Wassira ndani ya DK 45 ITV

Eti mfumuko wa bei ya vyakula uko juu kisa kizazi cha leo kinakula mchele sana kuliko kizazi chake......:angry::angry:..Mijitu mingine bana..aaaaarghhhh..hivi hawa ndo watu mnaowategemea wanyanyue uchumi wa nchi yetu?
 
Anamalizia kwa kusema watu wanaohoji wakuu wa wilaya nao wana matatizo,

Anavihusia vyombo vya habari kuwa majukumu yao ni kuelemisha, kuburudisha n.k

Amemaliza ila kifupi kapeta maana Wassira huyu aka Tyson alitakiwa arushe ngumi mle.
 
Wasira kichwa kinafanya kazi kweli yaan alishajua hata maswali atakayoulizwa akaandika majibu kazi kusoma tu kila anachoulizwa.
Ole wake mtangazaji angekuwa mama ndalichako wa necta angesha kuwa deleted kitambo
 
Anakanusha kuwa hakuzomewa, eti wale walikuwa walevi!!![/QUOTE]
Hata gadaf aliwaita wapinzani wake kuwa wamepewa madawa ya kulevya lakini kilicho mpata anakifahamu mwenyewe huko aliko.
 
Mwenye kumbukumbu sahihi naomba anisaidie, Wassira ni msemaji wa CHADEMA maana anaongea kuhusu CHADEMA tu?

CCM hana cha kuwaambia wananchi zaidi ya 'umbeya' kuhusu CHADEMA? Wassira na wizara yake wamefanya nini? ahadi za CCM zimekelezwa kwa kiasi gani?

Mkuu hawana sera zaidi ya kurudia siasa zao za maji taka.
 
Mzee andai hawana wanachama 10,000 bila kufikiria.CCM kila wakishikacho kinanajisika.Jamaa kadanganya kwa hasara ya CCM.Kuwa ktk jiji kama la arusha lenye wapiga kura zaidi ya 100,000/, wasiopiga kura zaidi bado wamekosa idada hiyo?Hiyo itatafsiriwa kuwa wamekimbiwa gradually.Na km ndivyo kwanini wang`ang`anie ushindi ktk jimbo wasilokubaliwa?

Pia kwa upande mwingine kadanganya kwani:
Mzee kimeo kweli.Jimbo lina wapiga kura zaidi ya 100,000 na wasiopiga kura kibao, mzee pia hajui kila siku mji unaingiza wageni wengi tuu kutoka nje ya mji na ni wanachama wa CCM.
 
afadhali kamaliza zake nilikua naskia kichefu chefu
 
Anakanusha kuwa hakuzomewa, eti wale walikuwa walevi!!!
Hata gadaf aliwaita wapinzani wake kuwa wamepewa madawa ya kulevya lakini kilicho mpata anakifahamu mwenyewe huko aliko.[/QUOTE]

Ile ndiyo siasa hali ni mbaya lakini unasema hali siyo mbaya.
 
Kweli CDM ni moto mkali,asilimia 100% ya maongezi yake ni CDM,MZEE AMECHOKA HADI ANAKWEPA KUZOMEWA NA WAPIGA KURA WAKE ETI NI WALEVI!
 
Wasirra anaichana chadema!!

huyu jamaa anaigopa sana CHADEMA, maana kila akipata air time, ni kuisema cdm tu..hata kwenye jimbo lake alijisahau kuzungumzia maendeleo aliyoyafanya, akajikuta akiiponda cdm, na wananchi kumzomea na kutaka kumpiga, mpaka alivyookolewa na polisi. abadilike sasa, azungumze ya kwao, na sio kushambulia cdm, anazidi kuipa cdm air time, wakati alitakiwa ajitangaze au atangaze chama chake!
 
Wasira na U-Tyson:

Bila kuathiriwa na mlalo wowote, kwa tathmini ya vipimo vyote vya matumizi ya lugha, uelewa na mbinu za kujibu maswali ya mwandishi wa habari, leo Wasira, amedhihirisha u- Tyson kwa kumsukukiza kwenye kona ya ulingo na kumgeuza muuliza maswali kwa makonde ( akawa mjibu maswali bila kujitambua).
Tunaweza kusema chochote au kumdharau huyu mzee, lakini kwa leo piga ua, mwenye tatizo ama ni mwendesha kipindi hicho cha dakika 45 na maswali yake au ni kwamba uwezo wa huyu mheshimiwa bado uko juu sana katika kazi ya utetezi na ulinzi wa CCM.

Yaani katika %, leo ameweza kujibu vizuri sana (yapata 90%) maswali aliyoulizwa. Cha kushangaza na kosa kubwa, mwendesha kipindi akamruhusu Tyson kuwa ndiye anamswalisha Mtangazaji kwa ile style kali ya unapokutana na Rais Mahmoud Ahmadinejad!

Hizo 10 % nimemnyima kwa kuongelea sana kampeni (mashambulizi) ya CHADEMA ambao wao hakika wao wako kazini dhidi ya chama tawala ili wachukuwe dola.
 
huku jamaa km asingekuwa kijichekesha+haiba ya hawa waandishi kwa ccm ili wapate u DC jamaa angetishika vilivyo...
Mzee anamshukuru Mungu+ Rais sound km kawafananisha.
 
Back
Top Bottom