Wassira, Mkono wawashambulia wanaharakati

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Mussa Juma na Neville Meena, Samunge
Mwananchi

WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Mahusiano wa Uratibu), Steven Wassira na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, wamewashambulia wanaharakati wa mazingira, wanaopinga mpango wa serikali kutaka kujenga kwa kiwango cha lami, barabara ya kutoka eneo la Kigongoni, Mto wa Mbu hadi mkoani Mara.

Wakizungumza na timu ya waandishi wa gazeti hili waliopo Samunge, Wassira na Mkono, ambao juzi walipata tibaya Mchungaji Ambilikile Mwasapila, walisema ni upuuzi kwa wanaharakati hao kupinga ujenzi wa barabara hiyo na kusisitiza kuwa hakuna athari zozote dhidi ya wanyama pori.

"Tunajua kuwa hawa watu wanatumiwa na nchi jirani, ili barabara isijengwe, lakini wajue kuwa barabara hii ni muhimu kwa maisha ya watu, leo hii maelfu ya watu duniani wanaokuja Samunge kupata tiba, wanataabika kwa sababu ya ubovu wa barabara na kuna wenyeji huku hawana barabara ya uhakika,"alisema Wassira.

Alisema serikali ina dhamira ya kweli ya kutaka kujenga barabara hiyo, kwa manufaa ya Watanzania.

Pia alikanusha madai kuwa barabara hiyo itapita katikati ya Serengeti kama inavyoelezwa na wanaharakati wa mazingira.

"Tunasema kipande ambacho kitapita jirani na Serengeti ni kilometa 53 tu na tumesema kipande hizo kitabaki kuwa cha changarawe. Sasa hawa wanaopinga sijui wana nia gani na wananchi wa Tanzania na hasa wa Mikoa ya Arusha na Mara,"alisema Wassira.

Kwa upande wake, Mkono alisema baada ya kupita katika barabara hiyo, anakusudia kulifikisha suala hilo bungeni, ili lijadiliwe kwa kina na kuwezesha barabara hiyo kujengwa.

"Hawa wanaopinga ujenzi wa barabara hii ni Manyang'au na wanatumika. Huko kwao kuna barabara nzuri tu lakini huku kwetu wanataka kupotosha kuwa tunajenga barabara ndani ya Serengeti,"alisema Mkono.

Alisema barabara hiyo lazima ijengwe na kwamba wakati umefika wa binaadamu nao kuthaminiwa zaidi ya wanyama."Hawa watoto wa huku kweli tunataka waishi maisha bora, watasoma wapi, watapata wapi huduma muhimu, ifike wakati tujali maisha ya binadamu,"alisisitiza mbunge huyo.

Mbunge wa Ngorongoro, Saning'o ole Telele, alisema wanaopotosha hoja kuhusu ujenzi wa bara bara hiyo, hawajafanya utafiti wa kina kujua sehemu itakamopita.

Hali kadhalika kujua manufaa kwa taifa zima la Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa jumla.

Telele alisema, kukosekana kwa barabara ya uhakika, kunawafanya wananchi wa Ngorongoro kutengwa na wenzao hasa katika kupata huduma muhimu.

"Kukosekana kwa barabara kuna manufaa makubwa kwa wenzetu wa nchi jirani ya Kenya kwani bidhaa nyingi za madukani hapa Loliondo, zinatoka Kenya. Kilio changu mimi miaka yote ni barabara hii" alisema Telele.

Hata hivyo, uchunguzi wa timu ya waandishi wa mwananchi walioweka kambi Samunge, umebaini karibu robo ya magari ambayo yanafika kila siku kijiji cha Samunge kupata tiba yanatoka nchini Kenya.
 
Walikua wana kila sababu ya kwenda kupata kikombe........... kwa huo uchafu walioungea, wao sio experts wa mazingira ila wanavyojidai, uchafu tupu........................
 
kama huna cha kuchangia ni bora uake kimya kuliko kukashifu maumbile ya watu.Kumbuka ni kazi ya Mungu ile

Mkuu japo kukashifu maumbile ya mtu si haki kama ulivyosema, nami nakubaliana na ww! Swali langu ni hv huyu Mkulu Wassira ile sura ni kazi ya Mungu au?
 
Baada ya kupata kikombe wameamua kujifanya wamewaonea huruma wananchi wa samunge mbona kabla hawaja enda hawakutoa hizo kauli zao?

Utafiti kuhusu uharibifu wa mazingira na viumbe hai kama umefanyika umetoa matokeo gani kabla hawajatoa kelele zao zenye mlio wa kikombe? Hata km 1 ina athari kwa mazingira ya viumbe hai, waache siasa wasikilize watalaamu wa mazingira wanasemaje?
 
teh teh jamani wasameheni hiyo ni gia ya kuondokea mnajua samunge watu wamepinda viongozi wakipiga kikombe wao wanawananga sasa wanapokuwa wanaondoka ni Lazima waseme kitu kungekuwa na network wangeweza kuongea na simu ila kwa mazingira ya sasa yanawalazimisha kuongea na waandishi kwani wananchi wanapiga kelele hatutaki politic mmeshachakachua mmepiga kikombe tupisheni.
Hii ndiyo sababu kila kiongozi anaongea vitu visivyoeleweka ni katika kuua sooo !! Teh keh
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom