malipo anayoyajua mwenyewe. Lakini mwisho wa siku ndoa ni kati ya watu wawili na iheshimiwe na watu wote.