Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 22
- Thread starter
- #21
We acha tu. Ni tz pekee .
Kwani vijana wetu hawawezi kazi hizo wakuu?
We acha tu. Ni tz pekee .
Vijana hawajatulia.
We acha tu. Ni tz pekee .
Siri yake ni kuwa ipo imani kubwa ndani ya system kwamba, old soldiers never die...they just fade away. Kuwaacha watu waliokuwa na siri nyingi za ulinzi bila control, inaweza kuwapa wao shida, kama waliokuwa nazo wakiamua kuzitumia vibaya.Nimefuatilia kwa muda mrefu suala la uteuzi wa viongozi katika Tanzania nikashindwa kuelewa usahihi wa mtu kustaafu, eneo moja (hasa jeshini) na kisha kupewa madaraka mengine eneo jingine.
Kwa mfano unasikia KANALI MSTAAFU ..... ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa fulani au wilayaa fulani.
Kuna siri gani kuhusu jammbo hili wana JF?
Wanakuwa washazizoea hela za kifisadi(si unajua zilivyo nyingi)?!Sasa muda ukiisha akiondoka moja kwa moja bila kurudishwa tena serikalini atazipata wapi tena?!
Sharti la hela za kifisadi uzichote kisawasawa,sasa wanaona wakimuweka fisadi mtoto hatazitumia vile inavyotakiwa...!
Bwana weh! wanaogopa watatoa siri wakikaa domant...
Bwana weh! wanaogopa watatoa siri wakikaa domant...
Eti Mkuu.Jamani si kuna muda maalumu wa mtu kustaafu? Na hapa kwetu ni miaka mingapi? na kama upo kwa nini bado wanapeana.
Kwa wanajeshi ukiacha generals, wanastaafu wakiwa na umri mdogo kwa hiyo mtu kama anaelimu nzuri anaweza bado akatumika ktk shughuli nyingine. Mimi kinacho niboa ni kumpa cheo mtu ambaye hana elimu ya kutosha lakini sababu tu ikiwa ni uanajeshi wake, hili si sahihi.
Wanajeshi kazi yao ni ya mkataba nafikiri kila baada ya miaka 6, unajaza mkataba upya kama unataka tena 6 ingine au umechoka.
Sasa mtu akikataa mkataba anaitwa mstaafu, suala la kuteuliwa katika uongozi limekaa kiusalama zaidi ili kuwafanya waliopo jeshini watulie kwani wanajua kuwa nao one day wanaweza teuliwa. Lakini kimaendeleo na ubunifu ni kuua maendelea kwani hawa si wabunifu wa maendeleo (entrepreneurial skills hawana) wao ni wazuri kwenye ulinzi tu.
Ndiyo maana Tanzania hatuna maendeleo bali tuna amani. Wanajeshi hawafikirii kuiondoa serikali madarakani japo inaweza kuwa si kwa maslahi ya nchi. Kitu kingine watawala ni wajanja sana, wanahakikisha wanajeshi wanapata huduma zote muhimu. Yaani hapa kutulizana zaidi ya kuwajibika