Wassira acha Hasira

Nashangaa wanaaa kujibizana na Wassira. Ni mtu mzuri sana akiwa nyumbani kwake au anapoongea na ndugu na marafiki, lakini akishatoka nje tu, ni monster asiyekuwa na akili yoyote ile.
Sio akitoka nje ila ukiwa mwanasiasa lazima akili ya kawaida iende likizo leo kutana na Makamba utadhani si yule wa mwaka jana.
 
Vituko haviishi na wala havitaendelea kuisha, mheshimiwa kapigwa picha kachapa 'usingizi' nasi sote tumekuwa mashuhuda wa hilo, sasa hapa uchochezi uko wapi hapa? hata mheshimiwa ukisema ulikuwa unaumwa bado huwezi ku -justify kulala kwako wakati vikao vya bunge vikiendelea, labda mheshimiwa ungetumia busara kidogo, baada ya kutumia hizo dawa zinazosababisha hali ya kujisikia usingizi ukeenda tu kupumzika hotelini kwako, bunge si sehemu ya kupumzikia 'rest house'. Vinginevyo wewe ndio unaeleta uchochezi.......
 
Hana ishu huyu babu. Ni kweli alilala. Na hapo alifanya hata watu wengi especially wapiga kura ambao hawakufuatilia hilo gazeti na kuona picha washutuke. Tungoje na mrema atasemaje.. Labda ni overdose ya kikombe cha babu
 
wanakula bata na vimwana mpaka majogoo halafu bungeni ndo kwa kulalia. hilo monster halina dili sioni linachofanya bungeni aende zake huyo mwana kwenda
 
09asiraaa.jpg
wasira alishambulia mwananchi
send to a friend

thursday, 07 july 2011 11:16
0diggsdigg


leon bahati, dodoma

waziri wa nchi ofisi ya rais, (mahusiano na uratibu) stephen wassira, amelishambulia gazeti hili akisema linaandika habari za uchochezi.

Wassira alisema kwamba hivi karibuni gazeti hili lilitoa picha yake akiwa amelala bungeni,akijitetea kwamba alikuwa mgonjwa na alitumia dawa ambayo inasababisha usingizi.

Hata hivyo, wassira alikiri kuwa alikuwa amesinzia wakati bunge likiwa linaendelea, lakini akakiita kitendo cha gazeti la mwananchi kutoa picha wakati akionekana amelala kuwa ni “uchochezi”.

"juzi nilikuwa nimekaa pale alipokaa mheshimiwa samuel sitta, lakini nilikuja hapa naumwa nikapitia zahanati ile pale (zahanati ya bunge), wakanipa dawa ya mafua, ile dawa ya mafua inaweza kukufanya ukawa drowse (ukalala), kesho nikakuta gazeti eti limenipiga picha kwamba nimesinzia.

“sasa ninawaambia wanipige picha niko live sasa. Wanafiki wakubwa hawa wanachochea wanataka kuleta mgogoro usiokuwa na msingi," alisema wassira.

Wassira aliyaeleza hayo juzi jioni wakati akifanya majumuisho ya bajeti ya matumizi ya ofisi ya rais, mahusiano na uratibu ambapo bunge lilimuidhinishia sh7.4bilioni kwa mwaka 2011/12.

Kwa tafsiri ya wassira, mwananchi lilitoa picha hiyo kwa lengo la kuchochea huku akitaja baadhi ya habari ambazo ziliwahi kutolewa na gazeti hili ambazo kwa mtazamo wake anasema ni za kiuchochezi.

Wassira alikwenda mbali zaidi akanukuu vichwa vya habari ambavyo alidai ni za uchochezi akisema: “ kuna gazeti hapa linaitwa mwananchi limeandika chadema yaibwaga ccm kuhusu posho’ kulikuwa na mpira wa posho humu bungeni?,” .

“…. Mimi nilileta hapa hoja ya tume, ndani ya hoja mle ndani ya kitabu tumesema tutatazama upya posho mbalimbali kwa ajili ya kupunguza matumizi. Waziri wa fedha amesema, sasa hoja ilikuwa iko wapi ambayo chadema iliibwaga ccm? Uchochezi mtupu”.

Wassira alikuwa akizungumzia pendekezo la kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge na watumishi wengine wa umma ambalo liliibuliwa na wabunge wa chadema, kiasi cha wabunge hao kuitwa “wanafiki”.

