Wassira azomewa vibaya mkutanoni na kuondolewa chini ya ulinzi mkali wa Polisi!

Ester Bulaya amemmaliza mzee Wassira kwa kuanzisha ligi yake ya Ester Cup. Amewakamata vijana.

Hivi mbona nakumbuka kwamba wakati akiwa Waziri wa Maji Wassira aliwahi kushutumiwa kwa kulipendelea jimbo lake kwa kupeleka mradi mkubwa wa maji huko? Huo mradi uliishia wapi kama Bunda haina maji?
 
huyu mzee alistahili kabisa kuzomewa. majibu yake kama sura yake.Ester bulaya kashawateka vijana kuna kipindi niliwahi kusoma kama ester 2015 anataka agombee jimboni si viti maalum kama Halima mdee. hahaha kazi kweli kweli amchukue lusinde wakatukane
 
Wassira alishinda Bunda by a landslide and a half. Miaka miwili baadae iweje watu wale wale wamekuja kumzomea? Unless alifanya mkutano pembeni ya makao makuu ya CHADEMA jimboni. Itisha uchaguzi kesho Bunda uone itakuwaje kwenye ballot box!
Taarifa hizi za true lies ndio zinafanya wapinzania wanaendelea kupigwa bao sehemu ambazo wanategemea kushinda mpaka dakika ya mwisho, hakuna technical polling wala scientific survey wala in-depth analysis of citizen sentiment. What has happened to change these people's minds all of a sudden?
What is the margin of a landslide?Before you throw words aimlessly check their meaning?
 
Waziri Wasira azomewa


  • Ni wapigakura wa jimboni kwake
  • Akerwa na Wenje kuzoa wanachama
Na Waandishi wetu | Nipashe | 23rd May 2012
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, amejikuta katika wakati mgumu kwa kuzomewa na kuulizwa maswali magumu na wananchi wa jimbo lake wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Bunda, mkoani Mara.

Waziri Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda alikumbwa na zomeazomea hiyo pale alipoanza kumponda Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, kwamba ana shaka na uraia wake na kwamba huenda ni raia wa nchi jirani, ambaye hata hivyo, hakuitaja.

Wananchi waliendelea kumzomea Wasira alipoviponda vyombo vya habari kuandika habari kwamba CCM Bunda yapata pigo, baada ya aliyekuwa mgombea ubunge kwenye kura za maoni za chama hicho mwaka 2005 na 2010, Jeremiah Maganja, kukihama na kujiunga na Chadema.

Alisema kuwa pia habari zilizoandikwa kwamba wanachama wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, wamehamia Chadema siyo za kweli, kwa kile alichoeleza kuwa yeye ni mlezi wa mkoa huo.

Alisema kwamba anaijua vizuri Arusha, ambapo alisema wanachama waliohamia Chadema ni watatu tu, akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James Millya, na kuongeza kuwa vyombo vya habari mara nyingine vinapotosha habari.

Hata hivyo, Wasira alisema mtu kuhama chama siyo kosa na kutamba hata yeye aliwahi kuhamia upinzani (NCCR-Mageuzi) na kwamba akiwa huko aligombea ubunge na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, na kumbwaga.

"Kuhama chama siyo kosa hata mimi niliwahi kuhama na katika kugombea ubunge nilimbwaga mtu mzito Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba, lakini baadaye nilirudi CCM," alisema.

Aliendelea kuviponda vyombo vya habari kwamba habari hiyo haikuwa sahihi kwa sababu, Maganja hakuwa na nguvu ndani ya CCM, kauli iliyowafanya wananchi kumzomea tena wakidai hiyo siyo hoja.

Zomeazomea iliendelea baada ya Wasira kuhoji kwamba Wenje alikwenda kuhutubia Bunda akiwa kama nani, kwa sababu hilo siyo jimbo lake.

"Hivi mimi nauliza Wenje alikuja kuhutubia hapa akiwa kama nani....maana hili siyo jimbo lake?" alihoji Wassira na kabla hajaendelea kutetea hoja yake hiyo, alikumbwa na zomeazomea nyingine kutoka kundi la wananchi wengi wakiwa ni vijana huku wakimuonyesha alama ya vidole viwili.

"Mheshimiwa waziri kumuongelea Wenje kwamba siyo raia na pia alikuja kuhutubia hapa kama nani hiyo siyo hoja, wewe ukiwa mbunge hauoni kwamba unaleta makundi ndani ya jamii...wewe twambie mambo ambayo tangu tukuchague umeyafanya na unaendelea kuyafanya kwa ajili ya kutuletea maendeleo, siyo kumuongelea Wenje hapa," alisema kijana mmoja msomi wa chuo kikuu, Joash Kunaga.

Godfrey Nyamusenda, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, aliuliza swali akisema kwamba sasa hivi hapa nchini wananchi wamekosa uzalendo kutokana na vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali na kuhoji serikali inachukua hatua gani kurejesha uzalendo.

Katika mkutano huo wananchi waliibua hoja ya kukosa maji safi na salama ambapo mwananchi mmoja alihoji kama Wasira naye anakunywa maji hayo.

Waziri Wasira alisema kuwa hata yeye pia anakunywa maji hayo, na baada ya kujibu hivyo akakumbana na zomeazomea nyingine.

"Hata kama mkizomea ukweli ndiyo huo, sasa mnazomea hooooooo nini sasa," alisema Waziri Wasira akionyesha kukasirishwa na zomeazomea hiyo.

Pia Waziri Wasira alisema kero ya maji itaisha kabisa baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji ya bomba kutoka katika ziwa Victoria unaotekelezwa na serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. Alisema uko katika hatua ya pili ambayo ni ya uchimbaji wa mtaro, kwa ajili ya kutandaza mabomba.

Kero nyingine walizozitaja wananchi hao ni pamoja na manunuzi mabaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambapo mwenyekiti mmoja wa kitongoji katika mji mdogo wa Bunda, Maximillian Bwire, alitoa kielelezo cha waraka mmoja uliyokuwa unaonyesha utengenezaji wa milango tisa katika Shule ya Sekondari Nyiendo umegharimu Sh. 6,440,000.

Kadhalika Wasira alielezwa kuwa mkuu wa zamani wilaya ya Bunda, Chiku Ghallawa, alichukua eneo la Shule ya Msingi Balili na kuwekeza majengo ya hoteli bila kuchukuliwa hatua licha ya wananchi kulalamika mara kwa mara.

Naye Mzee Korogo Korogo alisema kero nyingine ni wazee kutokupata huduma za matibabu bure kwenye vituo vya afya na hospitalini, hivyo wamekuwa wakilazimika kununua dawa madukani, pindi wanapougua licha ya sera ya serikali inayosema kwamba wazee watibiwe bure.

Wananchi hao walisema kuwa kero nyingine ni ahadi za Rais kutokutekelezwa kwa wakati, ikiwemo ahadi ya barabara za mjini Bunda kuwekwa lami na barabara ya Bunda-Kisorya hadi Ukerewe kujengwa kwa kiwango cha lami.

Akijibu kero hizo, Wasira alisema sera ya serikali ni wazee kupata huduma za matibabu bure na kwamba siyo wazee wote bali wale ambao hawana uwezo. Kuhusu ahadi za Rais, alisema zinaendelea kutekelezwa na nyingine zitatekelezwa ndani ya kipindi cha uongozi wake.

KIMBUNGA CHA CHADEMA BALAA

Wanachama wa CCM zaidi ya 400, wakiwepo mabalozi 16 na wajumbe wa serikali za vijiji wa Kata ya Mbulumbulu, wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha, juzi walijiondoa katika chama hicho na kujiunga na Chadema.

Kata ya Mbulumbulu ni moja kati ngome chache za CCM, katika Wilaya ya Karatu ambayo halmashauri yake inaongozwa na Chadema. Diwani na viongozi wengi wa serikali za vijiji wanatoka CCM.

Wanachama hao walitangaza uamuzi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kambi ya Simba na kuongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Lazaro Massay, Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Moshi Darabe.

Katika mkutano huo ambao ni sehemu ya mikutano ya Chadema iliyopewa jina la "vua gamba vaa gwanda", mamia ya wana-CCM hao walisema waliamua kukihama chama tawala kutokana na kupinga utendaji mbovu wa watendaji wa serikali za vijiji katika kata hiyo ambao walidai kuwa umekuwa ukiungwa mkono na viongozi wa serikali na CCM katika wilaya hiyo.

Massay ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, alisema hakuna sababu ya wakazi wa kata hiyo kuendelea kug'ang'ania kuwa CCM wakati wanakabiliwa na matatizo mengi yanayosababishwa na uongozi mbaya.

"Jamani nyie wenzangu wa Kambi ya Simba, ondokeni huko CCM, njooni Chadema tukae pamoja kama kata nyingine, matatizo yenu mengi ambayo mmetueleza yanatokana na uongozi mbaya mliouchagua," alisema Massay.

Alisema viongozi wa kijiji hicho wamekuwa kikwazo kutokana na kuvuruga miradi ya maendeleo, ikiwepo miradi ya maji na afya.

"Sisi tumepata malalamiko yenu na tutatuma timu ya wataalam kuja kupitia mahesabu ya kijiji hiki cha Kambi ya Simba na maeneo mengine," alisema Massay.

Naye Mchungaji Natse alisema Halmashauri ya Karatu itahakikisha inawashughulikia watendaji wote wa kata hiyo ambao wanatuhumiwa kwa ubadhirifu.

"Hapa kwenu kuna matatizo mengi sana, ambayo yanachangiwa na hawa viongozi wa CCM kubebana, sasa tunasema ni mwisho, kama tulivyofanya bungeni naomba mfanye na hapa tuwaondoe viongozi hawa," alisema Mchungaji Natse.

Aliwataka wakazi wa kata hiyo kushirikiana kwa pamoja bila kujali itikadi zao na kujitokeza kuchangia miradi yao ya maendeleo na pia kutoa maoni juu ya mabadiliko ya Katiba mpya.

Imeandikwa na Mwandishi wa Nipashe, Bunda na Cynthia Mwilolezi, Arusha.
 
Kuzomewa kwa wassira hii inaonyesha dhahiri ni kwa jinsi gani hakuna aliyesafi ccm manake kama hakubaliki nyumbani ajiulize mwenyewe atakubalika wapi? Hongera wananchi wa bunda kwa kuonyesha hisia zenu waziwazi ni mfano mzuri sana wa kuigwa
 
Wapiga kura wake sasa ndio wamemshtukia kuwa ni Nyara ya Serikali kwahiyo anatakiwa arudi gombe kugombea uongozi
 
1. Amekuwa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani-IDARA YA UHAMIAJI?

2. Kama ni watatu si awataje Majina...?

Jamani penye ukweli tuseme ni kweli ole millya aliokota watu wakadai wamehama ccm kwenda chadema,mie nilikuwepo arusha wazi kabisa ungejionea kama ungekuwepo,
 
Hii jamii forum sasa inaonekana ina Fungamana na chadema,haitoi habari kwa usawa,juzi juzi hapa kuna wanachama wa chadema wamehamia Ccm hamjasema!!!
 
Tatizo kuwa la JF ni ushabiki na uongo. Mimi mwandishi wa habari hii nilihudhulia mutant aw wasira pale Bunda. Mkurya no Iliana saa 9 alasili Hadi saa 12 jioni. Wasira alieleza mambo mengine ya kitaifa. Vyombo vinginevyo vya habari vilikuwepo Kama vile ITV, star TV, channel ten na TBC1 . Vito hivi vote vimetangaza uhalisia uliokuwepo hapo mkutanoni. Kama ilivyo kawaida mikutano mikubwa kama ilivyo kuwa mkutano huo aw Bunda , hapakosi walevi ambao nao waliotaka waonekane wapo. Na kwa walevi waliokuwepo kupigisha make lee ni kawaida. Baada ya hotuba yake ya kusisimua, alijuibu maswali 10. Baada ya kufungwa kwa mkutano majira ya saa 12, wasira alibaki hapo uwanjani akisalimiana na Watu wengi waliomfuata kumsalimu na kumpongeza. Sasa habari ya kuondolewa china ya ulinzi ili tokea wapi? Tukiacha uongo na ushabiki JF itakuwaj combo cha maana cha kupeana habari za kweli.
 
