Chigwiyemisi
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 531
- 225
Wadau leo asubuhi Waziri Wassira alikuwa anahojiwa TBC1 kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria ya mchakato wa Katiba unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni. Cha kusikitisha na kutia aibu ni kwamba Wassira badala ya kuongea kama Waziri wa Serikali ameongea kama mwanapropaganda wa CCM tena mwenye uelewa wa chini kabisa pungufu ya ule wa Tambwe Hiza.
1. Kwanza ameongea uongo kuwa marekebisho yanayokusudiwa sio maoni ya CDM ni maoni ya rais na CCM na kwa hiyo hakuna lolote linalotokana na maoni ya CDM. Wakati anaongea haya alikuwa anaangalia chini kwa aibu! Shame on him!!!
2. Amekataa kuwa hakuna wabunge wa CCM wasiopenda muswada huo kuletwa tena bungeni wala hawana tatizo lolote na mwenyekiti wao wa chama yaani JK kwa kukutana na CDM na kusababisha muswada huo kurudishwa tena bungeni! Huu ni uongo pia kwa sababu wote tunajua walivyomuwekea bifu!
3. Anajaribu kujenga hoja kuwa marekebisho hayo ni madogo na ni ya serikali na sio kwa kushinikizwa na kwamba waandishi wa habari wanaeneza uzushi!
4. Alikuwa anakwepa maswali ya msingi na kuzungumzia mambo yake mwenyewe akilenga kuwaponda CDM hadi mtangazaji akawa anaduwaa kwani alitegemea anaongea na waziri wa serikali kumbe anaongea na kada wa chama!
Kwa maoni yangu waziri kuwa mbabaishaji kiasi hiki ni dalili za kushindwa! Uelewa wake pia ni mdogo sana kama anashindwa kuelewa kuwa ni wakati gani anazungumzia mambo ya chama na wakati gani anazungumza mambo ya serikali!