Hata hivyo, baadaye mbunge wa bumbuli, january makamba aliwagutua wabunge wenzake wa ccm ambao walikuwa wakipinga hoja hiyo kwa kuwaambia kwamba suala la kufutwa kwa posho lilikuwa sehemu ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa bungeni na serikali.

Kadhalika, wassira alisema: "juzi alikuwepo mheshimiwa edward lowassa, akatoa maoni yake kama mbunge tu wa monduli, gazeti hili la mwananchi linasema; “vita ya lowassa, serikali ya jk sasa wazi’ vita gani? Ipi? Hawa ni wachochezi na gazeti hili lina asili ya nje."

" na labda lingependa mambo ya nje yawe kama ya hapa, tunamwambia umechelewa hapa hayawezekani," alisema wassira.

Kauli ya makinda
akizungumzia malalamiko ya wassira, spika wa bunge, anne makinda alisema yako mengi ambayo vyombo vya habari vinakosea katika kuripoti.

“tunajitahidi kuwahimiza wajenge umoja wa waandishi wa habari za bunge kwa sababu kwa kweli wanapotosha vitu vingi sana, zaidi ya hapo wanasema mimi naongoza bunge, lakini mbumbu, sasa si unaona mambo yenyewe hayo, halafu ninapayuka payuka, sasa kazi yenyewe hii jamani,"alisema makinda.

Hata hivyo, makinda aliweka bayana kwamba wabunge hushindana kwa hoja ndani ya bunge, lakini akaeleza kufurahishwa kwake na wabunge hao kuanza kukomaa kwa kutokuwea maadui nje ya bunge.
"juzi tulicheza dansi na tundu lissu, wakasema mnaona hawa, niko kwenye gazeti mojawapo, sasa mtu wangu mmoja alikuwa anawasikiliza akaniambia aliwasikia wanasema ‘unawaona hawa waongo kabisa hawa, kila siku anamwambia kaa chini, kaa chini, sasa unawaona wanachokifanya hapa,"alisema.

Aliwaeleza wabunge kwamba wao hawana uadui wala ugomvi ila wanataka watu wawakilishe watu kwa sauti yao na nguvu zao zote, lakini wakitoka nje wanashikana mikono.

"mheshimiwa freeman mbowe, huyu ameshiriki kwenye msiba wa mama yangu, amefika mwenyewe physically (yeye mwenyewe) na wenzake wengi kule ndani kijijini, unajua pale kijijini wanasemaje?" alisema na kuongeza:

"hawa wanasema wapinzani, wapinzani kitu gani? Mbona amefika kwenye msiba? Hivi kweli kwenye msiba hatuwezi kwenda? Mimi nitakwenda kwenye msiba wa mtu yeyote, sasa wananchi watuelewe tuko hapa tumeshinda, tumechaguliwa tunakuja kuwakilisha, tutashindana kwa hoja hapa, nje tutakaa pamoja, tutakula pamoja na tutatembea pamoja."

mwananchi bungeni
wasira alilishambulia gazeti hili ikiwa ni karibu wiki mbili zimepita mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kamati ya hesabu za serikali, augustine mrema kulisifu mwananchi kuwa ni gazeti linaloandika habari zake kwa umakini.

Vilevile, mashambulizi ya wassira yamekuja wakati wabunge kadhaa wamekuwa wakinukuu taarifa za gazeti hili ili kujenga hoja kuhusiana na kero mbalimbali zinazowapata wananchi.

Mojawapo ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma, susan lyimo aliliambia bunge kuwa mfuko wa rais wa kujitegemea (ptf), umekuwa ukijihusisha na vitendo vya kitapeli.

Susan akionyesha kuwa taarifa hizo ni kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la julai 2010 pamoja na mtandao wa youtube, alifafanua kuwa wanachama hao walikuwa wameambiwa watoe sh18,000 kama kiingilio na amana ya sh250,000 kwa ahadi ya kukopeshwa sh1 milioni ndani ya kipindi cha wiki moja

source: mwananchi

hii habari inasikitisha,inakera na inaudhi.

Kwako mhe. Wassira watanzania wanakuheshimu sana lakini pia wanakuvumilia sana kwa upuuzi na tabia zako unazozionyesha ukiwa kama waziri. Mimi nakupa ushauri wa bure kabisa kuwa acha hasira we kibabu.

