Wastaafu walia na serikali...........................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Wastaafu walia na serikali


na Ambrose Wantaigwa


amka2.gif
BAADHI ya wastaafu waliokuwa watumishi wa serikali katika idara mbalimbali wameitaka serikali kufikiria kubadilisha utaratibu wa malipo yao ya pensheni kulipwa kila mwezi badala ya utaratibu wa sasa wa kulipwa baada ya miezi sita.
Walidai kuwa utaratibu wa sasa unawasababishia ugumu wa kutekeleza mahitaji yao ya kila siku ikiwemo kupata matibabu kutokana na kupanda gharama za maisha siku hadi siku.
Wakizungumza na gazeti hili jana mjini Tarime wastaafu hao ambao wengi walionekana kuwa na umri wa kati ya miaka 65-75 walisema awali serikali kupitia hazina ilikuwa na utaratibu wa kuwalipa kila mwisho wa mwezi na kisha baadaye ilibadilisha na kuanza kuwalipa baada ya miezi sita.
Mmoja wa wastaafu hao ambaye pia ni mwenyekiti wa muda wa umoja huo wilayani hapa, Otuno Bwana, alisema baadhi ya wazee hawana watu wa kuwahudumia mahitaji ya nyumbani kama vile chakula na mavazi na wameishi kama ombaomba licha ya kutoa mchango wao kujenga taifa wakiwa watumishi.
“Umefika wakati serikali ituangalie kwa macho ya huruma ikiwa pamoja na kusimamia huduma za msingi kama vile matibabu kwetu kwa kuwa tunastahili kupata mgao wa keki ya taifa ambayo kwa nafasi zetu tulishiriki kuitengeneza,” alisema.
Alisema katika maisha ya mtanzania wa kawaida kiasi cha dola moja ya Kimarekani kwa siku wanashindwa kuhimili makali ya maisha na hivyo kulazimika kuingia mikopo ambayo hujilimbikiza hadi kipindi cha miezi sita na hivyo kulazimika kutumia penseni hizo kulipa.
 
Kuwalipa mafisadi wa DOWANS ni kitendo cha haraka lakin kuwalipa haki halali wastaafu serikali ya kifisadi hii yapata kigugumizi............
 
Back
Top Bottom