Wassira alishinda Bunda by a landslide and a half. Miaka miwili baadae iweje watu wale wale wamekuja kumzomea? Unless alifanya mkutano pembeni ya makao makuu ya CHADEMA jimboni. Itisha uchaguzi kesho Bunda uone itakuwaje kwenye ballot box!

Taarifa hizi za true lies ndio zinafanya wapinzania wanaendelea kupigwa bao sehemu ambazo wanategemea kushinda mpaka dakika ya mwisho, hakuna technical polling wala scientific survey wala in-depth analysis of citizen sentiment. What has happened to change these people's minds all of a sudden?

Mwanasiasa hutumia ahadi kupata hiyo landslide and a half asipotimiza hizo ahadi huishia kuzomewa. Kikwete alipata asilimia 80% 2005 na 2010 akapata 64%
 
Ushauri wa bure kwa viongozi wasiotimiza ahadi zao, bora wajichimbie huko waliko. Hakuna atakaye wakera, hakuna atakayewauliza. Lakini waelewe kuwa Watanzani wamechoka na wamechoshwa, kwa sasa hawamuangalii kiongozi kavaa nini, anatoka chama gani; wanachotaka ni maendeleo na sio ahadi. Kwa hivyo wasishangae kujiona siku moja na sio mbali, wanageuzwa kama raisi wa muda wa Mali.
 
sijawahi kupata jibu kwa nini wananchi wa Bunda walimchagua Wassira kuwa mbunge wao maana hana jipya na ni mtu wa majungu tu!
 
Tatizo kuwa la JF ni ushabiki na uongo. Mimi mwandishi wa habari hii nilihudhulia mutant aw wasira pale Bunda. Mkurya no Iliana saa 9 alasili Hadi saa 12 jioni. Wasira alieleza mambo mengine ya kitaifa. Vyombo vinginevyo vya habari vilikuwepo Kama vile ITV, star TV, channel ten na TBC1 . Vito hivi vote vimetangaza uhalisia uliokuwepo hapo mkutanoni. Kama ilivyo kawaida mikutano mikubwa kama ilivyo kuwa mkutano huo aw Bunda , hapakosi walevi ambao nao waliotaka waonekane wapo. Na kwa walevi waliokuwepo kupigisha make lee ni kawaida. Baada ya hotuba yake ya kusisimua, alijuibu maswali 10. Baada ya kufungwa kwa mkutano majira ya saa 12, wasira alibaki hapo uwanjani akisalimiana na Watu wengi waliomfuata kumsalimu na kumpongeza. Sasa habari ya kuondolewa china ya ulinzi ili tokea wapi? Tukiacha uongo na ushabiki JF itakuwaj combo cha maana cha kupeana habari za kweli.

Wewe kila mkutano wa Magamba upo.Juzi ulikuwa Bunda.Wiki iliyopita ulikuwa Arusha na ile nyingine ulikuwa Mbeya.Haya malipo ya buku mbilimbili ili kusema uongo ni hatari sana
 
Jamani jamani hili zee lina matatizo huwa hajengi hoja yeye 90% ya hutoba zake jimboni ni matusi tu na vijembe kwa wapinzani, mimi ni mkazi wa jimboni kwake na nilishawahi kuhudhuria mkutano wake ambapo nilipata nafasi ya kutoa maoni na kuuliza swali 1.Kulingana na hadhi ya chuo cha ualimu Bunda ni vizuri kikaboreshwa na kuwa chuo kikuu kishiriki cha elimu,ni kikubwa sana kina mandhari nzuri,majengo mazuri na facilities zipo kimekaa kieimu zaidi.

2. Muda huo ndo matokeo ya msingi yalikuwa yametoka 2009 Nilimwuliza yeye anafikiri ni kwanini mkoa wa Mara umeshuka kitaaluma kwani matokeo ya elimu ya msingi yalionesha tumetoka Tano bora kitaifa na miaka nenda rudi huwa hatutoki Tano bora kitaifa. Mzee huyo hajajibu bali kufwokafwoka tuu!

Kama wassira anaperuzi humu ndani ya great thinkers namtaarifu kuwa ndo namalizia kashahada ka pili 2015 tuko ulingoni pamoja na umri wangu under 30, tumechoka tunataka mabadiliko.
 
Back
Top Bottom