Hivi gazeti kuchukua picha ya mbunge tena waziri anayelala bungeni ni uchochezi kweeri muraa?????labda kama maana halisi ya neno uchochezi itakuwa imepoteza maana yake. Yaani unataka uende mjengoni ukalale na kukoroma tu huku kila siku ukivuta hela zetu za walipa kodi 150,000/= bila aibu!

Kama ulikuwa unaumwa kwanini uliingia ndani ya ukumbi wa bunge? Kwanini ueze dawa ambazo unajua zitaku-drowse???kwanini hukuomba e.d.(excuse for duty) kwa siku hiyo? Hii inaonyesha jinsi vibabu vya ccm mlivyo na uchu na pesa! Uliona kuwa ukipewa ed hutaingia mjengoni na hivo ile posho ya 80,000+70.000/ =150,000/=ungeikosa!

Je,ulitaka ufie mjengoni au uzimikie humo kwa sababu ya 150,000/=.?

Mjomba yako nyerere aling'atuka mapema kwasababu ya adha kama hizi. Wewe umeanza kuwa kiongozi ndani ya serikali tangu enzi za huyo mjomba yako nyerere miaka ya 1970s mpaka leo unang'ang'ania kuwa mbunge uende bungeni. Shame on you.

Nakushauri uombe kujiuzulu ubunge ili ukapata muda mzuri wa kupumzika na kulala nyumbani kwako na siyo bungeni. Muda uliolitumikia taifa unatosha sana. Lakini kama unang'ang'ania basi unapopigwa picha ukiwa umelala bungeni uache hasira na kulaumu vyombo vya habari kuwa eti vinaleta uchochezi.

Nawasilisha.


mura 150000 na afya njema kipi bora? Tusikuone tena unagombea huku bunda. Kalee wajukuu.
 
Tatizo awa wazee awajui kua wakati umewatupa sanaa...hapa tupo kwenye vipindi mbalimbali vya mpito na maendeleo ya taifa wenyewe wana sinzia ainzia tu bungeni shame on him..it about posho tu ndyomaana walikua wanazikomalia saaaaaaanaaaaaaaaaaa.
 
09asiraaa.jpg

Thursday, 07 July 2011 11:16
0diggsdigg


Leon Bahati, Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wassira, amelishambulia gazeti hili akisema linaandika habari za uchochezi.


Kadhalika, Wassira alisema: "Juzi alikuwepo Mheshimiwa Edward Lowassa, akatoa maoni yake kama Mbunge tu wa Monduli, gazeti hili la Mwananchi linasema; “Vita ya Lowassa, Serikali ya JK sasa wazi’ Vita gani? Ipi?
Hawa ni wachochezi na gazeti hili lina asili ya nje."

Kauli ya Makinda
Akizungumzia malalamiko ya Wassira, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema yako mengi ambayo vyombo vya habari vinakosea katika kuripoti.

"Juzi tulicheza dansi na Tundu Lissu, wakasema mnaona hawa, niko kwenye gazeti mojawapo,
sasa mtu wangu mmoja alikuwa anawasikiliza akaniambia aliwasikia wanasema ‘unawaona hawa waongo kabisa hawa, kila siku anamwambia kaa chini, kaa chini, sasa unawaona wanachokifanya hapa,"alisema.


Nyekundu: Wassira pamoja na serikali yako hamliwezi gazeti hilo...unadhani wamiliki wake wanatokea Kenya, mmiliki wake ni Aga Khan..kipindi kile cha uchaguzi si mlilitishia nyau tena gazeti hilo?!? Jaribuni kulifungia gazeti hilo sasa na mwone matokea yake!!! Acha Mwananchi lifanye kazi yake bana..husilete ukurya wako hapa alaa!!! Na bado picha utapigwa tu ukilala bungeni..bunge siyo zahanati au kituo cha afya alaa!!

Kijani: kumbe huyu mama ana wambea wake ambao kazi zao ni kusikiliza watu wanamzungumziaje?!?! That is a sign of insecurity na lack of self-confidence!!! Nadhani hadi humu JF wapo...kama wapo karibuni sana..na mkamwambie huyo bosi wenu yale yanasemwa humu juu ya utendaji wake mbovu msimfiche kitu, mwambieni in black and white format!!
 
Back
Top Bottom